Uhuru bila mipaka ni vurugu, lakini mipaka kwenye uhuru ni udikteta

Uhuru bila mipaka ni vurugu, lakini mipaka kwenye uhuru ni udikteta

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2011
Posts
25,982
Reaction score
51,157
CCM hupenda kusema "uhuru bila mipaka ni vurugu" kuashiria kuwa hakuna uhuru usio na mipaka.

Na CCM hutumia msemo huo kuhalalisha matumizi ya nguvu dhidi ya wanaowapinga kisiasa.

Lakini CCM huficha sehemu muhimu ya msemo huo inayosema "mipaka kwenye uhuru ni ugandamizaji".

Dhana hizi mbili zinaonesha kuwa uhuru ndiyo kitu muhimu kuliko mipaka.

Mpaka huja pale uhuru wa mtu mwingine huanzia na siyo ndani ya uhuru wenyewe.

Kama kuna mtu ana uhuru wa kusema rais aongezewe muda wa kukaaa madarakani, mpaka utatokea pale atakapotaka jambo hilo litokee kwa kuvunja Katiba.

Na hata atakayesema Rais hafai aondolewe madarakani, naye atakuwa yupo sawa mpaka pale atakapotaka Rais aondolewe madarakani kinyume cha Katiba.

Kwa hiyo CCM wajue kuwa hawawezi kuweka mpaka ndani ya uhuru wa watanzania wa kufanya mambo yao.

Kuipinga na kuikataa CCM ni jambo ambalo limo ndani ya uhuru wa watanzania kufanya mambo yao. Kutaka watanzania wapate kibali cha kuikosoa CCM toka CCM, huko ni kuweka mpaka kwenye uhuru wa watanzania.
 
Back
Top Bottom