Uhuru Kenyatta achagua baraza jipya la mawaziri

Uhuru Kenyatta achagua baraza jipya la mawaziri

Saitoti alikuwa anataka kugombea urais ama kumuunga mkono Raila na kwasababu alikuwa very powerful than Uhuru Kenyatta ilikuwa hakuna njia nyingine lazima afanyiwe mambo yaleeee.

Naona bado hujapatia siasa za Kenya, Saitoti alikua powerful than Uhuru? Kwa watu ambao ingekua wanauawa kwa ajili ya umaarufu, basi Saitoti sio mmoja wao, hakua na umati au wafuasi. Kenya kuna watu wenye wafuasi sio mchezo, akilisema linafanyika kwa mfano huyu Raila kuna wafuasi wake huwa tayari kufia mbali kwa ajili yake.
 
Mimi napenda sana siasa ya Kenya 2022 kuna possibility kubwa NASA na KANU wakaungana kama Jubilee watamsimamisha Ruto. Kura za Rift valley itagawanyika mara 2 hapo ndipo uwezekano wa Ruto kuwa Rais utakufa

Ndio maana nikasema huzijui siasa za Kenya, yaani Ruto agombee urais halafu kura za Rift Valley zipasuke, hivi kaka umeamkia mbege asubuhi. Labda uniambie KANU wakiungana na NASA, halafu viongozi wa NASA wote kwa pamoja wamuunge mkono Gideon Moi, hapo sasa nitakuelewa, ila hilo haliwezekani maana hao NASA wote wanataka urais 2022 na kila mmoja ameahidiwa hilo na Raila, sasa kuwashawishi wasitishe na kumuunga mvamizi ambaye hakua nao tangu mwanzo, ni ndoto za alfu ulela.
 
Inamuondolea sifa ukiwa na mtazamo chanya, lakini Afrika watu wenye sifa za ufisadi ndio hupendwa sana. Ilmradi jina lako linatajwa tajwa na kuanikwa kwenye vyombo vya habari, hiyo imetosha.
Japo pia hamna kiongozi msafi hapa Kenya, wote mafisadi lakini wana wafuasi ambao huwambii kitu, hebu leo rais Uhuru adiriki kumfuta huyo Ruto ndio utajua kisa kilichomfanya chui awe na madoadoa, kwanza huko kuthubutu ndiko kulimharibia Raila maana alipogombana na Ruto akaishia maisha ya kwenye gizani na baridi.

Leo hii huyo Ruto ndiye ngao ya rais Uhuru, kwa kweli nakiri kwamba isingekua Ruto, Raila angeingia ikulu tena asubuhi saa nne. Lakini Raila akiwa waziri mkuu kwa unafiki akajifanya kupigana na Ruto kisa ufisadi (ilhali Raila mwenyewe mfisadi mkuu na amezungukwa na mafisadi wakubwa), sasa alimfuta kazi na kumuondolea nje nje, Ruto akacheza high voltage politricks na leo yupo anakunywa chai ikulu kama naibu wa rais.

Ruto amekua anatumia raslimali za serikali kujiandalia mazingira ya kuingia ikulu kama rais kwenye uchaguzi ujao, amekusanya viongozi wake, hata gavana wa Nairobi bwana Mike Sonko ni kibaraka wake, aliwafadhili viongozi wengi sana hata mkoa wa kati ambao huko ni mfupa uliomshinda fisi. Nilishangaa sana juzi bibi yangu kijijini anasema bora afe kwenye foleni lakini lazima ampigie Ruto kura.

Jamaa ni mjanja sana kisiasa na hili nalisema bila kutetereka yeye ndiye atakua rais baada ya Uhuru, labda Mwenyezi Mungu amchukue, lakini kama bado yupo hapa, hatuna jinsi, bora tujiandae tu kwa urais wake. Japo ni mzuri kiutendaji lakini mfisadi vibaya sana, yeye hunyakua bila kujali chochote, yeyote, au lolote.
Watamtungua kwenye helicopter km wengne
 
Yaani ukiwa adui wa Ruto kisiasa wewe kwishney! Huyu mlokole anasa zake ni kuchapa tu karata za kisiasa. Hana time ya kujivinjari na Tusker baridi kama kina Raila, Mudavadi na Wetangula. Wanasiasa wenzake wanamuogopa kwasababu hawamuelewi. Cheki alivomnasua mwenzake Issack Rutto kule Bomet. 2022 hamna cha kubishana, kwa Ruto itakuwa ni 'walkover' tu hadi ikulu.
 
Mimi napenda sana siasa ya Kenya 2022 kuna possibility kubwa NASA na KANU wakaungana kama Jubilee watamsimamisha Ruto. Kura za Rift valley itagawanyika mara 2 hapo ndipo uwezekano wa Ruto kuwa Rais utakufa
Ata wakiungana na servers zinakuwa controlled na Jubilee ni upuuzi.
Ikumbukwe RAILA hajawahi kushindwa since 2007.
Date 26 october iliwafungua watu wengi macho.
 
Ata wakiungana na servers zinakuwa controlled na Jubilee ni upuuzi.
Ikumbukwe RAILA hajawahi kushindwa since 2007.
Date 26 october iliwafungua watu wengi macho.
Eti nini? Hata uongo usemwe mara hamsini kamwe hutobadilika, utabaki uongo tu. Ukweli ni kwamba wakenya tulimkataa kata kata huyo chizi. Endeleeni na kelele zenu sisi tutaendelea tu kuchapa kazi. 2022, inshallah wembe utakuwa ni ule ule.
 
Uliomba utajiwe hesabu za makabila ndani ya mawaziri wa Uhuru, huyo naye akakupa changamoto kwamba uanzie nyumbani, maana sizonje kapendelea kwao kwa Wasukuma
Basi sawa, ngoja mleta hoja anisaidie kuwabaini.
 
Rais Uhuru Kenyatta ametangaza baraza jipya la mawaziri leo Ijumaa ya leo jioni

Rais huyo amewabakisha mawaziri 6 na kuwaondoa 13, moja ya mawaziri wapya ni aliyekuwa mwendesha mashtaka mkuu wa serikali Keriako Tobiko.

==================================================
View attachment 669245

President Uhuru Kenyatta has unveiled his new Cabinet.

In an address to the nation Friday, President Kenyatta retained Cabinet secretaries Fred Matiang’i (Interior), Charles Keter (Energy), Najib Balala (Tourism), Henry Rotich (Treasury), Joe Mucheru (ICT) and James Macharia (Transport).

He appointed new Cabinet secretaries who include Director of Public Prosecution Keriako Tobiko, former Marsabit governor Ukur Yatani and former Turkana Senator John Munyes.

Former Nakuru Governor Kinuthia Mbugua replaces Lawrence Lenayapa as State House Comptroller. Mr Lenayapa has been appointed Kenya ambassador to Netherlands.

In changes in the National Police Service, President Kenyatta dropped Ndegwa Muhoro as Director of Criminal Investigations and George Kinoti appointed to the position in acting capacity.

Mr Joel Kitili and Samuel Arachi were also dropped as heads of Kenya police and Administration Police and were replaced by Mr Edward Njoroge Mbugua and Mr Noor Gabow
Mbona akina herufi O hawamo ktk uteuzi huo?
 
Kenyatta hawezi hilo, Kenya huwa pagumu sana kutawala kimabavu, leo hata urais wa Kenyatta haujatulia maana Odinga anamchokonoa sana.
Hata Uganda palikuwa pagumu sana, lakini kwa nguvu ya jeshi palilainika kama mkate
 
Back
Top Bottom