Uhuru wa Vyombo vya Habari hatarini: Waandishi wa Standard Media wazuiwa kwenye hafla ya Rais William Ruto

Uhuru wa Vyombo vya Habari hatarini: Waandishi wa Standard Media wazuiwa kwenye hafla ya Rais William Ruto

OwadeKuya

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2026
Posts
535
Reaction score
312
Waandishi wa habari kutoka Standard Media Group wamezuiwa kuingia katika event ya Rais William Ruto huko Naivasha wakati wa Second National Education Conference.

Kisa hiki kimeibua mjadala mkubwa kuhusu freedom of speech na haki ya wanahabari kufanya kazi yao bila vitisho au ubaguzi.

Inadaiwa afisa mmoja wa State House aliwaambia waandishi hao kuwa hawataruhusiwa kuingia kwa sababu ya kile alichodai ni “negative reporting” dhidi ya serikali. Huku media nyingine zikipewa accreditation, waandishi wa Standard walibaki nje ya venue.

Jamii wengi sasa wanauliza: Je, serikali inaweza kuchagua media ya kuripoti habari? Na kama media ikinyamazishwa, wananchi watapataje ukweli?

Katika democracy, kazi ya media si kusifu serikali pekee, bali kuuliza maswali magumu, kuangazia matatizo ya wananchi, na kuhakikisha viongozi wanawajibika. Freedom of the press ni haki ya kikatiba, sio favour kutoka kwa viongozi.

Ironically, mkutano huo ulikuwa unajadili matatizo yanayoathiri elimu kama delayed capitation, shortage ya walimu, na confusion kuhusu Grade 10 rollout mambo ambayo wananchi wanahitaji kuyajua kupitia media.

Wanahabari wakinyimwa access leo, kesho nani atasimamia ukweli?

Source: standardmedia.co.ke
 
Back
Top Bottom