Uhusiano wa mtoto kunyonya kidole na uwezo wake kiakili

Uhusiano wa mtoto kunyonya kidole na uwezo wake kiakili

Suluhisho ni kumchanja chale ndogo ktk kdole hicho akiona maumivu ataacha kwa wale wkubw kdogo, mlishe vyema kwanza.
 
Nimenyonya kidole hadi darasa la 6. Primary sijawahi kushuka number 3. Secondary form 3 hadi 4 number 1 hadi namaliza. Form 6 first in BAM coastal zone now namaliza masters in orthopaedics. Mwache mtoto anyonyeeeeeeeeeee
 
Duuh mwangangu kafikisha miez 3 saiv ananyonya vidole balaaa..
 
hizo ni tabia za kitoto tu , akikua ataacha. halafu pia yawezekana kuwa anawashwa na meno kutaka kuota ndio maana anaweka mkono mdomoni.
 
Kuota meno miezi mitatu? Kasi imeongezeka sana wikii hii haliii kabisa yupo bize na vidole hadi naogopa..
 
Daah vipi kuhusiana na mpangilio mbaya wa meno?
 
Havina uhusiano kabisa. Mimi nna ndugu yangu amenyonya kidole mpaka mkubwa kabisa hadi mwenyewe akaanza kuona aibu akaacha. Upande wa darasani alikuwa kichwa balaa amesima vipaji maalum sasa hivi ni injinia tena mkuu wa kitengo kwenye taasisi moja kubwa tu mkoa fulani nyanda za juu kusini. Ningeweza kutaja hata hiyo taasisi ila ntakuwa kama namuumbua kwamba alikuwa mnyonyaji wa kidole. Mdogo wake ye aliacha mapema kunyonya kidole (nadhani aliacha drs la nne hivi) sasa hivi ni mwalimu na anachukua masters
 
Yaani humu zaidi ya asilimia 90 ya ushuhuda wa wanyonya vidole ni namba moja darasani , duh! Kweli wanyonya vidole wanaonekana kuwa magenius.
Cha muhimu mtoto ashibe awe occupied.... Muwe mnacheza na watoto hata kama ana miezi miwili tu.
Siku hizi watoto wanaakili sana miezi miwili tu mtoto anaasikiliza sauti mbalimbali na kuzifurahia , wanafurahia mwanga kwenye simu na TV hivyo unaweza kushangaa mtoto wa miezi miwili anaangalia movie.
Vidole ni njia ya kujibembeleza.
 
tusemeje sasa wengine, mimi nina ndugu yangu above 30 years mpaka hii leo ananyonya tena madole yote mawili anayatumbukiza mdomoni, na mwanae wa kwanza ndo naye noma tena huyu mwanae (7years) wakati kidole kiko mdomoni mkono mwingine kidole kina viringa pindo ya nguo ya vest yake. Sasa hao wote ni vipanga balaa na hao wote ni very active.
kwa hivyo naona hakuna uhusiano kabisa
 
Mpe vitu ashike mkonon vya kuchezea tena ni rahisi sababu kwa umri huo muda wote mikono ameifunga hivyo atakishikilia hicho cha kuchezea bila kudondosha nami nina mtt wa miezi mitano ila tatizo niligundua kuwa alikuwa hashibi baada ya kumpa nyonyo kila wakati linapungua kwa kasi.
 
Binafsi sioni uhusiano kati ya kunyonya kidole na uwezo kiakili...mdogo wangu mimi wa kike,tunafatana kuzaliwa ananyonya kidole tena ananyonya cha mkoo wa kulia ila ana akili balaaaaaa hajawai kufeli popote,na hapa alipo ni daktari wa binadamu..Akili zake ziko vizuri sio darasani sio nje yaan hakuwai kuonyesha chochote cha tofauti hadi tuone may be kwavile ananyonya kidole noooo.....Mapungufu aliyonayo ni ya kawaida kama binadamu wengine...
 
Daah!! Mi naona nisubiri akishaanza kutembea ndio nianze kupambana na hii tabia,nikianza sasa hiv nitakuwa namuonea kwani bado mdogo sana,yaani anapenda kunyonya dole gumba hasa akiwa ameshiba au anapotaka kulala au akiwa amerelax,akianza kutembea nitatumia mbinu zote hata za jadi ili mradi tu aache huyu first born wangu
Duuh! Maisha yanakimbia huyo mtoto sahizi ana miaka kumi na Moja au sio mkuu?
 
Back
Top Bottom