Uhusiano wa mtoto kunyonya kidole na uwezo wake kiakili

Uhusiano wa mtoto kunyonya kidole na uwezo wake kiakili

BRAND

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2013
Posts
296
Reaction score
257
Habari zenu wadau! Mungu amenijaalia kupata mtoto wa kike hiv karibu,kwa sasa ana miezi mitatu,imefika wiki sasa tangu aanze kunyonya kidole gumba,yaani amekazana sana hadi kero!!

Kuna watoto wengi wanaokuwa na tabia hii ambao baadae wanakuwa na uwezo mdogo wa kiakili darasani n.k,tafadhari mwenye uelewa wa hili naomba msaada,nitawezaje kumfanya a aache hii tabia?
 
Hilo nitatizo kwani kwanza ,mdomo una athirika hizo lips zina legea kutokana na uzito wa kidole,pili mtoto hua ana chelewa kuwa na ufaham kutokana muda mwhngi hutumia kunyonya kidole.Ila ataacha mapema kama uta mzuia kunyonya kwa njia mbadala .
 
labda mii nitoe ushuhuda,ni kwamba kuna mtoto wa dada angu ambae kwa sasa ana miaka 17{ke}.Alianza kunyonya kidole gumba {mkono kushoto} akiwa na miaka miwili,aliendelea vivyohivyo mpaka alipo anza class 1.Uwezo wake daarsan ulikuwa mzuri mpaka class 4.alpofika darasa la 5 uwezo ulishuka ijapokuwa darasa la 7 alifauru kwenda kidato cha 1,mamake na nduguze walijaribu kumfanya aache kwa kumpaka pilipili akiwa usingizini,uharo wa kuku{anaetaga} mpaka konokono na jongoo kwenye kidole hicho lkn aliiendela vivyohvyo pasipo kuonyesha dalili za kuacha ispokuwa alipunguza baada ya kuona anachekwa na marafiki zake huko skonga,hiyo haikumfany aache(alipokuwa katika mazingira ya upweke alikuwa anakinyonya vizuri mnoo).kidole hicho ilifkia kipindi kikawa tofauti na cha kulia,hiki kilionekana kama kimesugulia na kitu flani ivi mfa labda kama jiwe na kilikuwa chembamba sana tofauti na vingne.Alipofanya mtihani wa kidato cha pili kwenda cha 3,baada ya kumaliza mitihani Alimwendea mama ake na kumwambia mama mii Sitaki tena kusikia habari za shule,alipo ulizwa sababu alijibu haelewi kitu na masomo yenyewe magumu.Basi mtoto akbaki nyumbani kwa mama ake.

Labda nikwambie ndg Mtoa Mada,
kwamba jitahidi kumfanya aache kunyonya hicho kidole kabla hajaanza kujitambua manake itmpa shida kuacha akiwa tayari kesha kariri hiyo kitu.
Jitahidi sana ndg.
 
Jamani hizo ni coincidence tu uwezo wa akili na kunyonya kidole Havina muingiliano. Hiyo ni dalili yakuwa huyo mtoto hashibi mnyonyesheni ashibe kabla hajakizoea kidole. Mama ale protein za kutosha maziwa yatoke mazito ashibe motto. Akitaka kunyonya kidole apewe nyonyo haraka NJAA imtoke. Kumuachisha mtoto kunyonya kidole zip simple approach na mtoto anaacha kupitia kwa daktari wa kinywa na meno sio medical dr wala hivyo mnavyowapaka watoto vidoleni.
 
Wala usiwe na wasiwasi kuhusu akili kucharge,..mtoto wangu wa kiume alikuwa ananyonya kidole mpaka darasa la kwanza (miaka 6) na akili zinachaj kweli,anakuwa wa kwanza tu darasani( la pili sasa) ..sema madhara yake anaweza akawa anaugua sana minyoo, afu kidole kinakonda kinyama, aliweza kuacha automatically lakin kwa kumkataza sana na ikiwemo mbakora!.....lakini kwa ushauri huyo mdogo mwache akifika kama umri wa miaka miwili mweke pilipili afu akinyonya mwambie chafu hiyo ataacha tu....
 
Jamani hizo ni coincidence tu uwezo wa akili na kunyonya kidole Havina muingiliano. Hiyo ni dalili yakuwa huyo mtoto hashibi mnyonyesheni ashibe kabla hajakizoea kidole. Mama ale protein za kutosha maziwa yatoke mazito ashibe motto. Akitaka kunyonya kidole apewe nyonyo haraka NJAA imtoke. Kumuachisha mtoto kunyonya kidole zip simple approach na mtoto anaacha kupitia kwa daktari wa kinywa na meno sio medical dr wala hivyo mnavyowapaka watoto vidoleni.

Sidhani kama hilo swala linahusiana na njaa kwasababu hata dogo ashibe vip akitulia tu anaweka kidole hata ukimpa chakula tena anakataa na dole anaweka tena.
 
Michango mizuri kwa mada hii ngoja na wengine tunufaike kidogo
 
Sidhani kama hilo swala linahusiana na njaa kwasababu hata dogo ashibe vip akitulia tu anaweka kidole hata ukimpa chakula tena anakataa na dole anaweka tena.

Mwanzo wakunyonya kidole unanjia mbili, moja mtoto mdogo sana kuanzia siku moja huwa ni njaa na mbili Mtoto mkubwa kidogo kama miaka miwili yawezakuwa kuiga. Baadae inakuwa mazoea ya hiyo tabia. Ikishakuwa mazoea basi hunyonya hata akiwa kashiba au usingizini.
 
Tafuta njia mbadala umuachishe bado mapema.........
Mnunulie zile nyonyo za watoto za plastic umpachike mdomoni
 
Mwanzo wakunyonya kidole unanjia mbili, moja mtoto mdogo sana kuanzia siku moja huwa ni njaa na mbili Mtoto mkubwa kidogo kama miaka miwili yawezakuwa kuiga. Baadae inakuwa mazoea ya hiyo tabia. Ikishakuwa mazoea basi hunyonya hata akiwa kashiba au usingizini.

Mimi alianza wiki moja baada ya kuzaliwa na bado hajafika miaka miwili hajaiga wala haikusababishwa na njaa.
 
Habari zenu wadau! Mungu amenijaalia kupata mtoto wa kike hiv karibu,kwa sasa ana miezi mitatu,imefika wiki sasa tangu aanze kunyonya kidole gumba,yaani amekazana sana hadi kero!!

Kuna watoto wengi wanaokuwa na tabia hii ambao baadae wanakuwa na uwezo mdogo wa kiakili darasani n.k,tafadhari mwenye uelewa wa hili naomba msaada,nitawezaje kumfanya a aache hii tabia?

Mkuu kama lengo nikumzuia

-Tafuta gloves za jumla (kama mfuko bila vidole) kwa walau size ya mkono wake mfunge vizuri.

Hakikisha ni safi na ziwe kama pair tatu hivi, ukimfunga kwa kama wiki mbili tu ataacha na utamwacha huru.
 
Kuna bwana mmoja anaitwa Sigmund Freud nafikiri alizungumzia hili swala katika nadharia yake ya psychosexual, kuna stages pale amezitaja, jaribu kumsoma unaweza pata majibu sahihi kuhusu hilo tatizo.
 
Daah!! Mi naona nisubiri akishaanza kutembea ndio nianze kupambana na hii tabia,nikianza sasa hiv nitakuwa namuonea kwani bado mdogo sana,yaani anapenda kunyonya dole gumba hasa akiwa ameshiba au anapotaka kulala au akiwa amerelax,akianza kutembea nitatumia mbinu zote hata za jadi ili mradi tu aache huyu first born wangu
 
Aiseee nami nina tatizo la mtoto kunyonya kidole pia.. Limekuwa likinitia wasiwasi sana na uwezo wake kiakili hapo baadae...
 
Hamna usiano wa mtoto kunyonya kidole na uwezo wake darasani no labda uniambie kama uwezo wako ni mdogo basi inawezekana kurithi kutoka kwako
 
Vitu viwili toafuti uwezo wa kiakili na kunyonya vidole..Muachiche kiistarabu ikishindikana kumbuka jinsi anavyokuwa ipo siku ataacha lisikuumize akili
 
Hata mm nina mtoto wangu anamiez tisa sasa,yan ananyonya kidole hatarii usiku kucha mchana kutwa,, wataalam mtuambie jaman kwani hata mm niliwahi kusikia kuwa mtoto akiwa anayonya sana kidole hupelekea kuwa mzembe na uwezo wake darasan unakuwa mdogo pia.
 
duuh sikuwahi kuhisi kama kunyony
a kidole kuna uhusiano na uwezo wa akili wa mtu mi mtoto wangu ana miezi kumi hajawahi nyonya kidole ila cku za hivi karibuni ameanza tabia akiona chakula juice au maji anaingiza kidole mdomoni anatoa kma mtu anae onja kitu ukishampa anachotaka basi harudi tena.
 
Back
Top Bottom