Uhuru wa Vyombo vya Habari: Nchi 7 kati ya 10 zina hali mbaya

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Joined
Aug 7, 2018
Posts
685
Reaction score
1,124
Katika Nchi 180 zilizofanyiwa tathmini ya Hali ya Uhuru wa Habari na Shirika la Reporters Without Borders (RSF), 4.4% sawa na Nchi 8 zimetajwa kuwa na Mazingira mazuri ya Vyombo Vya Habari Huru

Hali imetajwa kuwa mbaya zaidi katika Nchi 31 (17.2%) ikielezwa Mazingira ya Habari ni mabaya katika Nchi 7 kati ya 10, na ya kuridhisha katika Nchi 3 pekee


Tathmini ya Shirika la Reporters Without Borders (RSF) katika Nchi 180 Duniani imeitaja Norway kuwa Nchi yenye Hali nzuri zaidi ya Uhuru wa Vyombo vya Habari kwa mwaka wa saba mfululizo

Ireland imepanda nafasi nne na kushika nafasi ya pili, ikifuatiwa na Denmark (3), Uswidi (4) na Finland (5)


Korea Kaskazini imeorodheshwa kama Nchi yenye Mazingira mabaya zaidi ya Vyombo Vya Habari Huru. China nayo ipo kwenye orodha hiyo ikitajwa kuwa Mfungaji mkubwa wa Waandishi wa Habari

Masuala yanayotajwa kupelekea Mazingira mabaya ya Uhuru Wa Habari katika Nchi 180 zilizofanyiwa tathmini ni Mauaji ya Wanahabari, Sheria kandamizi na Ukatili dhidi ya Waandishi


Licha ya kuwepo Mabadiliko chanya katika baadhi ya Nchi, Hali ya Uhuru Wa Habari bado si nzuri katika takriban 40% ya Nchi za Afrika, ikilinganishwa na 33% ya Mwaka 2022

Miongoni mwa vikwazo vya Vyombo Vya Habari Huru ni Mauaji ya Waandishi wa Habari, ikielezwa kati ya Septemba 2022 hadi Januari 2023 Wanahabari 5 waliuawa Kenya, Cameroon, Rwanda na Somalia

Nchini Senegal na Burundi, Waandishi hususan wa Habari za Kiuchunguzi walikamatwa na wengine kufungwa jela


Chanzo: Reporters Without Borders, World Press Freedom Index
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…