Uhuru Hospital Mwanza, mmiliki ni kijana chini ya miaka 40. Tupe ujanja ulifikaje huko?

Uhuru Hospital Mwanza, mmiliki ni kijana chini ya miaka 40. Tupe ujanja ulifikaje huko?

Kwa hiyo barabara ya Uhuru kama unaelekea Mlango Mmoja vipo jirani na Nyegezi karibu kabisa na kambi ya jeshi?

Huo mtaa wa mkanyenye ndipo hospital ilipo nadhani pamekuwa padogo make panebanana ni kweli hata packing ni ndogo mno kwa hiyo pale Esien eneo lile ni kubwa na panafaa pia
 
Huu msemo mie naona huwa ni kujifariji tu!unanikera mno huu msemo!endeleeni kujipa moyo!
Sijui nani aliuleta!....
Hapa ndo huwa nayaheshimu mashairi ya mwanafalsafa kutoka wimbo wa we endelea tu;"Sikiliza waliofanikiwa,ongeza zako mbayu wayu!"
 
Kuna wazee wana MZIGO sema hawana pa kuuweka, inaonekana Dogo alimsomesha DON akamuelewa na kuivest MZIGO kwenye Project ya Hospital.
 
Hiyo Uhuru dispensary iko eneo gani Hapa mz?
Si zahanati bwana! ni hospitali kubwa kubwa. Hata marehemu Kibonde alivyoanza kuumwa akiwa kule Kagera kwa akina Ruge walianza kumfikishia hapo kabla ya Bugando
 
Kwa mara ya kwanza nilimsikia kwenye semina za fursa za clouds. Anaitwa Dr. Derrick.

Kwa jinsi anavyoongea, ni kama kwamba ni kwa vile ana uwezo mkubwa wa kuona fursa na kuchukua hatua na kwa akili na maarifa aliyo nayo, ameweza kufika hapo.

Pia nilimsikia akisema zipo fursa za wadau walio tayari kutoa mitaji kufadhili miradi iliyobuniwa, lakini watu wenyewe, ndio hawapo wanaobuni miradi.

Napenda kujua mwekezaji huyu alianzaje hadi kufika hapo?

Najiuliza mimi mtoto wa mkulima nimalize kozi ya udaktari na kwa miaka isiyozidi sita naweza kuwa na mtaji wa kuanzisha Hospitali?
Naamini kila kitu ni malengo na uthubutu. Plan iwe nzuri ila kuepuka kuanguka kunakokatisha tamaa.
 
Back
Top Bottom