Hivi wanajanvi chuo kikuu cha Dodoma ni cha serikali au cha mtu binafsi? Maana miaka mitatu mfululizo wanafunzi wanao hitimu UDOM wanadhulumiwa pesa za majoho. Tangu 2011-2013. Mwaka jana tuliambia tuchangie 55,000= kwa kila muhitimu kama gharama ya joho ambapo ukirudisha joho unarudishiwa 20,000= lakini hadi sasa pesa hiyo hajapewa licha ya kuwaachia namba zetu za akaunti kama walivyo dai uongozi wa chuo. Je huu ni wizi, utapeli au dhuluma? Je serikali inajua hili? Je hawa viongozi wa Udom wanafaa waendelee kuwepo? Je Serikali ikilaumiwa kwa hili itakuwa nongwa?