Gurudumu
JF-Expert Member
- Feb 5, 2008
- 2,349
- 264
Leo asubuhi hii mwanangu akiwa anachezea remote ya radio bahati mbaya akafungulia Uhuru FM. Wakipitia dondoo za magazeti ya chama (ya ccm, serikali, na yale ya mafisadi), mtangazaji wa kiume alisoma dondoo iliyosema "chadema wamwaga damu, watu tisa wakamatwa na polisi akiwemo mgombea wa chadema John Shibuda". Kisha yeye na mtangazaji mwenzake wa kike wakaendelea kutoa maoni yao juu ya taarifa hiyo kukashifu chadema (kinyume na maadili yao). Kisha akamalizia kwa kusama "Jana nilikuwa naongea na jamaa yangu mmoja akaniambia kwamba watu wengine wana uraia wa nchi mbili, Tanzania na Vatican".
Nilishutuka sana baada ya kusikia hayo maneno. Nikathani kumbe inawezekana radio hii ndiyo inayotumiwa na ccm kueneza propaganda za chuki, udini na ukabila?
Ni hatari sana kutumia vyombo vya habari kuchochea chuki na mgawanyiko wa uongo. Uhuru FM wamekuwa wakichochea chuki kwa muda gani sasa? Vyombo vya udhibiti vinachukua hatua gani?