Uhuru Kenyatta atumia jeshi baada ya mgomo wa wafanyakazi JIA, lakini akitumia Rais Magufuli hapa kwetu ni dikteta!

Hata kikwete alitumia jeshi la polisi kutawanya maandamano kama hayo hatujawahii kumuita dicteta ila ili uitwe kiongozi dicteta tunsangalia mfululizo wa maamuzi na matendo yako ya kika siku kwenye utawala wako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna tofauti ya msukumo

Jeshi la Kenya limeingia kutokana na kwamba hakuna jinsi kupunguza athari za kibiashara. Airport ikiwa kama kitega uchumi muhimu kwa sector ya utalii (necessary) kulinda mapato ya serikari

JWTZ limeingia kuleta madhara kwenye biashara ambayo hawakuwa na ulazima. Korosho ikiwa kama commodity yenye kuipatia serikari mapato (unnecessary) kwenda kuvuruga mambo
 
kulinganisha kenya na Tanzania ni sawa na kulinganisha mwanamke na mwanaume? kenya wanaishi binadamu, Tanzania wanaishi maishi wanaotembea! jitu halijaongezewa mshahara MIAKA 3 kisha kila siku linaenda ofisini. ukiliuliza linakwambia limesoma?
Wewe ni maiti?mbona ufipa hamjengi ofisi lakini unazungusha mikono?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jeshi linakuwa tayari kufanya kazi ambazo vitengo vingine vimeshindwa. Je, Korosho zilishindwa kununulwa na mashirika husika?
Jeshi lingeenda Njombe wanakouawa watoto ningeelewa lakini Korosho?
 
kulinganisha kenya na Tanzania ni sawa na kulinganisha mwanamke na mwanaume? kenya wanaishi binadamu, Tanzania wanaishi maishi wanaotembea! jitu halijaongezewa mshahara MIAKA 3 kisha kila siku linaenda ofisini. ukiliuliza linakwambia limesoma?
Afu kuna watu wamelike

Huu ni ushamba, Kama wewe ni mtanzania na unaandika uharo huu, you are a fool wa kiwango cha stigila geji

Matusi yaaishie kwa serikali, kutukana wananchi kuwa ni wafu tutakuja tuoana utumbo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kabla ya kuandika jambo sensitive kama ulivyofanya inatakiwa
ufanye angalau kautafiti kadogo ili kujiridhisha na post yako. Wanaombapana na wafanyakazi wa JKIA siyo KDF bali ni Administration Police (AP) ambacho ni kikosi cha polisi chakawaida kitanachotumika kwenye utawala wa kila siku. Vikosi vingine maalum vya polisi ni General Service Unit (GSU) , Anti-theft squad, Anti-poaching squad, Anti-Livestock theft squad, Prisons, Traffic police e.t.c. hii taarifa yote inapatikana mtandaoni
 
hivi hata ile akili ndogo tu ya kutwazia huwa haioni namna nyingine.ya kufikiria kidongo mbali na kutawaza?ok hivi kwetu wakulima wa korosho waligoma au nyinyi ndo mmewazuia wafanya biashara kwa lengo la kuwakomoa wao na badala yake mmejikuta walioumia ni wakulima..jeshi kutoa msaada kama wa kitabibu au kujenga madaraja au kuongoza ndege au kwenda kuzima moto au kwenda kuokoa meli iliyozama kazi zote zilizotekea gafla bila kuwa na infuluence za kiongozi wa kisiasa dharura yoyote ile jeshi hutumika..hapo kwenye korosho na maduka ya kunadilishia pesa sio dharura hizo tunayatengeneza kitaalam ilibidi itatuliwe na waliotengeneza sio jeshi..ona sasa jeshi letu limeshindwa kubangua korosho kwa meno mmelidhalilisha jeshi na tqifa letu maana limeshindwa kazi lingefanikiwa sawa
 
Leo jirani yetu Kenya kumetokea mgomo wa wafanya kazi na Rais Uhuru Kenyatta akaamuru KDF kuingilia kati kwa kufanya shughuli zote baada ya wafanyakazi kugoma.
Hivi we una akili kweli?! Wafanyakazi wa airport, sasa wewe ulitarajia abiri wasihudumiwe?! Alichofanya Kenyatta kinafanyika duniani kote! At the time of emmergency, jeshi linaenda kufanya kazi za kiraia kwa kutoa huduma mbalimbali, na ndicho kimetokea pale airport! Kwamba, jamaa wameweka silaha chini wakaingia kaunta kuhudumia wateja!!

Huyo unayetaka kumtetea huwa anatumia jeshi kutisha wananchi! Kwa mfano, kule Arusha katumia jeshi kwenye Bureau De Change! Hivi kulikuwa na umuhimu wa kutumia jeshi dhidi ya viduka vya kubadilisha fedha? Hivi BoT wakiambatana na askari polisi wangeshindwa kufanya lile zoezi?
 
Kwetu hapa malalamiko haya yangekuwepo watu wagome na Rais aamuru jeshi kunusuru hii hali angeandikwa ni DIKTETA hilo halina ubishi.

Je, ingekuwa hapa kwetu stori zingekuwaje make huwa kuna malalamiko kwa kutumia jeshi kila wakati.

Kwetu Dollar ingepanda thamani......
Na Tsh. kushuka....
Na abiria wangerudishiwa Tiket(Kama Korosho vile zilivyorudishwa)...
 
Sababu za mcng za Uhuru ni zipi?Nachojua bavicha chochote afanyacho Kenyata ni dhahabu na afanyacho jpm ni kibaya hata kama vinalingana.

The problem with the world is that the intelligent people are full of doubts, while the stupid ones are full ofconfidence.
 
Kulikua na umuhim wa kuleta wenye uniform?Kama ni walewale kwanini wasingevaa kama wanavyovaa siku zote?Ingekua Tanzania si tungesema jamaa anawatisha wananchi na porojo kibao sana?

The problem with the world is that the intelligent people are full of doubts, while the stupid ones are full ofconfidence.
 
kulinganisha kenya na Tanzania ni sawa na kulinganisha mwanamke na mwanaume? kenya wanaishi binadamu, Tanzania wanaishi maishi wanaotembea! jitu halijaongezewa mshahara MIAKA 3 kisha kila siku linaenda ofisini. ukiliuliza linakwambia limesoma?

๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚umeua..na hakuna watu woga kama hao waserikalini jaman maoga kama mapanya
 
Maoni yake ni kwamba kuna watu wanajua waliotaka kumuua lakini wanajifanya hawawajui!!
Si aliwataja au kuna wengine tena?

The problem with the world is that the intelligent people are full of doubts, while the stupid ones are full ofconfidence.
 
Yaani kuna mambo ukiyaendekeza unaweza uka palalyse uchumi wa nchi,airport ni mpaka wa nchi,ni sura ya nchi,wakigoma wafanyakazi,ni tatizo kubwa,ila kwa Kenya,mahakama ilikuwa imezuia huo mgomo,
Harafu wanachogomba wafanyakazi wa airport,ni maamuzi ya serikali kutaka kubinafsisha shughuri za airport kwa Kenya airways,shirika ambalo,linamilikiwa kwa asilimia kubwa na watu binafsi,na kama unavyojua Kenya,Ufisadi ni balaa,hawa wakipewa wasimamie airport,watajari faida zaidi,na sio kuongeza nafasi za ajira.
Upuuzi kama huu wa Kugoma,hata Ulaya na America,wasingeweza kuvumilia.
Demokrasia iliwahi sana Africa,tungeenda kidikiteta zaidi,tukuze uchumi,then demokrasia ije baadae,lakini ukiruhusu udikiteta Africa,kuwapata watu kama Maghufuri,Mao se Tung,kiongozi wa Korea,ni vigumu sana,unaishia kuwapata majizi kama Bokasa,Mobutu,Mseveni,Husein Mubarak,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ