Kujiongeza sio lazima, haipo kikatiba na ni matakwa ya mtu binafsi. Wakati huohuo ni kulea ujinga kila mtu akishindwa uchaguzi anataka sijui ugatuzi, handshake, serikali ya pamoja na mambo ya kijinga kama hayo alafu asipohusishwa ananuna na kuandamana makusudi ili avuruge amani. Hiyo sio tamaa?
Hiyo 51% to 49% unayoona ni ndogo bado ipo kikatiba. Kwahiyo tuseme Wakenya walikosea walivyoandika katiba na kuweka kipengele hicho? Kwamba wangeandika ni lazima mahindi awe amepata zaidi ya 60% au kitu gani? 51% aliyopata Rais ipo kikatiba. Angeipata Odinga kama ni ndogo.
Mambo ya kugombea ukiwa na targets mbili ni wizi, ya kwanza ushinde Urais au ukikosa option ya pili uandamane ili upewe nafasi ya uongozi na kutajwa kwenye vyombo vya habari. Sio lazima, subiri uchaguzi mkuu ukishinda ukae na wapinzani mgawane wizara. Kama ndio staili yako