Uhujumu uchumi udom

Uhujumu uchumi udom

NJALI

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2014
Posts
1,534
Reaction score
1,090
Hivi wanajanvi chuo kikuu cha Dodoma ni cha serikali au cha mtu binafsi? Maana miaka mitatu mfululizo wanafunzi wanao hitimu UDOM wanadhulumiwa pesa za majoho. Tangu 2011-2013. Mwaka jana tuliambia tuchangie 55,000= kwa kila muhitimu kama gharama ya joho ambapo ukirudisha joho unarudishiwa 20,000= lakini hadi sasa pesa hiyo hajapewa licha ya kuwaachia namba zetu za akaunti kama walivyo dai uongozi wa chuo. Je huu ni wizi, utapeli au dhuluma? Je serikali inajua hili? Je hawa viongozi wa Udom wanafaa waendelee kuwepo? Je Serikali ikilaumiwa kwa hili itakuwa nongwa?
 
Tatizo lililopo UDOM ni lile la kupeana kazi kindugu. Mfano ni huyu mbilikimo prof Mlacha ambaye amekuwa akilalamikiwa mara kwa mara lakini hakuna hatua inayochukuliwa. Kwahiyo hata haya malalamiko yako mkuu yataishia hapahapa. Mana mkuu wa kaya mwenyewe analijua hili kwa vile ana ughusiano wa karibu na prof Mlacha.
 
Wapo waliorudishiwa elfu 20 zao ingawa kwa kuchelewa so be patient...
 
Hivi Vyuo siku hizi ni kama magenge ya wahuni flan kuanzia Serikali za wanafunzi ni upuuzi mtupu kazi yao kuganga njaa kutwa kupanga mipango ya kupinduana badala ya kushughulikia matatizo ya wanafunzi, mi nilipokuwa Rais nilikaribia kununua bastola kwa sababu ya maudhi kuanzia Spika wa Bunge mpaka Menejimenti ya Chuo ni usaliti mtupu!. Hivi hizi fedha za majoho kwanza kuna ulazima gani wa wahitimu kulipia fedha yote hiyo?, afu bado mpaka chenji wanaiba!. Huu ni wizi kama wizi mwingine na kwa kweli Prof. Mlacha ni mwizi sugu na huwa najiuliza hivi asingesoma huyu jamaa angekuwa jela kwa wizi hakyamungu.
 
Hv joho la kutumia siku moja tu kanini lilipiwe zaidi ya 40000?
 
ndo mana products zenu huku mtaani wanatiliwa shaka kwa sababu mambo mengi yanaendeshwa kisiasa,karibu UDSM hutakuta upuuzi huu hata siku moja
 
Hata UDSM siasa ipo sema kwamba inatofautiana magnitude tu. Hakuna chuo au taasisi ya serikali isiyo athiriwa na siasa katika nchi hii hata jeshini siasa ipo sembuse UDSM?
 
Hata UDSM siasa ipo sema kwamba inatofautiana magnitude tu. Hakuna chuo au taasisi ya serikali isiyo athiriwa na siasa katika nchi hii hata jeshini siasa ipo sembuse UDSM?
Mada mezani ni wizi wa UDOM, siasa inaingiaje hapa? Au siasa kwako ni wizi ni wizi ni siasa? Ndio maana mnaibiwa kwa sababu ya kushindwa kupambanua mambo
 
Hv joho la kutumia siku moja tu kanini lilipiwe zaidi ya 40000?

Hata mimi,hili huwa linanishangaza joho siku moja 40,000???,chakushangaza zaidi hata wasomi wetu hawalioni hili,sijui mama na bibi zetu wa Mangaka na Kiomboi kule,wanaweza ng'amua kupanda kwa bei ya umeme!!
 
Dawa na nyie mkipewa hayo majoho poteeni nayo tu sio kulia lia kila siku, maana gharama ya hayo majoho itaji offset na fedha wanazowadhulum baaaaassss
Thubutu! Ukiondoka na joho utapata shida kila siku wanadai elfu kumi hivyo ukija kuchukua cheti utalipa kama m hivi! Wao kwa pesa wako choncho kama ma bamaid.
 
Kuna watu walisoma pale wameenda kuchukua vyeti wamebambikiwa madeni ni hakuna wanaambiwa wajaze upya clearance form wamekaa huko wiki nzima, mpaka wakaenda kwa mkuu wa chuo ndo akawaamuru wawapatie vyeti vyao na hapo wameishalipa madeni na ada ambayo wanasema bodi ya mikopo haikuwapatia, mpk aibu!
 
Chochote kinachosemwa kuhusu UDOM siwezi kubisha hata wakikiita chuo cha mtaa sio kata tena sibishi ni kweli. Maana mambo yanayofanyika hapo chuoni huwezi amini kama kuna maprofesa na madokta hapo wana vyeo lakini ndio hovyo kabisa bora hata na darasa la saba anaweza kutumia akili. Mimi nahisi hata hizi thesis zinawachanganya cognition na kuwa watu wa ovyo ovyo.
 
Hata UDSM siasa ipo sema kwamba inatofautiana magnitude tu. Hakuna chuo au taasisi ya serikali isiyo athiriwa na siasa katika nchi hii hata jeshini siasa ipo sembuse UDSM?

unahisi ila huna uhakika,huku UDSM hakuna upuuzi kama wa chuo chako cha kata-UDOM
 
unahisi ila huna uhakika,huku UDSM hakuna upuuzi kama wa chuo chako cha kata-UDOM

Unachosema ni kweli UDSM kunawashikaji zangu kibao wamepiga pale bachelor lakini sijawahi kusikia wakilalama kudhulumiwa pesa za majoho, kusingiziwa madeni wakati wa kuchukua vyeti,kudhulumiwa special faculty. N.k. Kwa udom yote hayo huenda pamoja, ukisoma udom tegemea lolote linaweza kukutokea. Tumetangaziwa tukachukue transcripts 8/1/2014 tulipofika tunaambiwa havijawa tayari, hadi sasa 16/1/2014 college of education hatujapewa! Watu wanaishi gesti kwa zaidi ya wiki nzima na hawana hakika watapewa lini. ONLY UDOM
 
Mi nimemaliza mwaka 2011 huwezi amini mpaka leo hela yangu nimedhulumiwa,hii ni hatari sana hawajua hata hela yenyewe niliipataje mbu.zi wale....!!Acha waendelee na michezo yao nmichafu one day they will pay for that am sure.Wanafikiri hii nchi ya baba yao kila siku
 
Back
Top Bottom