Uhuru off to the Hague with 120 strong entourage.

Hawa jamaa wanajua kweli kujichanganya. Angekuwa ni huyu wa kwetu Mr Fastjet hiyo Airport ingefungwa ili apite, as if kuna mapinduzi!!!


Sent from my iPhone using JamiiForums app

Mkuu genekai acha mzee! Mbona jamaa akienda huko majuu watu wanamkaushia kama hawamjui vile. Jamaa mbwembwe ni hapa tuu kule nadhani kuna wakati anapita kwenye scanner ili wamcheki.
 
Last edited by a moderator:
Uhuru Kenyatta ambae kwa sasa amekaimu Urais kwa William Ruto amewasili Hague jioni hii kwa ajili ya kesho kuhudhuria vikao vya kesi yake ICC. Alichowavutia wengi ni kwamba, amekwenda kule kama RAIA wa kawaida na sio kama RAIS wa Jamhuri ya Kenya. Hata ukiangalia namna alivyoondoka pale Kenyatta Int'l Airport ametumia sehemu ya abiria ya kawaida na hata msafara wake wakati wa kuelekea airport na alivyopokewa Uholanzi haukuwa na zile mbwembwe wanazopewa marais.
Mengi zaidi tutayajua kesho vikao vitakapo anza.
Source:Citizen Television.
 
ICC tayari kwa mkutano na Kenyatta











Kenyatta amemkabidhi mamlaka kwa muda naibu wake William Ruto kwa siku mbili atakazokuwa nje

Mahakama ya kimataifa ya ICC, inajianda kuwa mwenyeji wa mkutano maalum wa siku mbili kuhusu kesi ya Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ambaye atakuwa rais wa kwanza aliye mamlakani kufika mbele ya mahakama hiyo.

Kenyatta anakabiliwa na tuhuma za uhalifu dhidi ya binadamu anazodaiwa kutenda baada ya uchaguzi wa mwaka 2007.
Mahakama hiyo inasama kuwa Kenyatta alihusika katika kupanga na kufadhili ghasia za kikabila baada ya uchaguzi uliozua utata mwaka 2007/08
Zaidi ya wakenya 1,000 waliuawa kwenye gasia hizo.


Ruto ambaye ni rais kwa muda naye pia anakabiliwa na kesi katika mahakama hiyo ya

ICC
Mawakili wa Kenyatta wanasema kuwa kesi hiyo inapaswa kufutiliwa mbali kwa kukosa ushahidi.
Kenyatta ameombwa na mahakama hiyo kufika mbele yake ili kujadili malalamiko yaliyowasilishwa na kiongozi wa mashtaka Fatou Bensouda kwamba serikali ya Kenya imekataa kuwasilisha ushahidi unaohitajika katika kesi ya Kenyatta.

Majaji wa mahakama hiyo hata hivyo watathmini kauli kutoka kwa pande zote mbili.

Mkutano huo wa siku mbili unatarajiwa pia kutangaza tarehe ya kuanza kusikilizwa kwa kesi dhidi ya Kenyatta.
ICC imemtaka Kenyatta kujibu madai ya upande wa mashitaka kuwa Kenya inakataa kutoa ushahidi unaotakikana na mahakama hiyo.


Rais Kenyatta akikagua gwaride la heshima kabla ya kuondoka nchini kuelekea

Hague
Mwezi Septemba, mahakama iliahirisha kesi dhidi ya Kenyatta baada ya upande wa mashitaka kusema kuwa Kenya imekosa kutoa ushahidi unaotakikana na mahakama hiyo.
Mashahidi wa upande wa mashitaka wamejiondoa katika kesi hiyo.
Mamia ya wabunge wa Kenya wanatarajiwa kuambatana na Kenyatta kama ishara ya kumuunga mkono. Chanzo.BBC
 
Katiba yao inaruhusu Kukaimisha madaraka ya Urais.
 

na wale wengine? wamekwenda kama wabunge, wapambe, marafiki au raia wa kawaida?
 

Bush mbona hawajampeleka??
 
Kesi iishe tu jamani;
Mi napenda awe huru.
 
BRAVOooo MUGABEEEEE mugabeee "Un-touchable"
 
Kwani Uhuru hata hivyo ni raia tu wa kawaida, aende kwanza akasikilize kesi tujue kama anapatwa na hatia au laa!
 
Hawa jamaa wanajua kweli kujichanganya. Angekuwa ni huyu wa kwetu Mr Fastjet hiyo Airport ingefungwa ili apite, as if kuna mapinduzi!!!


Sent from my iPhone using JamiiForums app

With all due respect mheshimiwa, is there even contest in Africa, likija swala la kujichanganya na raia?this is JK's only strong point. I dislike the guy's leadership skills with passion, but i will never turn away to how civil and social the guy is. He is a very nice human being, what he does he does naturally, he is not forced, or doing it for PR. It's who he is. Bahati mbaya tu kwenye Uongozi hayuko vizuri. na wajanja wanatumia u-approachability wake kumuingiza mkenge kila dakika.
 
Did he have any other choice?

kwa mnaoijua katiba ya Kenya, anaruhusiwa kufanya hivi?What happens if he is to stay there for more than 2 days?lets say a week, will he automatically become president after the expiry of two days?or there will need to be a handover,signing from RUTO?did he need to do that?isn't it automatic that when president is not inside the country his second in command assumes his power?until he returns?au ndio mambo ya PR zilizopitiliza over non issues?
i see a precedent set in KENYA over this.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…