joto la jiwe
JF-Expert Member
- Sep 4, 2017
- 26,117
- 46,617
Wakati wakenya waliendelea kubebeshwa mzigo wa kodi, WB ikiwakataza wahisani kuikopesha Kenya kutokana na deni kubwa la Kenya lisilolipika, rais wao ameendelea kufanya safari za kifahari zisizokua na umuhimu wowote kwa uchumi wa Kenya.
Ni hivi majuzi tu, Uhuru alimaliza ziara yake katika visiwa vya Jamaica na Visiwa jirani kwa kutumia ndege ya kukodi ndogo Gulf stream G650. Hii ni miongoni mwa ndege ghali sana duniani kukodisha au kununua.
Kama vile haitoshi, Uhuru Kenyatta ameamua kukodisha dege kubwa la kifahiri Aibus series yenye uwezo wa kubeba watu 150 kwa kawaida, kwa gharama ya $370,000 kwa siku, kwenda Japan na baadae Urusi, ambako marais wa Afrika walikutana na rais wa URUSI.
Safari hii alikodi kwa muda wa siku 10 na kufanya gharama kufika takriban $3.7M, usafiri pekee. Zaidi ya 80% ya marais wa Africa waliohudhuria mkutano huo walitumia ndege za Abiria, isipokua Museven aliyetumia ndege yake G500, na rais wa South Africa, aliyetumia ndege yake.
