Uhuru wa Mahakama katika kesi ya Freeman Mbowe na wenzake watatu

Uhuru wa Mahakama katika kesi ya Freeman Mbowe na wenzake watatu

DaudiAiko

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2012
Posts
409
Reaction score
343
Wanabodi,

Hivi karibuni, Hakimu Mustapha Siyani alitupilia mbali hoja za mawakili wa Freeman Mbowe akisema kwamba maelezo ya washtakiwa wote yaliandikwa na kuwasilishwa mahakamani kwa njia zilizo kidhi matakwa ya sheria. Kwa kuamua hayo, hakimu alijiridhisha kwamba mshtakiwa namba mbili Bw Adam Kasekwa hakuteswa wala kutishwa alipotoa maelezo yake. Katika maelezo yake, Bw Adam Kasekwa alikiri makosa. Maamuzi hayo yamewafanya wengi haswa wana CHADEMA kuhoji utaratibu wa kupata haki nchini na uwezekano wa mifumo yetu kushindwa kutekeleza hayo bila upendeleo.

Ni muhimu kuelewa kwamba kuna kesi ambazo zinaweza zisiwe na hamasa kubwa kutoka kwa wananchi na kesi za watu maarufu na wenye ushawishi mkubwa nchini. Kesi ambazo zinahusisha watu maarufu na wenye ushawishi mkubwa ndio za kuangaliwa sana kama kipimo cha uhuru wa mahakama na ubora wa haki. Kwa bahati mbaya au nzuri, mtu mmoja tu ambaye ndiye hakimu ndio anaye bebeshwa vikoba vya kufanya maamuzi mazito yanayoweza kuwa mazuri au mabaya kwa wahusika.

Inawezekana kabisa kwa mahakimu kujiuliza kama mtuhumiwa anaweza kujirekebisha akipewa nafasi nyingine au kama mtuhumiwa hajutii aliyoyafanya na hivyo kuwa tishio kwa wananchi wengine uraiani. Kwasababu hiyo maamuzi yoyote lazima yanasababisha "Psychological burden" kwa mtoa maamuzi na lazima yachambuliwe kwa kina. Kwa mfano, aliyeuwawa lazima ana ndugu, lazima ana familia na kwasababu kama hizo lazima kuwe na "Justice". Baada ya hayo yote, lazima tujiulize kama kuna hakimu anayependa kufunga watu au anayefurahia kuona mianya kwenye mifumo yetu ya sheria.

Adam Kasekwa kukubali kosa ni pigo kubwa sana kwa Freeman Mbowe kwasababu wameshtakiwa pamoja. Inawezekana kwamba kuna mengi ambayo hatufahamu. Unapo ongelea kuhusu haki inayotolewa mahakamani ni muhimu kufahamu kwamba watoa haki wote wakiwemo mahakimu, wanatakiwa wawe salama wanapofanya maamuzi yenye uzito na maamuzi yanayo lengwa kwa watuhumiwa maarufu.

Vilevile uwezo wa kupinga matokeo ya chaguzi mbalimbali mahakamani inaenda sambamba na kuwa na mahakama huru isiyo na upendeleo na inayoweza kufanya maamuzi mazito kwa ufasaha. Sijaribu kusema kwamba haiwezekani kupata haki mahakamani ila ukijaribu kufikiria kuhusu maamuzi yanayofanywa mara kwa mara mahakamani, inawezekana kwamba watoa hukumu wanaweza kuwa na maadui wengi.

Mungu ni mwema, wakati wote
 
Lengo lao ni kumfunga mboye na kukifuta chama cha CHADEMA katika usajili

Next door:
Baada ya Samia kuapishwa Nov 2025 kama Raisi ndipo atatoa msamaa kwa wafungwa akiwemo mboye.
 
Lengo lao ni kumfunga mboye na kukifuta chama cha CHADEMA katika usajili

Next door:
Baada ya Samia kuapishwa Nov 2025 kama Raisi ndipo atatoa msamaa kwa wafungwa akiwemo mboye.
Na atakuwa amepoteza haki yake ya kugombea hata ujumbe wa nyumba kumi!
 
Jaji/Hakimu hutoa hukumu kulingana na ushahidi uliofikishwa au kutolewa mahakamani, na si vinginevyo. Hivyo basi, mwenye kubeba lawama kuhusu mapungufu ya hukumu yoyote ile ni mawakili wa pande zote (waendesha mashtaka na utetezi). Na kama hukumu ina utata, nafasi ya kuirejea ipo nayo ni kukata rufaa (rejea kesi ya Mbowe na Wenzake, yenye kuhusu kifo cha Akwilina, na nyinginezo nyingi tu).

Tusijivike ujuaji na kubadili mitandao ya kijamii, vijiwe au hisia zetu binafsi, kuwa mahakama.
 
😁😁😁
AIgmal.jpg
 
Lengo lao ni kumfunga mboye na kukifuta chama cha CHADEMA katika usajili

Next door:
Baada ya Samia kuapishwa Nov 2025 kama Raisi ndipo atatoa msamaa kwa wafungwa akiwemo mboye.
Ndio yamekuwa hayo. Tujiandae kisaikolojia kwa kufahamu adhabu za kesi za ugaidi.
 
Hivi kweli mhalifu akiri kosa mwenyewe bila kufinywa??!! .
 
Back
Top Bottom