Mpaka huu Uzi uishe 50% ya wasomaji watakuwa wamesilimu. Mana Kuna tactics za hali ya juu kufundisha basics za uislamu. Good approach. Mpaka Sasa nimeshajua kwamba ukilitaja jina la mtume Mohamad unapaswa kumalizia na na maneno "Amani na neema za Allah ziwe kwake"
Sent using
Jamii Forums mobile app
Actually pamoja na usisimuaji wa simulizi yenyewe lakini pia na:-
1. Kuleta misamiati ya kiswahili sanifu na cha zamani
2. Kuwajulisha vijana kuwa hata wazee walikuwa vijana hivyo wanajuwa kuliko wanavyowa-underestimate
3. Kuwakubusha wazee wenzangu na kuwaonesha vijana baadhi ya vifaa ama bidhaa na vitu vya zamani
4. Kuwakumbusha vijana kuwa dini zipo nyingi lakini pia kuna mila na desturi, tofauti ya imani za kidini zisitufanye kubaguana ama kunyanyapaana
5. Kuelimisha juu ya ubaya wa ubaguzi wa rangi na faida ya kuchangaya nasaba
6. Kutoa elimu ya namna bora ya kufanya mapenzi
7. Kuonesha umuhimu wa kusoma, kusoma vitabu na kujisomea
8. Kufundisha ama kuonesha namna bora ya kusimama na unachokiamini bila kukata tamaa au kutatishwa tamaa
Na mambo mengine kadha wa kadha.
James Jason