Elections 2010 Uhuru FM wachochezi

Elections 2010 Uhuru FM wachochezi

Gurudumu

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2008
Posts
2,349
Reaction score
264
Leo asubuhi hii mwanangu akiwa anachezea remote ya radio bahati mbaya akafungulia Uhuru FM. Wakipitia dondoo za magazeti ya chama (ya ccm, serikali, na yale ya mafisadi), mtangazaji wa kiume alisoma dondoo iliyosema "chadema wamwaga damu, watu tisa wakamatwa na polisi akiwemo mgombea wa chadema John Shibuda". Kisha yeye na mtangazaji mwenzake wa kike wakaendelea kutoa maoni yao juu ya taarifa hiyo kukashifu chadema (kinyume na maadili yao). Kisha akamalizia kwa kusama "Jana nilikuwa naongea na jamaa yangu mmoja akaniambia kwamba watu wengine wana uraia wa nchi mbili, Tanzania na Vatican".

Nilishutuka sana baada ya kusikia hayo maneno. Nikathani kumbe inawezekana radio hii ndiyo inayotumiwa na ccm kueneza propaganda za chuki, udini na ukabila?

Ni hatari sana kutumia vyombo vya habari kuchochea chuki na mgawanyiko wa uongo. Uhuru FM wamekuwa wakichochea chuki kwa muda gani sasa? Vyombo vya udhibiti vinachukua hatua gani?
 
Nimesoma sana gia za kuingilia za watu mbalimbali wiki hii.. this one will be the best of the best.. !!

Mkjj,
Are you serious?...au umeibiwa p/word yako!:A S 39:....i ddnt xpect this from especially you!

BTW, hukumu yao hawa ccm iko around the corner,...wanatapatapa, and they are finally doomed!
 
Mkjj,
Are you serious?...au umeibiwa p/word yako!:A S 39:....i ddnt xpect this from especially you!

BTW, hukumu yao hawa ccm iko around the corner,...wanatapatapa, and they are finally doomed!
All the years Mwanakijiji amekuwa mkosoaji wa CCM na jk wake si kwa sababu haipendi la hasha.
Tis man is progressive CCM na anatamani kizazi kipya cha watawala kiibukia kutoka ndani ya CCM na si nje ya hapo.
Lakini kama hakuwa anafahamu ni kwamba zile posts zake nyingi zimesaidia kuandaa kizazi cha viongozi nje ya CCM. na mwanasiasa wa kweli hawezi kujiunga na ccm ya sasa maana atakuwa anajipaka matope ugenini.

Lakini nachelea kumhukumu mpaka atueleze maana ya kauli yake hapo juu ingawa nimemwelewa tofauti mlivyomwelewa ninyi.
 
CCM nchi hii iko juu ya sheria. Kuanzia Rais hadi tarishi ni watawala. Sisi watawaliwa tunatazamwa kama raia wa daraja la chini na tumegeuzwa kama kandambili ambazo umuhimu wake ni kuzivaa unapoingia msalani na wakishamaliza haja zao hawahitaji hata kujua walikoziacha.
Uchochezi huo ungefanywa na gazeti au hata Redio binafsi wahusika wangeshafungiwa na kuburuzwa mahakamani. Jambo hili lingeweza kukemewa vyema na Tume ya Uchaguzi lakini itakuwa vigumu kwani ni wapiga zumari wanaolipwa na mchagua wimbo.
Hukumu ya CCM ni 31 Oktoba, ikitoka ikatambike maana watanzania tumechoka na dharau zao kwetu. Waseme watakavyo lakini safari hii hawatoki na hao watangazaji wachochezi wana nafasi zao kule De Haig Uholanzi wakatolewe ushamba na Kikwete wao aliyeunda Green Guards wa kuwafyeka wapinzani mapanga. Tanzania Bila ya Kikwete,CCM, Makamba, Kinana, Msekwa na ma Green Guards inawezekana - kila mtu atimize wajibu wake 31 Oktoba.
Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika.
 
Mkuu inabidi tuinyofoe madarakani ccm ndo tutakuwa tumeitendea haki tanzania
 
Jmani eeeh, tukumbuke 2 kile kibonzo cha KP!!!!!!!!! Ndo utajua ka Uhuru FM itakaripiwa au vipi?
 
Attachments

  • 9989199.jpg
    9989199.jpg
    48.4 KB · Views: 45
Uhuru FM Radio ya Chama unataka TCRA wafanye nini?
 
Pamoja na hayo yote, nadhani kuna sababu ya kufanya ufuatiliaji uchochezi huu wa uhuru fm ili
kama mambo yatakuja kwenda ndivyo sivyo (siombei), tuweze kuwawajibisha.
 
Ni wakati muafaka wa kuanzisha chombo makini cha kukagua Integrity ya watangazaji na wahariri wa taasisi zote za habari nchini Tanzania.
 
Mkjj,
Are you serious?...au umeibiwa p/word yako!:A S 39:....i ddnt xpect this from especially you!

BTW, hukumu yao hawa ccm iko around the corner,...wanatapatapa, and they are finally doomed!
Hapana: Mwanakijiji; ameongelea Gia Ya Kuingilia: Gurudumu ameanza ile report vizuri (according to Mkjj): Gia/Gear; how you start your story; and your audience or readers will get it and assimilate it/shauku ya kuisoma: "Leo asubuhi hii mwanangu akiwa anachezea remote ya radio----" was the best gear. Mkjj ni mwandishi; hiyo ni taluma yake-------- tumpe heshima yake kwa kusoma in between the lines----!
 
Back
Top Bottom