Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,362
- 48,879
Mara nyingi binadamu walio wengi, wanapoyasikia mabaya, kama hayawagusi moja kwa moja, ni rahisi kufikiria kuwa hayawahusu, na wale wanaopatwa nayo wanawaona ama ni wajinga ama hawana uthamani kama walio nao wao.
Leo hii, kama kuna mtu au anakuwa ametekwa au kukamatwa na vyombo vya usalama, unakuwa na uhakika wa karibu wa 70% juu ya anachokuwa ametenda, na utakuwa na uhakika wa zaidi ya 95% juu ya mashtaka atakayoshitakiwa nayo mahakamani.
Wahalifu wa kweli hawatekwi bali wanakamatwa au kutakiwa kuripoti Polisi. Lakini ukisikia ametekwa, unaanza kufuatilia ili kujua kama mtu huyo siku za karibuni aliwahi kuwakosoa watawala, serikali au vyombo vya usalama. Kama ametekwa:
1) Utakuwa na uhakika kama wa 70% hivi kuwa mtu huyo atakuwa amewakosoa watawala, vyombo vya dola au serikali
2) Kama atabahatika kufikishwa mahakamani, makosa atakayoshtakiwa nayo ni uhujumu uchumi na/au utakatishaji fedha haramu.
Mashtaka hayo yanamfanya mtuhumiwa kutopewa dhamana, na hivyo kukaa rumande wakati wote.
Waliotunga na kupitisha sheria ya kuwanyima dhamana watuhumiwa wa makosa hayo mawili, nina uhakika kuwa hawakufikiria kuwa kuna siku sheria hiyo itatumika kuwatesa au kuwakomoa watu wasio na makosa.
Watunga sheria waliamini kuwa watawala watakuwa genuine, vyombo vya usalama vitakuwa genuine na mahakama pia zitakuwa genuine.
Hali ya sasa inatoa funzo kubwa kwa sisi sote, watunga sheria, wananchi wa kawaida na hata watawala wa sasa.
Sheria inayomnyima mtu haki ya dhamana kwa tuhuma yoyote ile ni mbaya kwa sababu kuna watu wanaweza kuitumia sheria hiyo vibaya kwa dhamira mbaya ya kutaka kuwakomoa watu ambao kisheria hawajatenda makosa ya jinai.
Ni wakati sahihi sasa wa kuifuta hiyo sheria kwa sababu inatoa mwanya kwa vyombo vya dola na watawala kuitumia vibaya tofauti na ilivyokusudiwa.
Sheria hii mbaya ya kuwanyima watuhumiwa dhamana, kama itaendelea kuwepo, hata wanaoitumia leo, kuna siku itawageuka, na watajutia kwa nini walipokuwa kwenye nafasi za kuifuta hawakuchukua hatua.
Sheria hii kama itaendelea kuwepo, hakika nawaambieni kuna siku, baadhi ya wenye mamlaka leo, iwe ni wakuu wa mikoa, wilaya, mawaziri, polisi, usalama wa Taifa na hata wanajeshi, watauona na kujutia ubaya wake.
Leo ninapoyanena maneno haya, kuna wengi watayaona ni maneno ya kijinga kutoka kwa mtu mjinga asiye na mamlaka kwa sababu leo wapo kwenye nafasi ambazo, kauli zao tu, mtu anafurahi au kuumia, awe anastahili au hastahili.
Wanachosahau ni kuwa mamlaka hayo siku nyingine hayatakuwa mikononi mwao, na wengine watayatumia dhidi yao.
Ukiwa na nafasi yoyote iwe ya kuongoza, kutawala au kusimamia, ufahamu kila tendo unalolitenda kwa dhamira mbaya, litalipwa kwako kwa namna tofauti, kama siyo ya moja kwa moja kwako, itakuwa kwa mtu wa karibu yako ambaye akitendwa, utaumia kama Mfalme Daud alivyoumizwa na mateso na kifo cha mwanae ambaye alikuwa zao la uovu, japo mtoto hakuwa ametenda uovu wowote.
''Ni kwa njia hii, Mungu aliupenda Ulimwengu, hata akamtoa mwanae wa pekee ili Ulimwengu wote upate kuokoka''. Watawala na wenye mamlaka, mnatoa nini kwa watu mnaowaongoza? Mnawapa upendo badala ya chuki? Mnawapa msamaha badala ya visasi? Mnawapa ulinzi badala ya kuwateka? Na mimi kama raia wa kawaida, ninawapa nini wananchi wenzangu?
Ni tafakari ya Noeli. Kristo ni upendo. Azaliwe kwenye mioyo yetu. Azaliwe kwenye mioyo ya watawala. Afute roho za unafiki na hila maana yeye ni Kweli ya Mungu toka kwa Mungu.