Uhuru's 5th trip to Beijing

Hii ndo matatuπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Duh!! Kwa hiyo wewe huijui Kenya halafu upo busy kuitetea!! Nenda google kaulize kama una roho ya huruma machozi yatakulenga.
Kumbe unategemea Google kaka mtu wa Pwani ya Dar ambaye hujui hata mpakani kunakuwaje ni ngumu sana kuelewa Tanzania CCM imetuloga
 
Huwezi kuelewa ni kwamba Wakenya wanasafiri usiku na Mchana hakuna kulala.
Sisi tunalala na mashine zinalala mfanya biashara analazimishwa kufunga biashara na kusafiri mchana.
Unamlaza mtu aliyetoka Mwanza Morogoro kisa huwezi kulinda ni aibu
Tz ipi hiyo mbona mimi ninasafiri usiku sana tu. Wewe jamaa unaonekana una frustration za kupambana na life. Mimi binafsi napambana ila siilaumu serikali kwa kila kitu kwa kua tu kuna sehemu nilikwama au ilinikwamisha. Mfano umesema kuhusu kuzuiwa kuuza mazao Kenya, nahisi wewe ni mhanga wa hili swala na pole sana, mtazamo wangu kuhusu hiyo ishu ni tofauti na serikali ila haina maana niponde ujenzi wa reli au elimu bure kisa kuzuiwa kuuza mazao yangu Kenya.
 
Bei ya unga Tz shilingi ngapi?
 
Kumbe unategemea Google kaka mtu wa Pwani ya Dar ambaye hujui hata mpakani kunakuwaje ni ngumu sana kuelewa Tanzania CCM imetuloga
Sasa ulitaka nikwambie upande bus uende Marsabit au Turkana!! Uko nilipo kuelekeza ungekutana na chambuzi za journalist wa kikenya wakiongelea hali duni za huko kwa andani kabisa. Ila wewe kwakua ni mbishi ata ishu ndogo tu unagoma kuifanya ili uendelee kubaki na fikra zako mgando. Ila pole sana kwa yaliyo kukuta, sasa hivi si mmeruhusiwa kuuza lakini
 
Wewe Unalako
Nilicho gundua hujatembelea hiyo Kenya
Wacha nikuache
Kuna kitu lazima ujue sisi tunaiona Kenya kama jirani mzuri na rafiki anaefaa katika maendeleo. Tunaenda Kenya tunatembea tunajifunza. Tunaowa huko na dada zetu wameolewa huko tunafanya biashara nao tunaweka vitega uchumi nao wanawekeza kwetu.
Hebu niulize popote katika Kenya au pata masaada mwambie Mkenya akuulizie ili ujue tunavyoijua
 
Wapi Tanzania utapata ticket ya basi inaondoka jioni toa mfano saa hii niko Arusha au Mwanza naambiwa tuonane kesho Dar kuna biashara kama nisipopanda gari za magazeti na malori ndio hela ishanipita kisa tu Police wanaogopa wahalifu
 
Wewe Unalako
Nilicho gundua hujatembelea hiyo Kenya
Wacha nikuache
Kweli mkuu jamaa analake binafsi. Kenya haijui ila ameamua tu kutoa frustrations zake. Halafu amekosea njia, kuna maeneo yake anashindaga huku kaja kibahati mbaya..
 
Wamekopa kutengeneza Reli au kununua Train ?Maana sisi tunajenga reli pia ambayo hatujui itapita ipi labda ya makaa ya mawe.
Wewe tu ndo hujui.. Wewe wa wapi hivi! unajichoresha tu. Kuuliza siyo ujinga
 
Kweli mkuu jamaa analake binafsi. Kenya haijui ila ameamua tu kutoa frustrations zake. Halafu amekosea njia, kuna maeneo yake anashindaga huku kaja kibahati mbaya..
Wewe unaijua Kenya ipi labda ukiulizwa?
Frustration tunazo maana tunalazimishwa na CCM kuwa Masikini wakati tuna Jirani kama Kenya angenunua mazao yetu
 
Wewe tu ndo hujui.. Wewe wa wapi hivi! unajichoresha tu. Kuuliza siyo ujinga
Jibu swali ni kama mtu aliyejenga nyumba nzuri halafu unamsimanga kwa Sofa lake ambalo si muda atalibadilisha
 
.Binafsi nimependa vile unavyoeleza mambo kinaga ubaga bila kusita jambo ambalo hata maripota wa bongo hawawezi kulifanya kwa sababu hawana Uhuru wowote .Ni dhahiri shairi kwamba nchi yenu inakabiliwana majanga mengi ambayo serikali hujaribu kuyaficha kwa kuhakikisha hayaripotiwi tofauti na Kenya, wanahabari wanaruhusiwa kuanika habari zozote watakavyo na ndio maana wengi humu huikebehi Kenya bila kujikumbusha hali ya nchi yao. Hayo yanayofichwa humo bongo yataendelea kufichuka na dunia itagundua huu unafiki wenu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…