SoC01 Uhusiano wa Uchumi na Utawala Bora

SoC01 Uhusiano wa Uchumi na Utawala Bora

Stories of Change - 2021 Competition

melony

New Member
Joined
Jul 14, 2021
Posts
1
Reaction score
3
Kabla ya kuelezea uhusiano uliopo Kati ya uchumi na utawala bora, ni vema kuanza kueleza dhana ya uchumi na utawala bora.

Uchumi, ni usimamizi wa rasilimali, uzalishaji bidhaa, usambazaji wa bidhaa na utoaji wa huduma kwa jamii ili kuwa na maisha bora kwa jamii na watu kwa ujumla. Uchumi hujengwa na mambo makuu matatu: uwekezaji, uzalishaji na utoaji huduma au usambazaji.

Utawala bora, ni kitendo cha kuongoza watu au taasisi fulani kwa haki na usawa bila kubagua ili kuwawezesha watu wote kufikia malengo yao kiuchumi, kijamii, kisasa na kiutamaduni.

Dhana hizi mbili yaani uchumi na utawala bora hutegemeana kwa kiwango kikubwa mno, Kwani bila utawala bora hakuna uchumi imara. Ufuatao ni uhusiano baina ya utawala bora na uchumi.

Uhusiano katika sera, Sera ambazo huundwa na serikali ndio ambazo hutambulisha aina ya uchumi ambao nchi au jamii inaweza kuupata. Serikali huandaa Sera mbalimbali, Sera hizo ndio misingi katika uwekezaji na uzalishaji. Kwa mfano, Sera ya nchi ya viwanda iliyoanzishwa na hayati Mh. Dr. John Pombe Magufuli, imepelekea watu wengi kuwekeza katika viwanda, hii imechangia vijana wengi kupata ajira na kujikwamua katika dimbwi la umaskini. Hivyo ikiwa viongozi au serikali utajengewa Sera imara itapelekea maendeleo bora kwa jamii na watu kwa ujumla.

Uhusiano katika Demokrasia, Demokrasia ni kitu cha msingi sana katika kuinua uchumi. Demokrasia humuweka mtu huru katika kutoa maoni na ushauri kwa serikali hasa katika kuandaa bajeti na vipaumbele katika jamii. Demokrasia huondoa rushwa katika jamii hivyo kupelekea maendeleo na kuinua uchumi. Aidha; katika kueleza demokrasia kuna mawanda mengi sana ya kidemokrasia, baadhi yake ni: uwajibikaji, mfumo wa vyama vingi, uwazi, uongozi bora, haki za binadamu na usawa, katiba bora na Uhuru wa vyombo vya habari. Mambo haya yote huchangia katika kuinua uchumi.

Uhusiano katika amani na usalama, utawala bora hujengwa na uwepo wa amani na usalama wa raia na Mali zao. Nchi yoyote yenye misingi ya Amani na usalama, huvutia watalii, wawekezaji pamoja na biashara ambapo mambo yote haya huchangia katika kuinua uchumi wa jamii. Ikiwa nchi itakosa Amani yaani itakuwa na vita vya mara kwa mara hakutakuwa na aendeleo yoyote ya kiuchumi. Mfano, nchi ya Somalia kutokana na vita vya mara kwa mara hakuna uzalishaji wala uwekezaji wowote unaofanyia Jambo ambalo linashusha uchumi wa nchi. Pia , tazama mfano wa nchi ya Libya ambayo ilikuwa imejijenga kiuchumi lakini kutokana na ukosefu wa amani, uwepo wa vita imepelekea nchi hiyo kushuka kiuchumi.

Mwisho, napenda kutoa ushauri kwa nchi yetu ya Tanzania hasa kwa raisi wetu mama Samia Suluhu Hassan katika hotuba yake aliyosema kuwa kwa sasa tuinue Kwanza uchumi mambo ya katiba baadaye. Mimi napingana nae kwani uwepo wa katiba ndiyo utaongeza chachu ya maendeleo. Ikiwa katiba haitobadilika, machafuko yanaweza kutokea Jambo ambalo kuyafanya taifa letu kurudi nyuma kiuchumi.

Pia napenda kuishauri Serikali ya Tanzania, wakati wa kuandaa Sera ni vema kuwashirikisha wananchi na wadau mbalimbali wa uchumi ili kuunda Sera zenye tija ambazo zinaendana na Kasi ya sasa ya ushindani na utandawazi.
 
Upvote 6
Back
Top Bottom