Uhuru una mipaka Jiheshimu Mkuu

Sawa Mkuu.

HILI BANDIKO LIMENIFANYA NIJUE NADILI NA WATU WA NAMNA GANI.
Unadili na watu wa aina gani?

Unakubali kwamba, ingawa inawezekana ni kweli inatubidi tufanye mazungumzo kwa staha fulani, kwa sababu bila staha yoyote tutatukanana na mazungumzo hayatawezekana, lakini pia, kuna mstari mwembamba sana kati ya kusisitiza staha na kuwanyamazisha watu wasitoe maoni yao kwa kutumia hoja ya staha?

Unakubali kwamba hoja za staha, kuheshimu dini, kuheshimu utamaduni wa Mtanzania, kuheshimu viongozi, kuheshimu wakubwa, etc., zinaweza kutumika kunyamazisha hoja muhimu tu ambazo zinapaswa kuzungumzwa kwa uhuru?
 
nachukia sana kuambiwa nimelamba asali
Usichukie. Pinga tu kwa hoja.

Kwa mfano. Mimi ikiwa nimetoa hoja ya kimantiki kusifia kitu, halafu akaja mtu kuni dismiss tu kwamba nimelamba asali, naweza kumwambia huyo mtu kuwa anafanya logical fallacy ya ad hominem.

Anaacha kujadili hoja, anamtukana mtoa hoja.

Hiyo ni dalili ya kukosa hoja.
 
Upo sahihi Mkuu.
 
inawezekana wew umeona ina mantiki, yeye kaiona kero na imemkera

kumbuka mazingira tunamoishi unaweza chukiwa au ukawa kero bila sababa ila imetokea tu
 
inawezekana wew umeona ina mantiki, yeye kaiona kero na imemkera

kumbuka mazingira tunamoishi unaweza chukiwa au ukawa kero bila sababa ila imetokea tu
Sasa hayo ni mapungufu yake, watu wengi wenye hekima wa JF wakipima kwa mizani wataona tu, huyu hapa kahemka kihisia tu.

Huwezi kumaliza mapungufu ya kila mtu.
 
Sasa hayo ni mapungufu yake, watu wengi wenye hekima wa JF wakipima kwa mizani wataona tu, huyu hapa kahemka kihisia tu.

Huwezi kumaliza mapungufu ya kila mtu.
Yes,
Apo tunaelewana. Ukitoa bandiko lako jamaa akitukana au kubeza kwa namna yeyote ile mchukulie poa tu, tambaa na reply za maana, chota maarifa, ufahamu, uelewa na ujuzi....

Muache na mitusi na mihemko yak kwa uhuru na nafasi yake...
 
we ni mgeni humu? Kama unaona huwezi kuona ukipingwa na kuzodolewa usiposti kitu. Wenzio tunajua kuwakabili wenye majibu yenye karaha na dharau, tunawanyuka humuhumu mpaka wanakimbia wenyewe na kushika adabu zao
 
Unaomba hurumaaa😂😂😂😂


Yaani mi nile gambe kwa hela zangu alafu uje unilazimishe kucoment vizuri kwenye andiko la hovyo!!!?

aaaa bwana weeee mi laazma nikuchane laaaivuuuu kabisaaa!!!! Kwanzaa Babuu USIFORCE TUFANANEEEE!!!!!!!
 
Posa msichana mzuuuuuri hapo ulipo nakulipia mahari 100%.
 
Hiyo sentensi ya mwisho ndiyo imebeba ufumbuzi wa tatizo.
 
Ukikua kiakili utaacha.

KWASASA TUNAKUPA MUDA UKUE KIAKILI KWANZA (HAUJIELEWI).

KaziKweliKweli/JobTrueTrue
 
Kabisa Mkuu, wanakera sana.

YANI INAFIKIA HATUA MPAKA MLETA UZI NAYEYE ANATUKANA KWA KUKOSA UVUMILIVU.
Hapo juu kulia kwa mada kuna vidoti 3, ukivifungua kuna option ya kuripoti bandiko la mchango unaodhani umekiuka maadili. Tatizo hata ukiripoti mara 100 hakuna hatua inayochukuliwa, wakati fulani nadhani natenda dhambi kufikiri kuwa labda hali iko hivyo kutokana na kwamba huenda mmiliki wa jamvi naye kakuzwa kwenye mazingira dhalili kama haya ndiyo maana hawezi kuchukuwa hatua.
 
Wewe utakuwa mgeni wa mtandao, karibu mtandaoni...

Actually JF imekuwa ya kistaarabu sana sasa hivi, sababu joto la kisiasa sio kubwa sana, na tension za kidini hazijafikia za wkati ule

miaka ya 2015/2016 hii unayoiona ilikuwa cha mtoto
 
Mkuu,

Kama matusi ni lazima yawepo najiuliza ni kwanini mtandao unaweka disclaimer zinazopinga matusi. Wee andika neno la kujaamiana kwa Kiingereza, mfumo wa mtandao utaukataa chap.

Hii pia nadhani mfumo umekaririshwa misamiati bila kujuwa kuwa lugha ina misemo pia.

Mfano, msemo "https://jamii.app/JFUserGuide off" siyo tusi, bali unamaanisha "kuachana na jambo/kitu"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…