Tindo
JF-Expert Member
- Sep 28, 2011
- 63,730
- 111,542
Sheria ni msumeno mkuu
Unapotaka kupambana na serikali yoyote duniani hakikisha kuwa ni msafi na huachi alama yoyote chafu
Tetea uovu maana uko kwenye meza ya mfalme unakula na kusaza.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sheria ni msumeno mkuu
Unapotaka kupambana na serikali yoyote duniani hakikisha kuwa ni msafi na huachi alama yoyote chafu
Acha kulia lia kama mwanamke,jikite kwenye sheriaTetea uovu maana uko kwenye meza ya mfalme unakula na kusaza.
Acha kulia lia kama mwanamke,jikite kwenye sheria
Si kwweli pia serikali safi huwa hazina wakosoaji ni tawala dhalimu tuSheria ni msumeno mkuu
Unapotaka kupambana na serikali yoyote duniani hakikisha kuwa ni msafi na huachi alama yoyote chafu
Dpp msukuma unategemea amuangushe ndugu yakeWakati huo huo mahakama nazo hazishinikizi kwa watawala kuharakisha upelelezi!
Mtu anaendelea kusota ndani kwa kukosa dhamana, miaka na miaka!
At the end utatoka tu hata ukifungwa 100Lengo la hizo kesi ni kukukomoa sio kwamba wanakesi ya kukufunga maana wanajua miaka mi3 mahabusu ukitoka kichwa kimevurugika
Sent using Jamii Forums mobile app
Pana watu utembea gizani unawahurumia kesho yao,hakuna mwanadamu yeyote pasipokujali hadhi yake ajuaye kesho yake.Mwisho wao si mzuriWacha iendelee kuwepo ili iwakute hawa waliyoiweka. Ipo siku tu
Ni vizuri unavyojaribu kutoa maoni ambayo kwa hakika yana uzito. vile vile tujaribu kuangalia upande wa pili wa wakosefu. na jee mbona wewe upo njee. Zungumzia na wakosefu pia ili hoja yako iwe nzito vya kutosha. Mkosefu kioo chake ni mahakama, na kila ujuaji huzaa ujuaji. hili suala ni fikirishi kwa mwenye uelewa wa mahusiano ya jamii.Watawala wajue kuwa hata wakifanya mambo 1000 mazuri lakini wakafanya matendo 10 ya uonevu wa dola dhidi ya raia, yanafuta chochote kilichofanywa. Utakuja wakati ambao watu hawatataka hata kuvigusa vitu vizuri vilivyofanywa kwa sababu wataona ni kushiriki uibilisi.
Ni aheri kula mchunga ukiwa umekalia kigoda kuliko kula biriani ukiwa umekatilia michongoma.
Watawala wakitaka wanaweza kuendelea kuyaamini maneno ya wanafiki kuwa wananchi wanafurahia mambo yanayofanywa. Lakini ukweli ni kuwa ni awamu hii pekee watu wengi hawana furaha, wanaishi katika mashaka makubwa, siyo kwa sababu ni wahalifu bali ni kwa sababu mtu yeyote anaweza kufanywa kuwa mhalifu wakati wowote. Hali hii siyo ya kuikumbatia.
Mara nyingi binadamu walio wengi, wanapoyasikia mabaya, kama hayawagusi moja kwa moja, ni rahisi kufikiria kuwa hayawahusu, na wale wanaopatwa nayo wanawaona ama ni wajinga ama hawana uthamani kama walio nao wao.
Leo hii, kama kuna mtu au anakuwa ametekwa au kukamatwa na vyombo vya usalama, unakuwa na uhakika wa karibu wa 70% juu ya anachokuwa ametenda, na utakuwa na uhakika wa zaidi ya 95% juu ya mashtaka atakayoshitakiwa nayo mahakamani.
Wahalifu wa kweli hawatekwi bali wanakamatwa au kutakiwa kuripoti Polisi. Lakini ukisikia ametekwa, unaanza kufuatilia ili kujua kama mtu huyo siku za karibuni aliwahi kuwakosoa watawala, serikali au vyombo vya usalama. Kama ametekwa:
1) Utakuwa na uhakika kama wa 70% hivi kuwa mtu huyo atakuwa amewakosoa watawala, vyombo vya dola au serikali
2) Kama atabahatika kufikishwa mahakamani, makosa atakayoshtakiwa nayo ni uhujumu uchumi na/au utakatishaji fedha haramu.
Mashtaka hayo yanamfanya mtuhumiwa kutopewa dhamana, na hivyo kukaa rumande wakati wote.
Waliotunga na kupitisha sheria ya kuwanyima dhamana watuhumiwa wa makosa hayo mawili, nina uhakika kuwa hawakufikiria kuwa kuna siku sheria hiyo itatumika kuwatesa au kuwakomoa watu wasio na makosa.
Watunga sheria waliamini kuwa watawala watakuwa genuine, vyombo vya usalama vitakuwa genuine na mahakama pia zitakuwa genuine.
Hali ya sasa inatoa funzo kubwa kwa sisi sote, watunga sheria, wananchi wa kawaida na hata watawala wa sasa.
Sheria inayomnyima mtu haki ya dhamana kwa tuhuma yoyote ile ni mbaya kwa sababu kuna watu wanaweza kuitumia sheria hiyo vibaya kwa dhamira mbaya ya kutaka kuwakomoa watu ambao kisheria hawajatenda makosa ya jinai.
Ni wakati sahihi sasa wa kuifuta hiyo sheria kwa sababu inatoa mwanya kwa vyombo vya dola na watawala kuitumia vibaya tofauti na ilivyokusudiwa.
Sheria hii mbaya ya kuwanyima watuhumiwa dhamana, kama itaendelea kuwepo, hata wanaoitumia leo, kuna siku itawageuka, na watajutia kwa nini walipokuwa kwenye nafasi za kuifuta hawakuchukua hatua.
Sheria hii kama itaendelea kuwepo, hakika nawaambieni kuna siku, baadhi ya wenye mamlaka leo, iwe ni wakuu wa mikoa, wilaya, mawaziri, polisi, usalama wa Taifa na hata wanajeshi, watauona na kujutia ubaya wake.
Leo ninapoyanena maneno haya, kuna wengi watayaona ni maneno ya kijinga kutoka kwa mtu mjinga asiye na mamlaka kwa sababu leo wapo kwenye nafasi ambazo, kauli zao tu, mtu anafurahi au kuumia, awe anastahili au hastahili.
Wanachosahau ni kuwa mamlaka hayo siku nyingine hayatakuwa mikononi mwao, na wengine watayatumia dhidi yao.
Ukiwa na nafasi yoyote iwe ya kuongoza, kutawala au kusimamia, ufahamu kila tendo unalolitenda kwa dhamira mbaya, litalipwa kwako kwa namna tofauti, kama siyo ya moja kwa moja kwako, itakuwa kwa mtu wa karibu yako ambaye akitendwa, utaumia kama Mfalme Daud alivyoumizwa na mateso na kifo cha mwanae ambaye alikuwa zao la uovu, japo mtoto hakuwa ametenda uovu wowote.
''Ni kwa njia hii, Mungu aliupenda Ulimwengu, hata akamtoa mwanae wa pekee ili Ulimwengu wote upate kuokoka''. Watawala na wenye mamlaka, mnatoa nini kwa watu mnaowaongoza? Mnawapa upendo badala ya chuki? Mnawapa msamaha badala ya visasi? Mnawapa ulinzi badala ya kuwateka? Na mimi kama raia wa kawaida, ninawapa nini wananchi wenzangu?
Ni tafakari ya Noeli. Kristo ni upendo. Azaliwe kwenye mioyo yetu. Azaliwe kwenye mioyo ya watawala. Afute roho za unafiki na hila maana yeye ni Kweli ya Mungu toka kwa Mungu.
Kwa ujumla wabunge wengi wa CCM ni mzigo.Uta waambia nini wabunge wa Ccm wanao pitisha kila kitu kwa ndioo halafu ukimuuliza umeunga nini mkono hajui? Inatakiwa kuwe na bunge lenye wawakilishi serious sio wale wanao ongelea congo dust..
Sent using Jamii Forums mobile app
Sisi tunaitazama zaidi serikali na watawala maana hawa walistahili kuwa na hekima kubwa kwa vile waliapa kutumia hekima na kutenda haki wakati wote.Ni vizuri unavyojaribu kutoa maoni ambayo kwa hakika yana uzito. vile vile tujaribu kuangalia upande wa pili wa wakosefu. na jee mbona wewe upo njee. Zungumzia na wakosefu pia ili hoja yako iwe nzito vya kutosha. Mkosefu kioo chake ni mahakama, na kila ujuaji huzaa ujuaji. hili suala ni fikirishi kwa mwenye uelewa wa mahusiano ya jamii.
Asante sana elimu mkuuWatu wasio na hatia wanateseka. Leo watu wanashtakiwa kuhujumu uchumi wa nchi kwa sh 17m. Kule Segerea wapo watu 4 wanehujumu uchumi kwa sh 20m maana yake sh 5m kila mmoja. Hata makosa ya ukwepaji kodi ambayo yangeshughulikiwa na TRA, yanageuzwa kuwa uhujumu uchumi.
Mtu mmoja anapoonewa na kuteseka, kuna watu su chini ya 100 wanateseka moja kwa moja, na wengine si chini ya 100,000 wanajenga chuki dhidi ya watawala na vyombo vya dola.
Hakuna mahali popote Duniani, nguvu ya polisi au jeshi viliweza kuleta umoja wa wananchi. Tunawahitaji sana polisi, usalama wa Taifa na wanajeshi, kwa sababu hitaji la kwanza la binadamu yeyote ni usalama wake na mali zaje. Lakini vyombo hivi vikitumika vibaya huua umoja wa kitaifa na huweza kusababisha machafuko.