Uhusiano wangu kimapenzi na "Hamida"

Mkuu Shikamoo.

Kama Mwenyezi Mungu akakujalia na ukapata muda tunaomba japo kwa kiduchu hii ya Hatimaye Rose ameniPM

Kuna funzo kubwa sana nalipata hapa kupitia hizi simulizo zako.

Asante
 
Shikamoo baba mkubwa (umempita miaka michache baba yangu ) nilianza hii story kutokea kwenye uzi wa rikiboy ila jana usiku nikasoma sehemu zilizobakia huku mpaka usingizi ukanipitia. Nilipoamka nikaendeleza mpaka nimemaliza sijutii muda hata kidogo maana mafunzo niliyopata hapa ni mengi.
Nashukuru Mungu kwa kunifikisha hapa mpaka nikaweza kupata simulizi hii yenye mafunzo mazuri. Nashukuru sana kwa elimu nilioipata inanipa nguvu ya kupambana na changamoto ninazopata za mahusiano na za kifedha.
Nawasilisha
 
1. Nimeulizwa na mmoja wa mdau aliyesoma uzi huu, pm:-

"Je zamani mke ikijulikana hana bikra baada ya ule usiku inakuaje?"

Nimeamua majibu pia niyaweke hapa kwa faida ya wengine.

____

Enzi hizo kuna 'kitu' kilikuwa kinaitwa HARUSI KUJIBU.

Ukisikia harusi imejibu maana yake bibi harusi amekutwa bikra na bwana harusi wakati harusi yenyewe.

Kama harusi HAIJAJIBU maana yake bibi harusi amekutwa hana bikra siku ya ndoa.

Nini hutokea baada ya harusi kutojibu inategemea na bwana harusi ama upande wa bwana harusi watakavyo lichukulia swala hilo kwa uzito upi.

Ikimbukwe kuwa kuna bikra fake pia wakati wa harusi, hii inaweza kutokea bila bwana harusi kujuwa na zipo zinazopangwa akishirikishwa bwana harusi.

Enzi hizo, kama bibi harusi alikuwa hajawahi kuolewa na hakuwa na mtoto na siku ya harusi akakutwa hana bikra, kulikuwa na uwezekano mkubwa wa ndoa kuvunjia kwa baadhi ya maeneo...

Lakini wengine ndoa huendelea lakini thamani ya bibi harusi haitokuwa kama angekutwa na bikra...

Wengine hawakujali huendelea na ndoa kwa thamani ile ile lakini wengi wao ni wale ambao nao walionja kwa bibi harusi mhusika kabla ya ndoa.

Harusi ISIYOJIBU huwa gumzo mtaani kiasi cha kuleta fedheha (enzi hizo)

Harusi ISIPOJIBU, somo wa bibi harusi hupata aibu, ikumbukwe kuwa somo na kungwi kwa mukhtadha huu ni watu wawili tofauti, ingawaje kungwi aweza kuwa huyohuyo ndio somo. Bibi harusi pia huwaibisha wazazi wake na yeye mwenyewe pia.

Aidha, Somo ni yule 'aliyemuokota' kigoli alipovunja ungo, ama yule aliyekabidhiwa amfundishe baada ya 'kuokotwa'

Kuokotwa ni msemo tu wa kwamba 'kuonwa mwanzo'

Yaani, binti alipovunja ungo basi yule mwanamke aliyemuona ama kujuwa kabla ya wengine ndio anakuwa 'amemuokota' na automatically anakuwa somo yake.

Enzi hizo, hata sasa ni fahari sana kwa wazazi pindi wakimuozesha binti yao akiwa bikra.

Kuna siri nzito juu ya kuoa bikra, hili linahitaji uzi wake, maana siku hizi imekuwa siyo ishu tena. Lakini jaribu kuuliza tu walio oa bikra, watakumegea baadhi ya siri hizo.

Nikipata muda nitaanzisha uzi huo.


2. Nimeombwa na wasomaji wapya wa uzi huu niipandishe stori yote kwenye post ya mwanzo ili waisome kwa urahisi.

Nitafanya hivyo, lakini nawasihi pia wapitie uzi wote kwa maana kuna yatokanayo ambako kuna mafunzo mengi yapo ambayo hayapo kwenye simulizi.
 
Kama wanavyosema kuwa wajinga huzeeka,,,naamini pia wenye busara na hekima huzeeka pia,mkuu nakupa hongera sana kwa kuzeeka na hekima zako.
 
Chief.. huyu Marry hakumla kimasikhara maana ule ufundi wa kile kitabu cha mzungu ulikuwa umekolea [emoji3]
 
Chief hapa uliikatisha kikatili sana [emoji3]
 
Taarifa kwa tuliokuwa tunawasiliana telegram na whatsapp.

Sipatikani kwenye namba ya DRC tena, nipo Tz kwa muda mrefu sasa namba ya DRC haifanyikazi tena.

Nitawa contact kwa namba nyingine. ASAP.
 
Taarifa kwa tuliokuwa tunawasiliana telegram na whatsapp.

Sipatikani kwenye namba ya DRC tena, nipo Tz kwa muda mrefu sasa namba ya DRC haifanyikazi tena.

Nitawa contact kwa namba nyingine. ASAP.
Asante kwa taarifa Mzee
 
Taarifa kwa tuliokuwa tunawasiliana telegram na whatsapp.

Sipatikani kwenye namba ya DRC tena, nipo Tz kwa muda mrefu sasa namba ya DRC haifanyikazi tena.

Nitawa contact kwa namba nyingine. ASAP.
Nimerudi hewani

Tutaonana soon kwenye social media
 
Amen
 
Thanks
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…