Uhusiano thabiti kati ya Tanzania na China wafungua milango ya ushirikiano wa kina

Uhusiano thabiti kati ya Tanzania na China wafungua milango ya ushirikiano wa kina

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,116
Reaction score
1,121
VCG11447661365.jpg


Mwaka 2024 ni mwaka ambao umeshuhudia mafanikio makubwa kwenye ushirikiano na maendeleo baina ya China na Afrika, hasa China na Tanzania. Mafanikio haya yanatokana na mambo ya msingi yaliyowekwa na viongozi waasisi na kuendelezwa na viongozi wa sasa pamoja na sera nzuri ya mambo ya nje ya China kwa Afrika.



Kwa miaka mingi, China na Tanzania zimeshirikiana katika maeneo muhimu, ikiwa ni pamoja na maendeleo ya miundombinu, biashara, kilimo, elimu, utalii, afya, uchumi wa bluu na ufundi huku nchi hii ya Asia sasa ikitajwa kuwa miongoni mwa masoko yanayoibukia katika visiwa vya Zanzibar. Uungaji mkono wa China kwa Zanzibar chini ya Pendekezo la “Ukanda Mmoja Njia Moja” umerahisisha ujenzi wa miundombinu na kuboresha hali ya maisha ya wananchi wa visiwa hivyo.



Katika mahojiano ya hivi karibuni na Shirika la Xinhua, Katibu Mkuu Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Aboud Suleiman Jumbe alisema mafanikio haya hayakuja ghafla tu, bali yalitokana na mchakato wa nchi hizi mbili zenye uhusiano imara, mchakato wa kisiasa ambao umefungua njia ya ushirikiano wa kiuchumi na wa kiufundi, na mambo mengine mengi.

Zanzibar, iliyopo takriban kilomita 35 kutoka pwani ya mashariki ya Tanzania, imesheheni visiwa vingi vidogo na visiwa viwili vikubwa vya Unguja na Pemba. Vikitambulika kama "Lulu ya Bahari ya Hindi," visiwa hivi vya Zanzibar huvutia makumi ya maelfu ya wasafiri wa ng'ambo kila mwaka kwa mandhari yake ya asili na maeneo ya kihistoria, ikiwa ni pamoja na Mji Mkongwe ulioorodheshwa kwenye Urithi wa Dunia.



Katika kisiwa cha Unguja kinachotembelewa zaidi na watu, Terminal 3 ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume, iliyojengwa na kampuni ya China, ndiyo ilikuwa lango kuu kwa abiria wa kimataifa.



Wakati huo huo, Barabara ya Nyerere, inayounganisha uwanja wa ndege na Mji Mkongwe, pia imefanyiwa ukarabati upya kwa msaada wa wajenzi wa China. Pia mradi wa kuboresha njia zenye urefu wa kilomita 100 katika eneo la katikati mwa mji na ujenzi wa barabara za juu mbili unakaribia kukamilika.



"Bila kuungwa mkono na serikali ya China na wajenzi wa China, ingetuchukua miaka mingi kukamilisha miradi hii," alisema Jumbe. "Miradi hii iliyokamilika ndani ya miaka minne, ingechukua miaka 15 au 20 katika hali ya kawaida Zanzibar."



Kwa mujibu wa Jumbe, Zanzibar imekuwa na historia kubwa ya ushirikiano na China hasa katika masuala ya tiba na afya. Kuhusu utalii, alisema pande hizo mbili "zinahitaji kuongeza" ushirikiano kulingana na miradi ambayo tayari imefikamilika.



Takwimu za Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Zanzibar (OCGS) zinaonesha utalii kuwa moja ya nguzo za ukuaji na utoaji wa ajira katika visiwa hivyo, unaochangia asilimia 27 ya pato la taifa la Zanzibar na asilimia 80 ya mapato yake ya fedha za kigeni.



Kutokana na msisitizo wa China kuwa nchi zote duniani, ziwe kubwa au ndogo, zenye nguvu au dhaifu, tajiri au maskini, lazima zitendewe sawa ziheshimiwe na pia zipewe fursa za kujiendeleza, China sasa imekuwa miongoni mwa nchi zinazotambuliwa zaidi na mamlaka ya Zanzibar hasa kwa upande wa soko lake.



Ushirikiano huu bila shaka ni kielelezo kizuri cha namna historia ya uhusiano wa Tanzania na China imeweza kubadilisha mifumo muhimu ya miundombinu ya Zanzibar, ambayo inasaidia mifumo ya kiuchumi, kama vile utalii, biashara, usafirishaji na hata nishati.
 
Wachina hata waje wawekeze bongo na wafungue viwanda vya kutengeneza simu ila matokeo yake wanakuja bongo kuuza mahindi ya kuchoma.😀😀😀😀
Nasubiria copy mchina ya JBL Boom nikanunue😀😀😀😀
Huwa nashangaa sana mchina kavumbua operating system ya simu ila cha ajabu inatumia application za android zenye extension ya .apk😀😀😀😀
 
Back
Top Bottom