Uhuru una mipaka Jiheshimu Mkuu

Uhuru una mipaka Jiheshimu Mkuu

Habari zenu Wakuu,

Kumekuwa na Uhuru mbovu kwa baadhi ya watu linapokuja suala la kuchangia mada au Bandiko la mtu.

Nimeona sio mara moja, ni mara nyingi sana mtu analeta mada halafu anatokea mtu from nowhere ana-comment upuuzi au kumdharau mleta mada.

Hii hali nimekuwa naiona kwenye mabandiko yanayohusiana na Siasa au Dini, kiukweli sio jambo jema mnalolifanya kwa watoa Mada. Kukejeli au kumdharau mtu kwa Siasa au udini ni Ubaguzi na unapaswa kukemewa.

USHAURI
Kama unapinga mada ya mtu basi tumia hekima na staha kwenye maneno unayoyaandika.
Swadakta umesema kweli



Sent from my SM-A047F using JamiiForums mobile app
 
Wewe ni mtu usiye amini katika uhuru wa mawazo.

Wewe ni mtu ambaye ungetamsni Dunia iwe na taswira Moja tu.

Wewe ni mtu ambaye unatamani uhalisia utazamwe katika two dimension tu wakati Kuna three mpaka four dimensions.

Wewe ni dictator uchwara uliyejificha kwenye kivuli Cha wastaharabu.

N.B Ndani ya mada kuu, huwa Kuna mada ndogo ndogo nyingi ili kuikamilisha mada kuu.

Ndani ya hizo mada ndio nguvu ya hoja huibuka na mitazamo tofauti hufikia harmony.
Umeelewa nilichoandika Mkuu?

SIO KILA KITU NI LAZIMA UPINGE.
 
Amekusikia yule bibi mwenye chuki na akina fulani kisa tu wamempita umaarufu hapa jamvini
Muhimu ni kuwapuuza na kuwachukulia kama wapumbavu tu
 
Sawa.. uonavyo boss
Wewe ni muhuni tu, sijawahi kuona Mwanamke mwenye tabia kama zako.

Unachochea ugomvi siku zote, unapenda kuwakandamiza wenzako, unaongea maneno yasiyo na staha kwa jamii.

POLE SANA MUHUNI.
 
Wewe ni muhuni tu, sijawahi kuona Mwanamke mwenye tabia kama zako.

Unachochea ugomvi siku zote, unapenda kuwakandamiza wenzako, unaongea maneno yasiyo na staha kwa jamii.

POLE SANA MUHUNI.
Sipingi
 
Pole ndugu,ila kwa aina ya uchangiaji wa jukwaa hili ukiamua kumfuatilia kila mmoja utaumia sana.Jua kuwa kila mmoja anao uhuru wa kusema akitakacho,na zaidi wengi hatujuani hatuonani,na kila mmoja ana malezi yake,ana tabia yake na kamwe hatuwezi kufanana,ukiona mnatofautiana mitazamo mpotezee,angalia yupi mnaweza enda sawa,mtashare mawazo na mitazamo,huku furaha yako ikisalia.
Ni ukweli usiopingika kwamba kamwe hatuwezi kufanana, hatuwezi kukubaliana kila kitu na haitokaa itokee hivyo LAKINI kero ni inakuja pale ambapo mtu hajakubaliana na mawazo yako, badala ya kukupinga kwa hoja anakutukana ww, mwenza wako au hata mzazi wako. Hiyo sio sawa. Ingefaa wachangiaji nao watambue kwamba watu tunatofautiana katika uvumilivu. e.g. Mtu mwingine akitukanwa tu, hata kile kizuri alichonacho hatakisema tena.
 
Hivyo ni vitu ambavyo haviepukiki mnapokutana wa watu wa jamii tofauti tofauti. Utofauti wa mtaani ni kwamba watu hawatoi hizo kejeli kwa kuogopa kupigwa au kutukanwa. Ila humu ni rahisi kwa sababu haukutani na mtu physically, hivyo hata akikutusi uwezi kumfanya chochote
Mkuu umepotea sana sikuoni kabisa kwenye majukwaa
 
Umeelewa nilichoandika Mkuu?

SIO KILA KITU NI LAZIMA UPINGE.
Sipingi ila unashindwa kujua jambo Moja dogo sana.

Mawazo ni yako ikiwa yapo ndani ya kichwa chako.
Ukiyatoa yatoe kwa watu mnao fanana

Ukiyaweka wazi iwe mitandaoni au kwenye kadamnasi basi jiandae kukosolewa, kupingwa, kudhihakiwa na ikiwezekana kubanduliwa kwa hoja yako.

Sasa unataka JAMII FORUM mtandao wenye watu mbali mbali, wenye fikra na mitazamo tofauti, wenye uhuru wa kuchangia au lah, wote wawe na attitude sawa?

Huoni una tatizo la kisaikolojia?
Hata huko Qoura mnapo pasema ukisoma coments utaona wanavyo pishana.
 
Back
Top Bottom