Uhusiano wa kimapenzi na Mwanamke aliyekuzidi umri ni hatari Mkataba

Uhusiano wa kimapenzi na Mwanamke aliyekuzidi umri ni hatari Mkataba

View attachment 3671646
Nimekuja ila sina maelezo, sijawahi kujaribu kijana niliyemzidi umri, ila huko mbeleni ninaweza kutaka kujionea nyie vijana wa alfu mbili mna maajabu gani 😂😂
Vijana wa 2000 wamekusikia watakupapatikia huko PM kama kumbikumbi wa mvua za vuli.
Ubinadamu ni kazi/the humanity is work.
 
Unapoingia kwenye uhusiano wa kimapenzi na mwanamke aliyekuzidi sana umri, fedha, au uzoefu wa maisha, wengi huona tu miili miwili ikikutana au akaunti ya benki ikiongezeka. Lakini katika ulimwengu wa roho—iwe ni kupitia elimu za kale za Afrika (African Metaphysics), miiko ya kiasili, au hata maandiko ya kidini—tendo la ndoa halijawahi kuwa suala la kimwili pekee; ni mkataba wa kiroho unaounganisha nafsi mbili .

Katika misingi ya kiroho, mwanamke aliyepitia miaka mingi ya maisha ana historia ndefu ya nishati (energy), madhabahu za kifamilia, na pengine vifungo vya kiroho kutoka kwa wanaume wote aliowahi kukutana nao huko nyuma. Unapolala naye, unajikuta ukifungua mlango wako wa kiroho na kufanya mabadilishano ya moja kwa moja: unachukua mizigo, mikosi, au laana alizozibeba kwa miaka mikubwa, huku yeye akibeba nguvu, usafi, na nyota ya ujana wako (vital life force).

Hii ndiyo sababu vijana wengi wanaotoka na wanawake wa namna hii hujikuta ghafla wakipoteza mwelekeo wa maisha, nyota zao zikizimika, na maono yao ya baadaye yakifutika kabla hata hawajafikisha miaka 30—wakiwa wamebaki kama ganda tupu lililomalizwa ushawishi wake wote.

Baadhi ya wataalamu wa kimila wanaenda mbali zaidi na kudai kuwa wapo wanawake wazee au matajiri wanaotambua siri hii na kuitumia kwa makusudi kama aina ya muarobaini ya kiroho—wakitumia miili ya vijana wadogo kama busta za kuongeza miaka yao ya kuishi, kudumisha biashara zao, na kung'arisha nyota zao kupitia nguvu mpya za vijana wachanga.
Ushauri mzuri sana, ngoja marioo waje kutia neno.
 
Hii dialogue nimetoka kuifanya na jamaa yangu juzi, hili suala ni kweli kabisa.
Huwa wanasema katika mapenzi kunakua na transmission ya spiritual package.
Sasa ni hatari mwanamke akuzidi umri means magnetic power yake ni kubwa kuliko yako lkn ukimzidi umri hata kama anamikosi power yake ni ndogo kuliko yako wewe utabaki salama.
 
Back
Top Bottom