UHURU: Nimechaguliwa na wakenya, maoni ya wananchi siwezi kuyapuuza

Goliath mfalamagoha

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2012
Posts
602
Reaction score
2,506
UHURU: Nimechaguliwa na wakenya, maoni ya wakenya ni nguzo muhimu ktk uongozi wangu. Siwezi kuyapuuza.

JPM: Nilichukua fomu mwenyewe, kwa hiyo sipangiwi. Ukijaribu kunipangia ndio unaharibu kabisa.

UHURU: Nimefurahi kukutana na kaka yangu Raila. Tumeamua kuweka tofauti zetu kando kwa maslahi ya wakenya. Kenya ni kubwa kuliko sisi.

JPM: Mzee Lowasa amekuja kunipongeza kwa kazi nzuri ninazofanya. Mzee Lowassa ni mtu mwema, hakunitukana wakati wa kampeni. Wapambe wake ndio walionitukana lakini hakuwatuma. Kwani uliwatuma mzee? (Hapana, sikuwatuma).!

UHURU: Maandamano ni haki ya msingi ya wananchi wa Kenya. Serikali haitazuia maandamano yoyote ya amani. Nimemsikia IGP akisema waandamanaji hawana kibali cha maandamano yao. Nimemwambia Wakenya hawahitaji kibali ili kueleza hisia zao kwenye nchi yao wenyewe. Wanahitaji tu kutoa taarifa kwa polisi ili kupata ulinzi. Polisi hawaruhusiwi kuzuia maandamano, bali kuyalinda ili wale watakaofanya vurugu wakamatwe. Kwahiyo waliojiandaa kuleta fujo kwenye maandamano hayo watashughulikiwa.

JPM: Nasikia kuna maandamano. Waambieni waandamane waone. Kama kuna wajomba zao waliowatuma wataenda kuwahadithia. Mimi sijaribiwi.!

CHAKUBANGA: Hatuna la kujifunza Kenya. [emoji23][emoji28][emoji28]

Safari yetu ni ndefu utadhani hatutembei[emoji86]
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
UHURU: Katika Serikali "yetu tutafanya hiki na hiki"

JPM:Katika Serikali "yangu nitafanya hiki na hiki"

Mmoja anaamini katika Ushirikiano mwingine anamini katika Upekee.
Sisi ni maiti
Kazi ipo kwetu kwa jiwe mtetezi wa malaika hapangiwi wala hashauriki
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Kazi kubwa kuwa Mtanzania
Hizi komenti zimenichekesha na kuniliza
 
Naweza enda nchi yoyote africa mashariki bila paspot (kinyemela)?
 
Kwenye management, huyu wa pili kimsingi hajui chochote. To deliver you need strong teams not strong individuals.

Rais wetu anatakiwa kupata angalao basics za management. Hii ni nchi, inahitaji mchango wa kila mwananchi lakini mchango huo hauwezi kupatikana kama wananchi hawana ownership.

Sina uhakika, ninaposema wananchi wanahitaji kuwa na ownership, kama anaelewa.

Rais wetu asipobadili namna yake ya kuongoza, Taifa litakuwa limepata hasara kubwa. Na utawala huu utakuwa haujawatendea haki watanzania wa leo na vizazi vijavyo.
 
UHURU: Nimechaguliwa na wakenya, maoni ya wakenya ni nguzo muhimu ktk uongozi wangu. Siwezi kuyapuuza.

JPM: Nilichukua fomu mwenyewe, kwa hiyo sipangiwi. Ukijaribu kunipangia ndio unaharibu kabisa.

UHURU: Nimefurahi kukutana na kaka yangu Raila. Tumeamua kuweka tofauti zetu kando kwa maslahi ya wakenya. Kenya ni kubwa kuliko sisi.

JPM: Mzee Lowasa amekuja kunipongeza kwa kazi nzuri ninazofanya. Mzee Lowassa ni mtu mwema, hakunitukana wakati wa kampeni. Wapambe wake ndio walionitukana lakini hakuwatuma. Kwani uliwatuma mzee? (Hapana, sikuwatuma).!

UHURU: Maandamano ni haki ya msingi ya wananchi wa Kenya. Serikali haitazuia maandamano yoyote ya amani. Nimemsikia IGP akisema waandamanaji hawana kibali cha maandamano yao. Nimemwambia Wakenya hawahitaji kibali ili kueleza hisia zao kwenye nchi yao wenyewe. Wanahitaji tu kutoa taarifa kwa polisi ili kupata ulinzi. Polisi hawaruhusiwi kuzuia maandamano, bali kuyalinda ili wale watakaofanya vurugu wakamatwe. Kwahiyo waliojiandaa kuleta fujo kwenye maandamano hayo watashughulikiwa.

JPM: Nasikia kuna maandamano. Waambieni waandamane waone. Kama kuna wajomba zao waliowatuma wataenda kuwahadithia. Mimi sijaribiwi.!

CHAKUBANGA: Hatuna la kujifunza Kenya. [emoji23][emoji28][emoji28]

Safari yetu ni ndefu utadhani hatutembei[emoji86]

Kwa hiyo unalinganisha Wanaume ili iweje? Unataka Mshindi kati yao aje akuchukkuwe au vipi? Kwa maana nijuavyo mimi Wanawake ndo hufanya hivyo!
 
  • Thanks
Reactions: Oii
Kuishi Tanzania inabidi uongezee kwenye CV yako maana ni skill tosha hio
 
Back
Top Bottom