Kimsingi vyombo vya habari havikuwa na Uhuru at all. Pitia Sheria ya vyombo vya habari ambayo ofcoz ilipitishwa na Waziri aliyepo sasa hivi bwana Nape ndio aliisimamia.
Pia pitia Sheria ya TCRA kuhusu usimamizi wa vyombo vya habari haswa maudhui ya online TVs angalia sana Sheria ya kulazimisha kuzisajili hizo online TVs pia fees za usajili ambazo zimewekwa exorbitantly as if zile TV ni za starehe wakati zinasaidia jamii ambayo kwa sasa ndio inajizoesha kupata habari kiganjani.
Pitia regulations za Ile Sheria ya Habari zimekaa kipuuzi sana almost Sheria nzima inahinder utoaji na upatikanaji wa habari.
Kuna sheria ya takwimu nayo ilipitishwa na Magufuli nayo ina madudu mengi sana unaweza kupitia na regulation zake.
Ningekuwa nakufahamu ningekufanyia hiyo research aisee Ila pita humo nilipokuelekeza then waweza kugoogle maandiko mbalimbali yaliyohusu kubanwa kwa Uhuru wa Habari yapo mengi sana ya Jenerali Ulimwengu, Kuna matamko ya Baraza la wahariri Tanzania, Kuna Baraza la vyombo vya habari (MCT) nk hao wote walishatolea matamko kuhusu hizo Sheria na mambo kadhaa wa kadha.
Pia Kuna matukio ya waandishi mbalimbali kufungwa jela Kama Joel Kabendera, Kuna waandishi wengi sana walikamatwa wakafunguliwa mashtaka kipindi Cha Magufuli alikuwa hataki serikali yake isemwe au kukosolewa kwa lolote.
Kuna matukio ya mwandishi au waandishi kuuwawa baada tu ya kuonekana wakiripoti taarifa ambazo serikali ya kipindi kile ilikuwa haipendi. Mfano Azory Gwanda mwandishi wa BBC aliuawa katika mazingira ambayo ikionekana anaandaa makala ambayo ilisemekana angeipeleka BBC. Haya yote unaweza kugoogle na unapata habari zake.
Pia jiunge na Mwananchi Online lipia Ile fee ili uweze kuaccess library ya magazeti yote uweze kuweka proper reference.
Nitakutafutia Journals na Periodicals ambazo zimekuwa na makala za hayo mambo pia but you better find a journalist atakupatia kulingana na journals za taaluma yao but pitia LHRC watakuwa wanazo nitajaribu kumcheki Mkurugenzi wao she can be of assistance.
Naweza kuwa na msaada hasa kwenyupande wa sheria coz it's my profession.
I hope nitakuwa nimekupa mwwnga kidogo pa kuanzia.