Uhuru Kenyatta aonesha ustaarabu wa hali ya juu

Naona huyu mkulu wa lile taifa kusini mwa taifa langu amebandikwa majina mengi, si mchezo!



Napita tu.
 
Kiongoz bora anachukua hatua zilizo bora, Uhuru anajua mambo. Ukiwa Kiongoz mkubwa lazma challenges zkupate na uelewe sio kila raia atakukubali. Namfananisha na LOWASSA. alisemwa vibaya lakin still yet alijua nn maana ya siasa. Sio hii mijitu ukiongea kdogo tu ndani, hata useme ukweli ndani, halafu mnasema tuna Demokrasia. Hamna lolote!!!
 
Huyo mama angejaribu kipindi cha Arap Moi aone kama asingepotezwa Mara moja.
 
Nakubaliana na wewe kwamba yeye ndio mshindi, lakini ikumbukwe kuna sehemu nyingine ukiona moshi unafuka unaumwagia maji hapo hapo ili usije ukabadilika na kuwa moto mkubwa. Wakati mwingine umesema "ah ..acha tuu moto uwake maana sio mkubwa wa kutisha". Katika hili Kenyatta hana haja ya kulikuza ndio ODM wavune wafiasi. Lakini huko huko Kenya kuna vijana mablogger ambao wako jela kwa kumtukana Kenyatta, kwanini wako jela, kwasababu ni rahisi kumdhibiti mbunge au mwanasiasa kuliko kumdhibiti mwananchi wa kawaida. Kenya ipo kwenye harakati za uchaguzi, hakuna mwanasiasa mwenye akili timamu atamfunga mwanasiasa mwenzake wakiwa karibu na uchaguzi. Hata hapa Tanzania, nakuhakikishia ikifika wakati wa karibia na uchaguzi hautaona mwanasiasa yoyote anamsukuma mwenzake jela labda kama kufanya hivyo itamuongezea mwingine kura. Lakini if your high on opinion polls, why mess things up kubabaishana na vidagaa. Kumbuka Hillary was up in polls, wala hakumjibu Trump maswali yake aliyokuwa anamuliza, polls zilipo kuwa neck and neck, ndio vya chini ya kitanda vikatolewa (voice recording).
I think we haven't seen the worse of this Kenya upcoming election, big things will come tuwaombee wasichafuane, because we have 99 problems in EA, we don't need another one.
 
Ukitaka kujua uchungu wa tusi na umuhimu wa heshima na adabu, atukanwe baba yako au Mama aliekuzaa na mtu wa barabarani . Hapo ndipo utakapoelewa uzito wa neno kuvunjiwa heshima.
Katika demokrasia lazima kuwe na kuheshimiana hakuna demokrasia ya kukashifiana au kutukanana yule mama ata yeye akitukanwa katika Jimbo Lake na wapinzani wake hawezi kuvumilia naomba atokee mkenya mmoja, katika kikao cha huyo mama amkosoe kwa kukashifu tuone kama atavumilia.. Africa tunaacha kukosoana kwa Hoja tunabaki katika matusi
 
Ila moyoni atakuwa ameumia balaa na si ajabu moyo unawaka kulipiza kisasi ama cha kisiasa ama vinginevyo.

Na ni kweli kumporomoshea matusi rais namna hiyo ndiyo uhuru wa habari na demokrasia? Unajua kuwa hata kule Marekani mbunge hawezi kumtukana rais namna hiyo? Hatuwezi kuwa na demokrasia yenye heshima na kuhojiana vyema?
 
Ni sawa na kumkuta mkeo na mwanaume room, then ukavua viatu na kwenda living room kuangalia tv.
 
Tena hapo huyo mama akutane na muuza juisi barabarani, ampe matusi mazito mawili matatu tu juu ya namna alivyovaa na sura yake ilivyo mbaya etc, mbele ya mumewe na watoto wake huku wapita njia wakiona uone atakachokifanya. Tena utasikia, kamdhalilisha sana kwa vile ni mwanamke na huyo muuza juisi anaweza hata kupotelea jela msimsikie tena.
Watu wanachukulia haya mambo kishabiki tu, lakini ukweli unabakia palepale kuwa Demokrasia bila mipaka inaweza kuchochea uvunjifu wa kanuni muhimu zinazolinda ustaarabu wetu kama wanadamu.
 
Na usishangae anamlia timing tu na yeye ampe discipline kivingine.
 
Na usishangae anamlia timing tu na yeye ampe discipline kivingine.
Ndo maana wakasema siasa ni mchezo mchafu. Hapa alichofanya Kenyatta ni kujipatia political points za bure lakini kisasi kwa huyu mama lazima kitakuwa kinaandaliwa!!!
 
Ndo maana wakasema siasa ni mchezo mchafu. Hapa alichofanya Kenyatta ni kujipatia political points za bure lakini kisasi kwa huyu mama lazima kitakuwa kinaandaliwa!!!
Ndiyo maana yake. Yeye mama kaamua kulipuka Uhuru akaona aplay cool kama vile hajachukulia kwa umakini hilo swala, lakini ni vigumu kujua anachopanga. Huwezi kumdhalilisha mtu mzima hadharani ukabakia hivihivi.
 
This is the gentle way of confronting your enemy!!!!!
 
Plenty propaganda and propagandist in this thread.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…