Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Natamani ni LIKE mara ya pili...Nimefuatilia kwa ukaribu hii simulizi yako mwanzo mpaka mwisho kwa sababu kuu tatu;
1.Ni hadithi yenye uhalisia(ya kweli) iliyisimuliwa kwa ustadi wa lugha ya kuvutia na matukio
2.Ni hadithi yenye mambo mengi ya kujifunza hasa kwetu sisi vijana
3. Ni simulizi ambayo kwa asilimia kubwa mikasa yake inafanana na historia ya maisha yangu ya ndoa kama vile;
[emoji818]Jina la mkeo (Hamida),herufi mbili za mwisho 'DA' zinafanana na jina la mke wangu(sitalitaja hapa)
[emoji818]Nimeoa chotara kiarabu(mwafrika na mwarabu) wenye asili ya Yemeni
[emoji818]Nikiwa kwenye mipango ya kumuoa alikuwa tayari keshatafutiwa mchumba Oman na posa ilishaletwa
[emoji818]Familia ya mke wangu ni waislamu na Mimi nilikuwa mkristo
[emoji818]Nilikataliwa kuoa kwa hofu ya 'kuharibu' hasa kwa upande wa imani
[emoji419]Tofauti ni kwamba Mimi na binti tulishakubaliana kuwa yenye ndiye atabadili dini ili kuwa mkristo,hapa nilishikilia msimamo.
Baada ya misukosuko mikali Namshukuru Mungu tulifunga ndoa ambayo ilianzia bomani(Serikalini) halafu baadae kanisani kwa ajili ya kubariki.
Nilichojifunza ni kwamba unapoamua kusimamia jambo ambalo unaliamini, uwe tayari kulipigania kwa gharama kwakuwa si Mara zote utafanikiwa kirahisi.
Onyo;
Katika mazingira kama haya ambayo wazazi au ndugu wanakuwa na wasiwasi wa kukukabidhi binti kwa sababu zozote zile,inapotokea umefanikiwa kumuoa kwa namna yoyote ile,(kwa ridhaa yake) basi huna budi kuhakikisha binti hajutii uamuzi wake,au wazazi hawajutii uamuzi wao.
Najaribu kufikiri kama Mzee Jamaal baada ya kuoa angerudia 'ukipanga' wake na kuanza kumtesa huyu binti(Hamida),au angerudia dini yake ya zamani(ukristo),hii kwanza ingemfanya Hamida ajute kwa kujitoa kwake,pia ingempoteza sana kiimani.
Lakini kikubwa zaidi ingewapa sababu (Mzee Burhani na mkewe)za kuamini kwamba walikuwa sahihi kukataa kumkabidhi binti yao kwa Jamaal kabla ya kushawishiwa na kukubali.
Mwisho,nakupongeza kwa sababu mpaka hapo umeweka viwango vya juu sana,kwa kuvunja ile hofu ya wazazi na ndugu na pia kufanya Hamida ayaishi maisha ya upendo aliyoyotarajia kutoka kwako.
Kauli iliyonivutia katika simulizi;
"Nilibadilika na kuwa mume mwema sana".
Ahsante.
Sent using Jamii Forums mobile app
Hili swali sijui nilirukaje!Katika ugawaji wako wa chakula, unamkumbuka Juma Swedi? Alikuwa anakaa kimara maarufu Sana enzi hizo kwa wizi wa chakula
Sent using Jamii Forums mobile app
[emoji28][emoji28],Asante mkuu,simulizi yako ina fundisho sanaNatamani ni LIKE mara ya pili...
Lakini hakuna option hiyo hahahaha [emoji23]
Sent from my Infinix X690B using JamiiForums mobile app
Nimeshavipata hivi bado kuvisoma tu.Vijana jitahidini msome vitabu hivi vitatu, mtajifunza mengi:-
1. "The Perfumed Garden" - Umar ibn Muhammad Nefzawi - 15th Century
2. "French Sex Art Manners" - Georges Valensin - 1970
3. "Kama Sutra' - Vatsyayan Richard Francis Burton
James Jason
Safi sanaNimeshavipata hivi bado kuvisoma tu.
Sehemu ya 16 imebeba hisia kali sana.SEHEMU YA 16
****************
Sherehe ziliendelea hadi usiku mwingi, Ruti alikuta bidhaa zake zote zimenunuliwa na alikabidhiwa hela yake yote, Dada mkubwa aliniuliza kama nimeelewana na Ruti, nikamwambia nimemaliza kazi, kilichobaki ni wazazi kupeleka maneno kwa wazazi wa Ruti.
Watu walikuwa wengi kwelikweli na Manyomba nzima kulikuwa na gari yangu tu Corona Lift-back, vyombo vya usafiri vingine vilikuwa baiskeli na mikokoteni ya kuvutwa na punda na ng'ombe. Watu walikunywa pombe (ya mtama) na togwa la mtama kwa wachache.
Asubuhi Vikao vya Kitaturu vilianza na kufikia maazimio mbalimbali, vijana waliotoka jando baina ya July 82 hadi sasa (June 83) walipandishwa madaraja na kuondoka katika utoto. Vijana hao sasa rasmi waliruhusiwa kuchumbia (ama kuchumbiwa), mida ya jioni pilika za vijana zikaongezeka huku wazee wakiburudika kwa pombe na nyimbo za asili.
Tarehe 26 jioni sherehe zilifungwa rasmi, baadhi ya watu walianza kuondoka, wengine walibaki lakini bado Manyomba kulichangamka. Kesho yake tarehe 27 tulirudi Ibaga na kuwapa mrejesho baba na mama kuhusu Ruth. Walifurahi, wakasema niwaachie watamalizana na wazee wenzao. Nami nilipanga mwezi Disemba nichukuwe likizo fupi tena kwa ajili ya kuja kumuoa rasmi Ruti.
Niliendelea kuongea na wazazi na majirani, nilitembelea mbugani kila siku (kwa Ruti) kwa kisingizio cha kwenda kuhuisha boma la mbugani, japo kweli nilifanya utaratibu na kuhakikisha panajengwa upya kama palivyokuwa awali lakini kwa ubora wa hali ya juu, niliweka kijana mwaminifu (motto wa mama yake mdogo Ruth) kwa ajili ya kuangalia ng'ombe tano nilizo zinunua (majike wanne na dume moja), nilitaka kuwapunguzia wazee wangu gharama za mahari kwakuwa tayari tulishaambiwa tupeleke debe la asali, ngombe mbili jike na dume moja, ngozi zilizotengenezwa mbili, mkuki, upinde pamoja na shilingi mia moja ambazo ningekuja kutoa wakati wa kushuhudia tukio la kutoa mahari mwezi Disemba na kisha kuoa kabisa kabla mwaka haujaisha.
Dada mkubwa na mumewe walisaidia kuangalia vizuri boma, na pakawa pamehuika.
Tarehe 2 July tulianza safari ya kurudi Dar es Salaam. Tulikuwa mimi nikiendesha, mdogo wangu wa Bagamoyo na mdogo wetu wa mwisho Rehema.
Tulianza safari asubuhi baada ya chai, saa nane mchana tuliwasili Singida (njia haikuwa rafiki, ni chini ya km 120), tukapata chakula na kuongeza mafuta kwenye gari kisha kuanza kuitafuta Manyoni ambapo tuliwasili saa kumi na mbili na nusu hivi.
Saa nne usiku tulifika Dodoma, tulilala lodge fulani maeneo ya Uhindini, na saa moja asubuhi tulianza safari baada ya kuongeza petroli na kuwasili saa nane mchana jijini Dar es Salaam. Safari hii nilikimbiza gari hadi ile alarm ililia (gari ikifika 110kph), nilifurahia sana jinsi Corona ilivyotulia barabarani, kwenye buti tulijaza mazagazaga kutoka kijijini. Saa nane na robo nilikuwa nimepaki Upanga nyumbani, mdogo wangu wa Bagamoyo naye alikagua gari yake kisha siku hiyo hiyo alitangulia Bagamoyo na kumuacha mke wake ambaye angemfuata kesho yake.
Shemeji, mke wa mdogo wangu alituandalia chakula, nasi tulijimwagia maji na kubadili nguo.
"Shemeji, Juzi tarehe 1 kuna simu ilipigwa, akaanza kuongea mwanaume kwa lugha gani sijui kiarabu mara kigereza halafu akapokea mwanamke akaongea kiswahili vizuri tu..."
"Enhe!?" Nikawa na hamu ya kujuwa zaidi
Tulikuwa bado tupo mezani tukimalizia kula chakula cha mchana...
"Nilimuambia kwamba umesafiri, akaniambia kuwa ukirudi nikupe namba hii upige kisha uombe kuongea na Hamida Binti Burhani, ndiyo nikajuwa kuwa ni dada yule wa kiarabu, tukasalimiana vizuri kisha akanitajia namba ambayo nimeiandika, ngoja nikuletee..." Akainuka na kwenda chumbani kisha akarudi na karatasi ndogo mkononi.
"00968..." Alianza kuitaja nikamkatisha
"Hebu nipe hiyo karatasi"
Akanipatia, nikainakili kwenye kitabu cha orodha ya namba za simu.
Nikanawa mikono na kwenda kwenye meza ya simu. Simu yangu ilikuwa haijaunganishwa kupiga nje ya nchi moja kwa moja, hivyo nilipiga kwa operator wa shirika la posta na simu.
"Opereta wa simu, naomba nikusaidie" Sauti ilisikika baada ya kupokelewa
"Ahsante, nahitaji kuongea nje ya nchi namba..." Nikamtajia.
Akaniambia nisubiri atanipigia. Ilikuwa inaelekea saa kumi kasoro. Mara nikasikia grriiiin grrriiiin, nikapokea, akaniambia subiri...
Kisha nikasikia "Hallow"
Ilikuwa sauti ya kiume.
"Kaifa!?" Ile sauti iliongea..
"May I talk to Hamida bint Burhan?" Nilijibu kwa kiingereza.
"Hamida, Hamida ,no, no, not here" kisha akawa anaita mtu mwingine ili aongee
"Hallow, Can I help you" sauti nyingine ya kiume ilisikika.
"Yes, I need to talk to Hamida" Nilisema.
"Oh, binti Burhani, she is not here, call tomorrow morning" Alisema.
Nikamshukuru kisha tukakata simu.
Kesho yake saa mbili asubuhi nikapiga na ikapokelewa na mtu mwingine anayeongea kiarabu tu, akampatia mwingine ndio tukaelewana..
"Hallo, may I talk to Hamida please!" Nilimwambia baada ya kunisalimu.
"Yes, wait a moment" Kisha nikasikia Hamidaaaa
Sekunde chache baadaye sauti ikasikika
"Hallow" Moja kwa moja nikaitambua sauti ya kipenzi changu...
"Hamida, mimi ni Jamaal" Nilisema kisha kukawa na ukimya sana.
"Nitakupigia saa nane mchana, huko inakuwa saa saba, uwe jirani na simu, sasa hivi nipo zamu" kisha akakata simu.
Nilifurahi kusikia sauti yake lakini nilipatwa na bumbuwazi hata sikujuwa niseme nini. Kupenda ‘buaha'.
Hamida akawa kama amesimamisha muda, saa haziendi, hatimaye nikapata wazo la kulala na kumuambia Shemeji na mdago wangu waniamshe saa sita na nusu ili saa saba niongee na simu kisha saa nane na nusu nimsindikize shemeji Kariakoo akapande basi za kwenda Bagamoyo.
Nikaanza kuutafuta usingizi, wapi, hauji, nikachukuwa kitabu cha hadith 'Dogs of war' alichoandika Frederick Forsyth na kuanza kusoma, haikunichukuwa muda mrefu usingizi ukanichukuwa.
Niligongewa mlango saa sita na nusu juu ya alama, nikajimwagia maji kisha nikawa tayari nikisubiri simu.
Saa saba na dakika kumi hivi simu ikaita, nikapokea, nikasikia sauti ya Hamida. Akaniambia kuwa ameshatoka kazini na hapo anaongea kwenye kibanda cha simu jirani na kazini kwake.
Akaniambia kuwa kumbe baba yake alikuwa na nia ya kumtenganisha yeye na mimi na kufanya mpango wa kupata mume huko huko Oman.
Hivyo walivyofika Muscat, kampeni ya kwanza ilikuwa ni geti kali, hakupata kutoka kwenda popote bila dada yake na shemeji zake kuongozana nao. Aliniambia kuwa aliishi maisha ya tabu kama yupo jela, kwa mwezi mzima (wa kwanza wote) alikuwa akilia tumoyoni akiwa chumbani asijue la kufanya.
"Baada ya miezi mitatu wakaanza kuleta wageni (wanaume) mle ndani kisha kuniaambia niwahudumie chakula, wakiondoka naanza kuulizwa kati ya wale wageni nani nimempenda ili anioe" Alisema hamida huku akionesha sauti ya huzuni...
"Nilikuwa nawakataa, lakini waliendelea kuwaleta wengine na wengine lakini hakuna niliye mkubalia" Aliendelea.
"Baada ya miezi nane kupita nikapata akili, niliwaambia kuwa, siwezi kumpenda mtu wa kuletewa, hivyo nitafute mwenyewe kwa kumuoana ama akiniona, hivyo nitafutieni kazi katika Hoteli kwakuwa mimi nina ujuzi wa mapishi, nitafanya kazi lakini naamini nitapata mtu wa kunioa huko huko" Alisema.
"Lakini kichwani nilikuwa nakuwaza wewe, sikuweza kupata namna ya kukuandikia barua wala kukupigia simu nikiwa 'jela' ya nyumbani, hivyo kwa njia hii nimefanikiwa..." Alisita kidogo kisha akaendelea.
"Kazi nimenza majuzi tarehe 1 mwezi huu wa saba, na nimepangiwa ratiba ya asubuhi hadi mchana tu, pia wananichunga muda wa kufika nyumbani japo si mbali kutokea hapa, ni mwendo wa dakika kumi tu kwa miguu..."
Mie nipo kimya tu namsikiliza kwa makini.
"Leo hii sijui itakuwaje nyumbani, watanigombeza sana lakini angalau nimepata wasaa wa kuongea nawe. Siku hiyo hiyo nilyoanza kazi ndio nikapiga simu huko lakini nikaambiwa umesafiri". Aliendelea kusema
"Kazi wamenitafutia kwenye restaurant moja ya Waturuki, hivyo kila siku asubuhi hadi saa nane mchana ninakuwa Chef wa zamu" Alimaliza.
Nilimuonea huruma sana, na nikapata kujuwa nini kilichomsibu hadi akae kimya miezi tisa hivi tangia tuwasiliane mara ya mwisho.
"Pole sana kipenzi changu Hamida, na hongera kwa kupigania uaminicho, bila shaka mimi nawe tumeandikiwa tuwe mume na mke, kama ndivyo hakuna atakayeweza kuzuia, bali watachelewesha tu" Nilimpa pole na kumtia moyo.
"Mimi huku tangia umeondoka sijamwona mwanamke mwingine (?) zaidi yako, mawazo yangu yote yapo kwako, lakini leo nimefarijika sana kuongea nawe" Nilisema.
"Kutokana na kazi yangu ilivyo siwezi kuja huko, hivyo nakutegemea wewe ufanye unavyoweza ili uje Tanzania, tufunge ndoa, na kwa kuwa tunajuwa kikwazo kipo wapi basi itakuwa rahisi kushughulika nacho."
Tuliongea sana, kisha tukaagana na kuwekeana utaratibu wa muda huo yeye kunipigia.
******
Siku hiyo baada ya kuongea na Hamida mchana, nilikuwa na furaha sana, chakula kilishuka vizuri. Shemeji alikuwa tayari saa nane na robo hivi, hivyo nilimsindikiza stendi (Mkunguni St / Congo St) ambapo alipata basi la Champsi Mulji Co. Ltd maarufu kama Chemsi. Kampuni hiyo ilikuwa na mabasi mengi lakini basi hilo (Leyland CD) siku hiyo vijana walikuwa wanaiita 'Msala' kutokana na mpangilio wake mzuri wa rangi nyekundu na nyeupe wakilinganisha na miswala ya kuswalia wakati huo ilivyopambwa.
***
Siku moja katika kuongea na Hamida, aliniuliza kama nimeshafungua ile handbag aliyoniachia. Nikamjibu kuwa sijafungua bado, akaniambia nikaufungue, kweli jioni ile nikauchukuwa na kugundua, kulikuwa makeup set, handkerchief, makorokoro mengine ya wanawake lakini kwenye sehemu palipofungwa zipu, nilipofungua nilikuta kuna hela zilizofungwa kwa karatasi nyeupe na rubberband, zilikuwepo hela za Kenya na chache za Tanzania.
Kwenye ile karatasi aliandika:-
"Kwako mpenzi wangu Jamaal,
Salamu nyingi sana zikufikie hapo ulipo, utakapo kujuwa hali yangu mimi ni mzima wa afya, hofu na mashaka ni juu yako wewe ambaye sasa upo mbali na upeo wa macho yangu.
Madhumuni ya barua hii ni kutaka kukujulisha kuwa pamoja na ugumu unaoupitia lakini usikate tamaa, hata mimi sintokata tamaa kwa kuwa nakupenda sana tena sana na wala siyo kwa sababu ya kukwepa kuolewa na babu wa Oman.
Hivyo nitahakikisha narudi Tanzania ili tutimize lengo letu la kuoana na kuishi pamoja.
Naomba uvumilie na uniamini, ipo siku tutakuwa wote kama mke na mume.
Nakutakia kusubiri kwema.
Wako akupendaye daima,
Hamida."
Ilikuwa imewekwa seal ya busu (kiss) yenye lipstick ya pink, alichora pia ‘kopa’ na kuweka alama ya mshale. Nilipoinusa ile barua ilikuwa inanukia harufu yake, yaani harufu ya perfume ya Hamida.
Nafikiri ndiyo barua niliyowahi kuisoma kwa kuirudia mara nyingi kuliko zote maishani, nililala nayo kifuani usiku ule, lakini kila nikimkumbuka nilikuwa nachukuwa naisoma tena, na tena.
Siku ya pili yake (baada ya kuifungua ile handbag nilimuuliza kuhusu zile pesa ndipo akaniambia kuwa ni hela zake za akiba alizo-save wakati akiwa KUC, alizitunza kwa ajili ya kujinunulia kitu atakacho wakati wa harusi yake nje ya bajeti ya wazazi.
Tuliendelea kuwasiliana na Hamida karibu mara nne au tano kwa wiki, tuliungana tena kwa kutumia simu, mara nyingi yeye ndiye alipiga kwa kuwa gharama za kupiga nje kutokea Tanzania zilikuwa kubwa sana lakini pia yeye alikuwa anatumia 'telephone boothes' tofauti tofauti.
=
Mwezi wa kumi nilipokea simu kutoka Singida mjini, ni dada yangu mkubwa alinipigia nikiwa afisini. Akanijulisha habari za kusisimua...
"Hallow" Sauti ya Dada
"Hallow, Shikamoo dada" nilimsalimia.
"Marhaba, leo tumekuja na shemeji yako mjini kufuatilia dawa za kutibu ng'ombe, lakini pia kuna habari iliyonifanya nikupigie simu" Alisita kisha akaendelea
"Ruth ana mimba" Alitoboa
"Tena imeanza kuonekana kabisa ina miezi minne sasa, na ameniambia ya kwako" Alisema
Fasta kichwa kikaanza kuvuta kumbukumbu siku ile mtoni ndipo nikajuwa inawezekana kweli alikuwa kwenye heat period, maana ule utelezi ulikuwa wa aina yake, naye alifurahia sana siku ile na kutaka kurudia tena na tena ingawaje nilirudia mara moja tu.
Mbona hakuniambia nisimalizie ndani?
Alinitega?
Mbona mimi na Dada ndio tuliweka mazingira ya kumgegeda!?
Au hajui mambo ya siku za hatari?
Nilijiuliza maswali fasta fasta.
"Nashukuru kwa taarifa, ni kweli ni kazi yangu" Nilisema kisha Dada akacheeka sana.
Nakumbuka nilimgegeda mara mbili tena baada ya sherehe nilipokuwa naenda mbugani.
"Yani hiyo ni yangu kabisa, mwambie asiwe na wasiwasi, wazee wawahishe mahari tu ili nikija Disemba nimuoe kimila kisha nihalalishe kidini.
Tulishazungumza na Ruth kuhusu yeye kubadili dini kabla ya kumuoa na alikubali.
"Wazazi walishapeleka sehemu mahari bado ile shilingi mia na debe la asali." Alinijulisha.
"Ruti siku zake zilipopitiliza, akanifuata akaniambia, ndipo nami nikamjulisha mama, naye akamwambia baba ambaye aliamua wapeleke mahari kabisa" alisema Dada.
Tuliongea na mambo mengine kisha tukaagana na kukata simu.
Habari ili ilinichanganya kidogo ukizingatia tayari nina mawasiliano ya mara kwa mara na Hamida na hususani kwa barua yake aliyoniachia.
"Hamida akijua hii, ndoa naye basi" nilijisemea.
Nikaanza kuwaza jinsi nilivyoanza kukusanya 'silaha za mashambulizi' dhidi ya mzee Burhani, tayari hoja za kumvunja nguvu na kumuonesha udhaifu wake zilisha andaliwa.
Nilipanga kuwatumia Imamu wa msikiti anaoswali na mzee mmoja pale Shibam.
Tulishapanga Hamida mwezi ujao (Novemba) atoroke arudi Tanzania afikie Zanzibar kwa mamkuu wake, passport waliyoificha tayari aliona ilipo siku ile alipotakiwa kiripoti kazini ili wachukuwe taarifa zake muhimu. Hela yake nyingi alitumia kwenye kupiga simu kwangu lakini nilimuambia akiwa tayari anijulishe ili nimtumie tiketi.
Kichwa kilikuwa kimeanza kuwaka moto kwa kuwaza kupita kiasi.
Kazini napo hali ya upatikanaji wa bidhaa ilizidi kuwa mbaya, mapato na huduma zilikuwa zinashuka kila kukicha (kila uchao) lakini tuliendelea kupambana hivyo hivyo.
Mwezi Novemba Hamida hakuweza kuja kwa sababu alisema kuwa bado si muda mzuri wa yeye kutoroka, bado alikuwa anajenga uaminifu kwa shemeji na dada yake ambao walikuwa wanadhani muda wowote posa italetwa kwao.
Hamida alikuwa mzuri, yani mrembo wa maumbile na tabia pia, ni mwanamke aliyeandaliwa vyema kuwa mke na mama bora kwa familia kama ilivyo kawaida kwa familia za kiarabu kuhusu wanawake.
Haikuwa rahisi kwa kijana rijali amuone Hamida kisha ajue kuwa hajaolewa akaacha kumposa. Kutongozwa hapo kazini kwake alishazoea lakini alivaa pete ya uchumba niliyomnunulia Unguja ndiyo ilikuwa kinga yake (kulingana na msimamo alionao)
Mwezi wa kumi na mbili sikuweza kuchukuwa likizo kutokana na hali ya afisini ilivyokuwa. Kijijini nako Ruti mimba ilishakuwa kubwa, akahamia pale bomani kwetu na kuishi hapo pamoja na kijana aliyekuwa anasaidia kuchunga mifungo ambapo kwa bahati nzuri alikuwa ni ndugu upande wa mama yake.
Nilituma hela kwa ajili ya asali na ile hela waliyoitaka, wazee wangu walikamilisha mahari yote kilichobakia ilikuwa ni ndoa.
Mwezi Disemba ulipita, Januari, Februari hadi Machi mwishoni nilipopigiwa simu na Shemeji kwa dada mkubwa (alikuja Singida mjini), akaniambia kuwa Ruti anaumwa, amepelekwa dispensari ya Chemchem.
Dada mkubwa na mdogo wake wote walikuwa wakimsaidia pamoja na wazazi wake Ruti. Ilikuwa ni uchungu, muda wa kujifungua ulikuwa umewadia.
*****
=
Mashambulizi yalianza kwa mzee Burhani. Imamu wa msikiti anaoswali mara kwa mara pale magomeni (mkauni) pamoja na mzee mmoja mtata sana pale Shibamu kisha baadaye wakamuongeza na mzee Shebe aliyekuwa akikaa mtaa wa sunna. Alikuwa ana asili ya Umanga fulani hivi naye baadhi ya mabinti zake aliwaoza kwa vijana waafrika (weusi)
Kila siku pale Shibamu walianza kumsakama mzee Burhana kidogo kidogo. Kero kwake ikawa kubwa hadi kuna siku pale kijiweni ikawa ni mada maalumu.
"Ninyi waarabu mmekuwa mnafanya ubaguzi sana kwa vijana wetu wasioe kwenu, mbona nyie vijana wenu wanawapa ujauzito mabinti zetu tena hata kuoa hawataki, sasa kijana wa watu mstaarabu tena amesilimu ndani ya mikono yako unashindwa kuridhia binti yako aolewe naye!?" Imamu alisema...
"Angalia mimi binti zangu wengi wameolewa na wazaramo na wandengereko mbona wanaishi vizuri tu na kizazi kizuri sana" Mzee Shebe aliongeza...
"Unajuwa sisi sote ni ndugu, yaani binadamu wote ni ndugu, tuna udugu wa namna mbili, udugu wa asili na udugu wa kidini, sasa Jamaali kote kote anastahili..." Mzee mtata wa Shibam, aliongea kisha akaongeza...
"Kumbuka mzee Burhani, pindi Nabii Nuhu alivyokuwa akiwaita watoto wake wakubwa watatu Saam (Shem), Haam (Ham) na Yaafith (Japhet) akitaka kuwahusia..." Ameza mate na kuendea
"Katika hao, Ham alimtuma mtoto wake mkubwa aitwaye Misri (Masri), ambapo baada ya kupokea usia pia aliambiwa wadogo zake wakizaliwa pia awalete (mama yake alikuwa mja mzito), alipojifungua walizaliwa watoto wawili pacha mmoja mweusi (bantu) na mwingine mweupe (arab).
Hawa watoto pacha walitabiriwa kuwa mmoja (mweusi) atashika sana dini lakini hatokuwa na mali nyingi na mweupe atakuwa na mali nyingi na pia kizazi chake watashika dini, lakini akamsihi sana yule mweupe asimsahau mweusi kwa kumsaidia, kwani wote ni ndugu" Alitulia kisha akaendelea...
"Hivyo Waarabu na Waafrika (weusi) ni ndugu kabisa kupitia mjukuu wa Nabii Nuhu aitwaye Misri. Yaani hapo wewe ni Burhan ibn dash dash kisha ibn Misri ibn Ham ibn Nuhu, na Mimi hapa Muharami (alijitaja jina lake) ibn dash dash ibn Misri ibn Ham ibn Nuhu. Hivyo sisi ni ndugu kabisa ingawaje mie nina ngozi nyeusi" Alitulia kisha mwingine akapokea...
"Ina maana kwamba kizazi hiki cha Africa ni ndugu kupitia Mjuu kuu wa Nuhu Misri Ham, hivyo haifai kubaguana wala kutengana, yafaa kusaidiana, na masuala ya ndoa yanaongeza mshikamano katika udugu wa kidamu pamoja na wa kidini..."
Jina la nchi ya Misri (Egypt) ilitokana na jina la mjukuu wa Nabii Nuhu kupitia mwanawe Ham.
Alishambuliwa pale huku mimi niko pepembeni nimetulia nawasikiliza huku nikiwa namwamuru muuza tangawizi aendelee kumiminia kila amalizaye kunywa.
Ijumaa hiyo ilikuwa ya moto sana kwa Mzee Burhani ambaye mwanzo alikuwa akijibu mashambulizi lakini baadaye alizidiwa na hoja na kuamua kubaki kimya akisikiliza tu huku ameinama kidogo...
"Dini inataka ndoa zifanyike haraka, ni moja kati ya mambo matatu ambayo yanatakiwa kuwahishwa; mtu akitaka kusilimu ni muhimu kuharakisha, mtu akitaka kuoa vivyo hivyo ili mradi masharti ya ndoa yote yatimie, na mtu akifa basi yafaa awahishwe kuzikwa, yote haya yana faida kwetu sisi wanadamu." Imam alimeza mate kisha akaendelea..
"Muoaji yupo, muolewaji yupo na ameridhia kuolewa na Jamaal, au keshaolewa!?" Alihoji kwanza Imam
Mzee Burhan alitingisha kichwa kulia na kushoto kuashiria hapana, Imam akaendelea...
"Muoaji yupo, umesikia bwana, muolewaji yupo na yupo tayari kuolewa na muoaji, ni rizki yake kijana wetu Jamaal, ridhia tu amuoe..."
"Uwezo wa kulipa mahari anao, au huna Sheikh Jamaal? " Aliuliza kishabiki, nikajibu ninao, akaendelea...
"Walii wewe upo, wasomaji hutuba ya ndoa tupo na sharti nyingine zote zimetimia, usifanye ubahiri, unaweza kuleta madhara kwa mwanao na jamii kwa ujumla, legeza moyo kaka!" Alisema huku akimgusa bega maana alikaa jirani naye kisha akaendelea...
"Au hamjamchunguza kama Mtume Muhammad (Rehema na Amani zimwendee) alivyotuasa kwamba akikujieni mtu akitaka kuoa basi mchunguzeni tabia yake na kama ana dini; kwani Jamaal hamjui tabia yake? Na kwenye Uislam wewe mwenyewe si ndiye uliyemleta msikitini ukaniambia amesilimu mbele ya familia yako!?" Alihoji, mzee Burhani alikuwa kimya.
Mimi hapo kwenye tabia nikawa najiaemea moyoni, wangelijuwa hawa! Nikajipa moyo kwamba lakini ukishasilimu dhambi zote Allah (aliyetakasika) huzifuta na kuanza upya. Ila sasa 'kasheshe' ya Ruti nayo nikawa nayo moyoni tu hata sikujuwa itakuwaje mbele.
********
Usiku uleule nilipigiwa simu na mzee Kassim (Katibu Kata) akiniambia kuwa mzee Burhani alituma ujumbe kwake ili kesho adhuhuri tuonane nyumbani kwa mzee Burhani.
=
"Grriiiin greiiiin, griiiiin griiiin" simu ya ofisini iliita.
Nikainua mkonga wa kusikilizia nikasikia...
"Boss, kuna simu kutoka Singida"
"Unganisha" Nilimjibu na kuendelea kushikilia simu..
"Hallow" Sauti ya upande wa pili ilisema.
"Hallowa, habari?" Nilijibu
"Njema kiasi" sauti ilisikika
"Wewe ni nani?" Niliuliza
"Une ne shemejiako ku..." Alianza kuongea kinyiramba
Ndipo sauti nikaikumbuka vizuri, hali ya hewa nayo haikuwa nzuri maana simu ilikuwa inakwaruza...
Nina Shemeji mmoja tu mnyiramba, mwingine ni Msukuma, na Rehema bado alikuwa hajaolewa.
"Ahaaaaa, bwana shemeji" Nilimchangamkia, ni shemeji yangu mchangamfu sana, alimuoa dada yangu Rahel (Rachel) aliyeniachia ziwa. Dada wa kwanza (Rabeka) aliolewa usukumani.
"Nimetumwa nije nikupe yaarifa mbili" Akasita
"Enhe!?" Niliuliza huku mapigo ya moyo yakaanza kwenda mbio. Shemeji yangu huyu huwa mchangamgu na ana utani mwingi, lakini leo...!? Sijui!!??? Nilijisemea kimoyomoyo
"Enhe?!" Nilisema
"Moja mbaya na nyingine nzuri" Akasita...
"Enhe, hebu anza na nzuri" nilijitia moyo...
"Eeee, umeshakuwa baba, umepata mtoto wa kiume..." Akasita
"Enhe" nilisema
"Bahati mbaya mama yake amefariki" Alimaliza.
Kukawa na ukimya wa muda mrefu, kisha nikamshukuru kwa taarifa lakini nikamwambia asirudi kijijini, saa mbili usiku anipigie tena (reverse call) kwa namba ya nyumbani.
*****
"Boss vipi?" Betty aliniuliza alivyokuja mezani kuchukuwa mafaili, nilikuwa nimejiinamia kwa mawazo...
"Nimepata taarifa ya msiba kijijini, ni msiba unaonihusu, sina budi kwenda kesho asubuhi." Nilimjibu.
Betty alinifariji bila hata ya kuuliza nimefiwa na nani.
Kazi hazikufanyika tena, nikiamua nitoke afisini nielekee nyumbani kuanza kujipanga kwa safari.
Wakati natoka, Betty aliniuliza nimefiwa na nani, nikamjibu mchumba wangu amefariki.
"Mwarabu amefariki, oh masikini, sasa mbona simu imetoka Singida!?" Alihoji
"Hapana, siyo mwarabu, yeye bado yupo Ughaibuni huko, nilivyoona wazazi wake hawaeleweki niliamua kuchumbia kijijini" Nilimjibu.
"Oh, pole sana" Alinifariji
"Ahsante, kesho asubuhi nitawahi hapa, naomba nikukute maana nitakuwa 'njia moja' kuelekea Singida.
Maneno 'njia moja' ama njia namba moja (mbili au tatu nk) yalikuwa maarufu kwa watumiaji wa usafiri wa reli, ikimaanisha treni ipo tayari kuondoka nk.
*****
Nilifika nyumbani na kumueleza Rehema yaliyotokea na kumwambia saa mbili usiku tutapata taarifa zaidi.
Nikatoka kuwahi madukani na kununua baadhi ya vitu muhimu ikiwemo sanda, khanga, vitenge, na kuchukuwa vyakula kama Sukari na mchele, bidhaa hizi zilikuwa adimu sana kijijini na hata nchini kwa ujumla kwakuwa hali ya uchumi ilishafikia pabaya sana. Kisha nikakimbia Bagamoyo kwenda kumuandaa mdogo wangu ili twende naye.
Saa mbili usiku simu iliita na kusikia sauti ya mwanamke ikiniuliza...
" Jonas kutoka Singida anataka kuongea nawe kwa gharama za kwao, je upo tayari?"
"Ndiyo, nipo tayari" Nilijibu
"Ok, Subiri usikate simu" Alisema kisha nikasikia milio ya krrrrrruuuuu krrrrruuuuu kwa mbali kisha "Hallow"
Alikuwa Jonas ambaye ndiye Shemeji yangu.
Alinieleza...
"Jana Ruti alizidiwa, njia ilikuwa ndogo (ama haifunguki?!) mtoto alikuwa hapiti, hivyo wakaomba landrover ya mishen iwasaidie kuwapeleka Zahanati ya Mkalama ambapo napo walishindwa kwa kuwa ilibidi afanyiwe upasuaji hivyo wakaamua haraka wamkimbize Hospitali ya Kiomboi. Walifanikiwa kufika salama lakini presha ya Ruth ilishuka sana wakati wa upasuaji na hakuweza kuishi, lakini mtoto walifanikiwa kumtoa salama na alilia baada ya kupigwa makofi mawili. Mwili wa marehemu mpaka nakuja huku leo tarehe 5 (April) ulikuwa bado upo Hospitalini (mochwari) na mtoto anaendelea vizuri chini ya uangaliza wa mke wangu na shemeji Rabeka (Rebecca)"
Nilimuuliza maswali mawili matatu kisha tukaagana, lakini nikamwambia asiondoke Singida kwa kuwa mimi nitampitia Twende wote kijijini.
Asubuhi na mapema, mdogo wangu wa Bagamoyo alifika Upanga na gari yake Dutsun pickup.
Tukahamishia mizigo niliyonunua kwa ajili ya kwenda nayo kijijini kwenye pickup na kufunga turubai vizuri.
Aliendesha mdogo wangu, tukapitia afisini na kumuaga Betty baada ya kumpa taarifa vizuri ya msiba kisha tukapitia kujaza mafuta na kuondoka. Ilikuwa majira ya saa tatu na nusu asubuhi.
Alikimbiza sana mdogo wangu, saa kumi tulikuwa Uhindini Dodoma tunakula na kuongeza mafuta. Saa nne usiku tulikuwa Singida, tukampitia Shemeji wanapofikiaga ndugu zetu pembeni ya Hospitali ya Mkoa, na tuliondoka muda huo huo baada ya kujaza gari full tank kwa mara ya tatu.
Saa saba kasoro usiku tulifika Kinampanda Hospital. Tuliwakuta Dada zangu na mama yake Ruth na pia Shemeji yangu kwa dada mkubwa alikuwa amefika jioni hiyo.
Kilio kilitawala, tukabembelezana tukatulia.
Asubuhi taratibu za kawaida zilifanyika, tukapewa mwili, tulitandika godoro dogo ambapo tulilaza mwili, mizigo na sisi wengine tukajibanza sehemu iliyobakia.
Mtoto alishikwa na Dada mkubwa aliyekaa mbele, mdogo wangu wa Bagamoyo aliendesha.
Mdogo mdogo tulienda hadi tukawasili Ibaga mida ya saa saba na nusu hivi mchana.
Nilishuka pale kwa wazazi wangu, gari iliendelea hadi mbugani nyumbani kwa akina Ruth (R.I.P)
Jioni ileile mdogo wangu alinifuata na mimi pamoja na wazazi wangu tukajumuika msibani ambapo tulizika kesho yake baada ya misa takatifu Kanisani Chemchem na kisha misa nyingine nyumbani kwenye eneo la makaburi yetu walipozikwa Babu na Bibi.
*********
=
Baada ya kupokea simu kutoka kwa mzee Katibu Kata (siku hiyo Ijumaa tar 30 March 1984) nilifurahi sana, nikajuwa mdahalo wa mchana ulifanya kazi vizuri. Nililala kwa furaha na kuona kama saa haziendi vile.
Saa sita Jumamosi nilimpitia mzee Katibu Kata (tulizoea kumwita hivyo badala ya kutaja jina lake), kisha tukaenda kuswali msikiti wa Mkauni, tulionana naye baada ya swala tukaenda pamoja nyumbani kwake.
Tulimkuta Shangazi yake Hamida, Shemeji yake mzee Burhani, mamaza mzazi wa Hamida pamoja na yule mama Fungameza.
Tuliandaliwa chakula, tukawa tunakula huku mzee Burhani akiongea...
"Kwa kweli baada ya yale maongezi ya jana pale Shibam, nimejifikiria sana. Usiku mzima sikupata usingizi vizuri nikiwa natafari maneno yale." Akawa anakula kidogo kisha anaendelea...
"Nilikata shauri kuwa yafaa leo tukutane, japo kwa uchache lakini angalu mliopo msikie kauli yangu, hivyo nilimtumia ujumbe mzee Kassim ili akujulishe mje tuweze kuweka sawa suala hili" Akapiga matonge mawili hivi kisha akaendelea...
"Kwa kifupi sasa nipo radhi Hamida aolewe na Jamaal" Akatulia akala weee kwanza kisha akaendelea...
Wakati huo mimi nimejawa na furaha kubwa moyoni kwamba hatutotumia njia za panya kutimiza ahadi ya kuoana na Hamida, bali itakuwa halali. Chakula niliona nimeshiba tu baada ya kula tonge chache za wali samaki (papa mbichi chukuchuku)
Mama Warda na Shangazi walikuwa wanatabasamu kwa furaha, Mama Fungameza alipiga kigelegele pale aliposikia "...nipo radhi binti yangu Hamida aolewe na Jamaal...", Shangazi na Mama Hamida nao wakapokea kwa vigelegele.
" Eee kwa kuwa tulishapokea posa mwaka jana, hapa kilichobaki ni kumjulisha Hamida kama yupo tayari kuolewa na ataje mahari yake."
"Majibu ya mahari nitampatia mzee Kassim" Alimaliza mzee Burhan.
Mume wake shangazi alifurahi sana na kumpa mkono shemeji yake baada ya wote kunawa mikono, kisha wote tukapeana mikono kwa furaha.
"Shemeji umeamua jambo zuri sana, Mwenyezi Mungu atakulipa. Ulikuwa unamtesa tu bintiyo, Jamaal hana shida yoyote ya kumfanya asimuoe bintiyo, amechunguzwa kwelikweli na wataalamu wa uchunguzi, hakika umepata mkwe bora, hongera sana." Alisema mume wake aunt.
Mama Warda hakusema neno, alikuwa amefurahi tu hata nilivyokuwa namuangalia usoni niliona waziwazi furaha yake.
Ilipigwa fat'ha na kuombwa dua. (Fat'ha ni msemo wa tamko kuashiria isomwe suratil' fat'ha kisha kufuatia na dua)
Baada ya dua tulipeana mikono tena kisha tukaaga na kuondoka. Nikampeleka mzee Katibu Kata kwake nami nikarudi nyumbani nikiwa mwenye furaha isiyo kifani. Ilikuwa tarehe 31 Jumamosi, weekend hiyo nilienda Drive in Cinema pamoja na mdogo wangu Rehema kufurahia uamuzi wa mzee Burhani.
Jumapili nilienda Bagamoyo kumjulisha mdogo wangu pamoja na mkewe kuhusu maamuzi ya mzee Burhani, wote walifurahi sana. Nilirudi Dar na nazi na mihogo kama kawaida nikitoka Bagamoyo.
Jumatatu nilifika kazini nikiwa mwenye furaha na bashasha hadi Betty aliniuliza...
"Kulikoni Boss una furaha hivyo na hali ya uchumi imeshuka sana ofisini"
Nikamfuata kwa mtindo kwa kucheza, nikamshika mkono, nikamzungusha, aka respond vizuri, tukawa tunaswing, kushoto na kulia kama jahazi mawimbini kwa kuzama na kuinuka, huku nimemtolea macho ya furaha na tabasamu matata kisha nikafungua mdomo...
"Nimekubaliwa kumuoa Hamida, taraa taraa, taraa taraaa!" Nilijibu na kuendelea kumuongoza kucheza.
Hapakuwa na wimbo uliokiwa ukiimba (kuchezwa) ilikuwa ile ya kimyakimya, ila baada ya sekunde chache nilimuachia na kila mmoja aliendelea na kazi yake.
"Kweli, mvumilivu hula mbivu..." Alisema Betty.
"Kabisa, na subira yavuta kheri" nilijibu.
Nilifanya kazi kwa bidii zaidi siku hiyo. Ilipofika saa nane na dakika kumi hivi mchana simu ikaita.
Ilikuwa simu ya Hamida...
"Cheichei Bibie!" nilisema
"Cheichei Bwana!" alijibu Hamida na wote tukacheka kwa furaha.
Akaniambia...
"Baba ameniambia kuhusu kikao cha juzi mlichokaa, pia ameniambia nifanye utaratibu wa kuacha kazi na kurudi Dar ea Salaam..."
Alieleza kwa furaha sana hadi akawa analia...
"Leo tarehe 2 , hivyo sisubiri hadi mwisho wa mwezi, kesho tu naandika kuacha kazi kwa notisi ya saa 24" Alisema
Tuliongea kwa furaha pale na kumshukuru Mwenyezi Mungu kisha tukaagana na kuahidi kunipigia simu usiku kutokea nyumbani bila kificho sasa.
Siku ya Jumatano asubuhi nililetewa bahasha na mzee Kassim afisini, moja kwa moja nilijuwa ni majibu ya mahari. Nikaisoma na kukuta kama vilevile alivyoniambia Hamida siku za nyuma.
Sehemu ya barua ilisema...
"....Mahari ya binti yetu Hamida ni kama ifuatavyo:-
1. Kitanda futi sita kwa sita
2. Kabati la vyombo (show-case)
3. Kabati la nguo milango mitatu
4. Dressing table
5. Kusoma 'Ayatu Kursiyu' mara tatu.
....... ....... .......
Wabillah tawfiq
Wazazi wa Hamida bint Burhan."
Hakukuwa na kiwango cha hela. Kwa mahari hiyo tayari nilikuwa nimeshajiandaa, ila Suratil Yassin sikuwa nimeikariri yote, hata hivyo nimefurahi kwakuwa nimebadilishiwa na kupewa nisome Ayatul' Kursiyyu (Aya tukufu)
Tulifurahi na mzee Kassim kisha akaaga, nikamchukulia teksi akaondoka.
Siku moja baadaye (alhamisi mchana tarehe 5 April 1984) ndipo nikapokea taarifa ya kifo cha Ruth ambapo alifariki usiku wa Jumatano kuamkia alhamisi.
*****************
Itaendelea .....View attachment 1361067View attachment 1361068View attachment 1361069
James Jason
Babu hukufika nkalankala,mwanga,nkungi,gumanga nk?Kuna majukumu nimekuja kufanya Wilaya ya Mkalama,nimefika maeneo ya Nduguti,Msingi,Mwanga mpaka Mwangeza,nikasema haya ni maeneo ya Mzee wetu!
Gumanga nilifika, hata Nkungi wakati huo kulikuwa na kambi ya wenye ugonjwa wa ukoma.Babu hukufika nkalankala,mwanga,nkungi,gumanga nk?
Can you share your experience!?Hii story.. has taught me patience ..To never give up.. and that true Love always finds a way
Wajulishe na wengine waje wafurahie, wajifunze na kuburudika pia.Mzee Ubarikiwe kwa Uzi huu, Una Kila aina ya Mafunzo, Burudani na Kuchekesha pia. Hakika Hii Ninkazi Safi ya Fasihi. Nimeusoma Huu Uzi Mwaka Huu, sikua nautilia maanani siku za Nyuma, Nilikosea sana na kujinyima mengi.
Mkuu Tayukwa wee hii ushaisoma???? Ngoja niisome nasikia watu wanaizingumzia sana!UHUSIANO WANGU KIMAPENZI NA HAMIDA
Utangulizi.
'Mama watoto' aliridhia mimi kuandika simulizi hii kwa masharti.
Moja ya masharti nijitahidi kutoacha mlango / milango wazi itakayoruhusu watu kuunganisha dots...
Masharti mengine kwa kuwa ni sehemu ya codes, sintoyaeleza.
Hivyo katika simulizi hii nitaongeza 'chumvi' ama 'kuongeza maji' ili kuleta ladha kusudiwa.
Hamida ni mke wangu ambaye "hajaniacha"
=
=
=
Angalizo:
Picha ni kwa hisani ya "google"
Hazina uhusiano na simulizi hii.
Pia kuna sehemu inaweza kuamsha hisia za mapenzi,
Simulizi hii haina uhusiano na Hamida aliye-trend kwenye mitandao ya kijamii hivi karibuni.
Majina yote ya watu katika simulizi hii hayatokuwa halisi isipokuwa machache sana kwa sababu maalum.
SEHEMU YA KWANZA
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
"Hodiii!, hodi hodi humu ndani"
Nilibisha hodi huku nikigonga mlango kwa kutumia kipande cha chuma kilichoning'izwa maalum kwa ajili hiyo.
"Karibu, fungua mlango umeshindikwa tu"
Sauti nyororo ilisikika kutoka ndani.
"Starehe"
Nilijibu huku nikisukuma mlango mzito wa mbao ulionakshiwa kwa ustadi mkubwa. (Neno 'starehe' enzi hizo ndio lilitumika kujibu pindi ubishapo hodi na kukaribishwa)
Nilipofungua mlango nikakutana na korido ndefu nyembamba (wakati huo iliitwa 'ukumbi' japo siyo kama kumbi tuzijuazo leo), pembeni kulia na kushoto kulikuwa milango, wa kushoto ulikuwa mpana ambapo ulikuwa wazi ukiwa umesitiriwa na pazia zuri jepesi lenye 'kuangaza' (transparent) la rangi nyeupe, upande wa kulia mlango ulikuwa umefungwa, na milango mingine mitatu pia ilikuwa imefungwa.
Mbele mwisho wa korido kulikuwa na mlango ambao ulikuwa wazi kiasi cha kuweza kuona nafasi kubwa iliyokuwepo na sehemu ya uzio wenyeji waliita uani (sikuhizi ukisema uani watu watajuwa ni maliwatoni)
************
"Karibu tupo huku varandani"
Ile sauti nyororo iliendelea kunikaribisha na sauti hiyo ilitokea upande ule wa pazia jepesi angavu ambapo nilivyoingia nikatambua kuwa pale palikuwa ndiyo sebuleni.
Kabla ya kuingia nilivua viatu vyangu (raba - Morogoro shoes), havikutoa harufu mbaya kwa kuwa ndiyo nimevivaa kwa mara ya kwanza baada ya kuvinunua, vilikuwa vya rangi ya bluu na soksi zangu nyeupe. Hapo mlangoni kulikuwa na viatu vya sandarusi vyenye ukubwa tofauti pea tatu... nikajuwa utaratibu wa kuingia humo ni pamoja na kuvua viatu.
Nilipekenyua pazia kulia na kushoto na kupiga hatua kuvuka kivingiti cha mlango na kukanyaga zulia zuri la manyoya manyoya.
Ndani niliwakuta wanawake wawili na mtoto mmoja mdogo wa chini ya miaka mitano. Wale wanawake mmoja alikuwa mwafrika, amejitanda vizuri ushungi huku akiwa ameshika ukili (alikuwa anasuka mkeka).
Wote walikuwa wamekaa chini na kuegemea mito midogo, hapakuwa na viti bali meza ndogo iliyo chinichini sana jirani na zulia.
Yule mwanamke wa pili alikuwa mweupe, asili ya Asia, na sikuweza kufahamu maramoja kama alikuwa Mwarabu ama Mhindi. Alikuwa anakoroga maji ya rangirangi akichanganya sukari na yale maji, bila shaka alikuwa anaandaa "ashkrim", watoto walikuwa wanaita hivyo. Zilikuwa zile "ice-cream" (malai) ambaozo maji huwekwa kwenye "kijikopo" kidogo kisha kuchomekwa kijiti cha chelewa ambapo maji yakiganda kile kijiti huwa ni sehemu ya kushika ashkrim hiyo.
"Karibu uketi"
Alisema yule mwanamke 'mwarabu' huku akiendelea na kazi yake.
Ndipo nikajuwa kuwa ile sauti nyororo ni ya huyo mama.
"HAMIDAAAA"
Aliita yule mama wa kiarabu.
Mara nikasikia sauti mlango fulani ukifunguliwa na kisha hatua za kivivu zikija upande wetu kutokea koridoni.
Pazia lilisogezwa pembeni akachungulia msichana aliye jitanda ushungi.
"Abee"
Yule binti aliitikia huku akimuangalia yule mama mkoroga malai.
"Hebu kamletee mgeni kinywaji"
Yule binti aliondoka bila kusema neno.
"Mzee Mjumbe nimemkuta?"
Niliuliza hivyo baada ya kuwasalimia kama ilivyo desturi na kujitambulisha.
"Tangia alivyoenda msikitini bado hajarudi, bila shaka atakuwa pale Shibam wanapocheza keram na zuna"
Alijibu yule mama huku ameinama akiendelea na kazi yake.
*************************
Michezo ya Keram, Zuna, Karata, Bao ilikuwa maarufu sana kwenye 'kijiwe' cha kahawa na tangawizi pale Shibam na sehemu nyingine jijini Dar es Salaam. Mambo na mipango mbalimbali ilijadiliwa hapo ikiwemo siasa, michezo nk.
Mara yule binti alirudi huku ameshika magi iliyojaa sharubati na mkono wa kushoto ameshika bilauli ya bati.
Alimimina ile togwa kwenye ile bilauli mbele yangu kisha akanipatia. Ilikuwa togwa ya mtama uliokobolewa na kutengenezwa kwa ustadi mkubwa.
Maeneo ya FAYA (fire brigade) hivi sasa, zamani palikuwa na mti wa muembe mkubwa ambapo palikuwa maarufu sana kwa biashara ya togwa hadi eneo hilo likapewa jina la "mwembe togwa"
Pia haikuwa ajabu kukuta sinia yenye maji iliyowekwa chupa za 'fanta' ndani mkiwa na togwa, imezibwa na kipande cha gazeti iliyokunjwa vema kwenye kila chupa, wengine waliweka chupa moja tu ama stuli iliyofunikwa kawa bila kitu ndani, wateja hutambua moja kwa moja kwamba hapo kuna biashara fulani.
**********************
Niliipokea ile bilauli na kuigigida (kuinywa kwa haraka) kwani nilikuwa nataka niondoke niwahi kupeleka ujumbe sehemu nyingine kwa kuwa hapo tayari niliwaachia moja ya barua nilizokuwa nazo.
Nilikuwa nina karatasi kadhaa (barua) za kuwasambazia wajumbe wa nyumba 'kumi kumi' (waliitwa hivyo) kutoka kwa Katibu Kata, Kata ya Magomeni...
Niliwaaga wale wenyeji mle sebuleni na kuanza kuondoka. Yule binti naye akachukuwa ile bilauli pekee na kuacha magi yenye togwa iliyobakia pale sebuleni...
***********
Wakati navaa viatu pale koridoni, Hamida (siyo jina lake halisi) naye akawa anakuja kutoka uani (siyo maliwatoni) huku ameshika bilauli nne mkononi...
Nikawa namuangalia huku nikiwa nafunga kamba za viatu. Mara ghafla mtandio ukateleza akabaki kichwa wazi...
Moyo ulinilipuka paa! Kwa kumuona Hamida vizuri waziwazi...
Aliinama haraka haraka na kuchukuwa mtandio wake lakini kwa bahati mbaya tena zile bilauli zikamponyoka na kuanguka sakafuni...
=
=
=
****
Hivi ndivyo nilivyokutana na Hamida wangu...
***********
Inaendelea post #5
Mkuu Tayukwa wee hii ushaisoma???? Ngoja niisome nasikia watu wanaizingumzia sana!UHUSIANO WANGU KIMAPENZI NA HAMIDA
Utangulizi.
'Mama watoto' aliridhia mimi kuandika simulizi hii kwa masharti.
Moja ya masharti nijitahidi kutoacha mlango / milango wazi itakayoruhusu watu kuunganisha dots...
Masharti mengine kwa kuwa ni sehemu ya codes, sintoyaeleza.
Hivyo katika simulizi hii nitaongeza 'chumvi' ama 'kuongeza maji' ili kuleta ladha kusudiwa.
Hamida ni mke wangu ambaye "hajaniacha"
=
=
=
Angalizo:
Picha ni kwa hisani ya "google"
Hazina uhusiano na simulizi hii.
Pia kuna sehemu inaweza kuamsha hisia za mapenzi,
Simulizi hii haina uhusiano na Hamida aliye-trend kwenye mitandao ya kijamii hivi karibuni.
Majina yote ya watu katika simulizi hii hayatokuwa halisi isipokuwa machache sana kwa sababu maalum.
SEHEMU YA KWANZA
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
"Hodiii!, hodi hodi humu ndani"
Nilibisha hodi huku nikigonga mlango kwa kutumia kipande cha chuma kilichoning'izwa maalum kwa ajili hiyo.
"Karibu, fungua mlango umeshindikwa tu"
Sauti nyororo ilisikika kutoka ndani.
"Starehe"
Nilijibu huku nikisukuma mlango mzito wa mbao ulionakshiwa kwa ustadi mkubwa. (Neno 'starehe' enzi hizo ndio lilitumika kujibu pindi ubishapo hodi na kukaribishwa)
Nilipofungua mlango nikakutana na korido ndefu nyembamba (wakati huo iliitwa 'ukumbi' japo siyo kama kumbi tuzijuazo leo), pembeni kulia na kushoto kulikuwa milango, wa kushoto ulikuwa mpana ambapo ulikuwa wazi ukiwa umesitiriwa na pazia zuri jepesi lenye 'kuangaza' (transparent) la rangi nyeupe, upande wa kulia mlango ulikuwa umefungwa, na milango mingine mitatu pia ilikuwa imefungwa.
Mbele mwisho wa korido kulikuwa na mlango ambao ulikuwa wazi kiasi cha kuweza kuona nafasi kubwa iliyokuwepo na sehemu ya uzio wenyeji waliita uani (sikuhizi ukisema uani watu watajuwa ni maliwatoni)
************
"Karibu tupo huku varandani"
Ile sauti nyororo iliendelea kunikaribisha na sauti hiyo ilitokea upande ule wa pazia jepesi angavu ambapo nilivyoingia nikatambua kuwa pale palikuwa ndiyo sebuleni.
Kabla ya kuingia nilivua viatu vyangu (raba - Morogoro shoes), havikutoa harufu mbaya kwa kuwa ndiyo nimevivaa kwa mara ya kwanza baada ya kuvinunua, vilikuwa vya rangi ya bluu na soksi zangu nyeupe. Hapo mlangoni kulikuwa na viatu vya sandarusi vyenye ukubwa tofauti pea tatu... nikajuwa utaratibu wa kuingia humo ni pamoja na kuvua viatu.
Nilipekenyua pazia kulia na kushoto na kupiga hatua kuvuka kivingiti cha mlango na kukanyaga zulia zuri la manyoya manyoya.
Ndani niliwakuta wanawake wawili na mtoto mmoja mdogo wa chini ya miaka mitano. Wale wanawake mmoja alikuwa mwafrika, amejitanda vizuri ushungi huku akiwa ameshika ukili (alikuwa anasuka mkeka).
Wote walikuwa wamekaa chini na kuegemea mito midogo, hapakuwa na viti bali meza ndogo iliyo chinichini sana jirani na zulia.
Yule mwanamke wa pili alikuwa mweupe, asili ya Asia, na sikuweza kufahamu maramoja kama alikuwa Mwarabu ama Mhindi. Alikuwa anakoroga maji ya rangirangi akichanganya sukari na yale maji, bila shaka alikuwa anaandaa "ashkrim", watoto walikuwa wanaita hivyo. Zilikuwa zile "ice-cream" (malai) ambaozo maji huwekwa kwenye "kijikopo" kidogo kisha kuchomekwa kijiti cha chelewa ambapo maji yakiganda kile kijiti huwa ni sehemu ya kushika ashkrim hiyo.
"Karibu uketi"
Alisema yule mwanamke 'mwarabu' huku akiendelea na kazi yake.
Ndipo nikajuwa kuwa ile sauti nyororo ni ya huyo mama.
"HAMIDAAAA"
Aliita yule mama wa kiarabu.
Mara nikasikia sauti mlango fulani ukifunguliwa na kisha hatua za kivivu zikija upande wetu kutokea koridoni.
Pazia lilisogezwa pembeni akachungulia msichana aliye jitanda ushungi.
"Abee"
Yule binti aliitikia huku akimuangalia yule mama mkoroga malai.
"Hebu kamletee mgeni kinywaji"
Yule binti aliondoka bila kusema neno.
"Mzee Mjumbe nimemkuta?"
Niliuliza hivyo baada ya kuwasalimia kama ilivyo desturi na kujitambulisha.
"Tangia alivyoenda msikitini bado hajarudi, bila shaka atakuwa pale Shibam wanapocheza keram na zuna"
Alijibu yule mama huku ameinama akiendelea na kazi yake.
*************************
Michezo ya Keram, Zuna, Karata, Bao ilikuwa maarufu sana kwenye 'kijiwe' cha kahawa na tangawizi pale Shibam na sehemu nyingine jijini Dar es Salaam. Mambo na mipango mbalimbali ilijadiliwa hapo ikiwemo siasa, michezo nk.
Mara yule binti alirudi huku ameshika magi iliyojaa sharubati na mkono wa kushoto ameshika bilauli ya bati.
Alimimina ile togwa kwenye ile bilauli mbele yangu kisha akanipatia. Ilikuwa togwa ya mtama uliokobolewa na kutengenezwa kwa ustadi mkubwa.
Maeneo ya FAYA (fire brigade) hivi sasa, zamani palikuwa na mti wa muembe mkubwa ambapo palikuwa maarufu sana kwa biashara ya togwa hadi eneo hilo likapewa jina la "mwembe togwa"
Pia haikuwa ajabu kukuta sinia yenye maji iliyowekwa chupa za 'fanta' ndani mkiwa na togwa, imezibwa na kipande cha gazeti iliyokunjwa vema kwenye kila chupa, wengine waliweka chupa moja tu ama stuli iliyofunikwa kawa bila kitu ndani, wateja hutambua moja kwa moja kwamba hapo kuna biashara fulani.
**********************
Niliipokea ile bilauli na kuigigida (kuinywa kwa haraka) kwani nilikuwa nataka niondoke niwahi kupeleka ujumbe sehemu nyingine kwa kuwa hapo tayari niliwaachia moja ya barua nilizokuwa nazo.
Nilikuwa nina karatasi kadhaa (barua) za kuwasambazia wajumbe wa nyumba 'kumi kumi' (waliitwa hivyo) kutoka kwa Katibu Kata, Kata ya Magomeni...
Niliwaaga wale wenyeji mle sebuleni na kuanza kuondoka. Yule binti naye akachukuwa ile bilauli pekee na kuacha magi yenye togwa iliyobakia pale sebuleni...
***********
Wakati navaa viatu pale koridoni, Hamida (siyo jina lake halisi) naye akawa anakuja kutoka uani (siyo maliwatoni) huku ameshika bilauli nne mkononi...
Nikawa namuangalia huku nikiwa nafunga kamba za viatu. Mara ghafla mtandio ukateleza akabaki kichwa wazi...
Moyo ulinilipuka paa! Kwa kumuona Hamida vizuri waziwazi...
Aliinama haraka haraka na kuchukuwa mtandio wake lakini kwa bahati mbaya tena zile bilauli zikamponyoka na kuanguka sakafuni...
=
=
=
****
Hivi ndivyo nilivyokutana na Hamida wangu...
***********
Inaendelea post #5
Wali mbaazi lol!.... Hamida.....
SEHEMU YA PILI
******************
Kabila langu ni Taturu, baba yangu alibahatika kufanya kazi na Padri fulani mkoa wa Singida, hivyo masikio yangu yalinusurika kutobolewa, mimi pamoja na mdogo wangu niliyemuachia ziwa.
Miezi kadhaa nikiwa nimerudi nchini kutoka masomoni Ulaya, nikiwa mwajiriwa wa RTC maarufu kama UGAWAJI enzi hizo (siyo TRC), nilimtafuta Rose (wa Lindi; stori yake ipo kwenye uzi wa kula tunda kimasihara), Rozi hakujibu barua zangu tangia nilipo kuwa Ulaya. Miaka mitano ilikuwa imeshapita sasa.
=
Rose nilimuacha Lindi na kurudi Dar es Salaam baada ya kuwa naye Lindi kwa uhusiano wa mapenzi motomoto ya miezi miwili. Nikiwa Dar tulikuwa tunawasiliana kama kawaida lakini sikupata bahati ya kuonana naye ana kwa ana hadi leo hii ninapoandika haya.
=
Nilikata tamaa ya kuendelea kumtafuta, kazi yangu nayo ilichangia kwa kuwa nilikuwa bize mno hususani baada ya kurudi masomoni na kupandishwa cheo...
Labda mchumba wake aliendeleza uhusiano wao na kumuoa, hivyo aliamua kukata mawasiliano, hii ndiyo dhana kuu niliyobaki nayo, nahisi mtoto wake wa kwanza ni damu yangu.
************************
James mimi nilikuwa "kiwembe" sana kabla ya kukutana na Rose, umri wa kuoa ulikuwa umeshafika hivyo nilidhani kwake Rose ningehitimisha useja.
Baada ya kukata tamaa niliamua kuendeleza wimbi la 'ubazazi', kutembea na kila binti mrembo niliyemtaka...
Uingereza 'sikutembea' hovyo, nilikuwa na girl friend mmoja tu mwanchuo mwenzangu aliyetokea Hispania, Sue Parterson. Miss Sue ndiye aliyenipatia kitabu "Frech Sex Art Manners" kilichoandikwa na G. Valensin, nilijifunza mengi lakini uhusiano wangu na binti Paterson haukuwa wa malengo ya mbali, hivyo niliachana naye miaka miwili kabla ya kurudi nchini (nilidumu yaye kwa miaka miwili na miezi tisa hivi) ambapo nilienda Kaskazini zaidi kuchukuwa post graduate diploma fulani.
Enzi hizo kabla ya kwenda Ulaya hususani Uingereza, kulikuwa na utaratibu wa kupata semina fupi pale British Council, kwa ajili ya kuwaweka sawa kukabiliana na mazingira ya huko. Nakumbuka pamoja na mambo mengine tulifundishwa kufunga tai(japo nilikuwa najuwa kabla)![]()
Nilivyorudi Tanzania, nikapewa nafasi nzuri katika RTC (Regional Trading Company), nikatumia kufahamika kwangu na umuhimu wangu kujipatia mabinti warembo kila uchao hadi siku hiyo moyo uliponilipuka kwa kumuona Hamida.
*************************************
Makatibu Kata walitusaidia sana katika kazi zetu, nikazoeana na Katibu kata mmoja ambaye alikuwa Kata ya Magomeni.
Kulikuwa na mkutano uliandaliwa kati ya Uongozi wa Kata na wajumbe wa nyumba kumi kumi kuhusiana na hali ya upatikanaji wa bidhaa katika mkoa.
Nchi ilikuwa imetoka vitani, (Tanzania vs Uganda), hali ya uchumi ilikuwa imeyumba hivyo wajumbe walitakiwa kuwaandaa waananchi katika mashina yao kukabiliana na hali inayoanza kujitokeza.
Mzee Katibu Kata rafiki yangu nilipomtembelea afisini kwake, (nyuma ya Hotel Travertine hivi sasa) ndipo akaniomba nimsambazie barua kwa baadhi ya wajumbe Magomeni Mapipa; alikuwa hajisikii vizuri (alikuwa ana homa)
Magomeni Mapipa enzi hizo palikuwa maarufu sana, hapo ndipo kulikuwa na U-turn kubwa kwa ajili ya magari aina ya 'Ikarus' kugeuzia.
Mabasi haya pamoja na mabasi mengine yalikuwa yanamilikiwa na Shirika la UDA (Usafiri Dar es Salaam) ambapo walikuwa na mabasi yaliyotengenezwa na kampuni mbalimbali ikiwemo Mercides Benz (German), Isuzu (Japan), Ikarus (Hungary) nk.
Wanafunzi walikuwa wanapenda sana kupanda Ikarus, na waliyaita "ikarus kumbakumba" maana likija moja lilikuwa linapakia abiria wengi kwa mara moja. Mfano wake ni kama haya mabasi ya Kichina ya BRT yale marefu.
*****************************
Wakati nimechuchumaa nafunga viatu kamba huku nikimuangalia Hamida akiwa ameinama kuokota mtandio wake pamoja na bilauli zile, yule mama mwenye sauti nyororo nikamsikia akisema " Kwema huko?, taratibu mnatushtua na presha hizi..."
"Ziliniponyoka, ngoja nikazisuuze tena nizilete"
Hamida alijibu, nikaisikia sauti yake nyororo akiongea sentesi nzima.
Maa shaa Allah kumbe naye ana sauti kama ya yule mama Mwarabu.
"Kwaheri Hamida"
Nilijikuta nimeropoka huku nikirudi kinyumenyume kuelekea mlango wa kutokea nje. Hamida hakujibu kitu, aliinama na kugeuka akaelekea uani (siyo maliwatoni), mtandio alijifunika kichwani lakini kwa kuutupia tu.
Niligeuka na kuvuta mlango kwa ndani na kutoka nje.
***********
Mzee Burhani ni mjumbe wa nyumba kumi katika mtaa huo nilipotoka, ni mzee kwenye hekima na mcheshi sana, muislamu safi na mwenye kuipenda familia yake na jamii aiongozayo kwa ujumla.
"Salama leko"
Nilisalimia kama waislamu wanavyosalimia, waliitikia lakini mzee mmoja wa makamo akaniambia, wewe James inabidi ujifunze kusalimia vizuri...
Hatusemi salama leko bali tunasema Assalaam aleikum. Pale pale nikarudia
"Assalaam aleikum"
Wakaitikia tena kwa wingi.
"Inabidi usilimu kijana."
Mzee Burhani alidakia.
"Hahhaha" nilicheka, kisha nikamwambia kuwa ule ulikuwa ni 'mguu wake'
Kwakuwa haikuwa siri nilimueleza kuwa nilipitia nyumbani kwake na kuacha barua na kumpa yaliyo ndani kwa ufupi, kisha nami nikajisogeza kwenye benchi nikaketi huku nikiangalia wanavyocheza keram.
_____
SEHEMU YA TATU
*******************
Pale Shibam kwenye 'kijiwe cha kahawa' nilikaa dakika chache tu, 'niliwapiga' raund moja ya tangawizi wale wazee waliokuwepo pale kisha nikaaga na kuondoka kumalizia kusambaza zile barua nilizobakinazo.
Nilinyonga batavus yangu (aina fulani ya motorcycle) na kuwaka nikaendelea mitaa mingine.
Kabla ya machweo nilikuwa nimeshamaliza kazi niliyopewa na 'Mzee Katibu Kata', hivyo nilielekea moja kwa moja nyumbani.
Hapo Dar nilikuwa naishi kwenye nyumba za Shirika la nyumba (NHC) zilizokuwepo Magomeni Mapipa (jirani na Tanesco Magomeni), zilikuwa nyumba bora sana enzi hizo. Miaka mitano nyuma nilikuwa nakaa 'kota' zilizokuwepo jirani na kituo cha afya Magomeni Mapipa (hospitali)
Ilikuwa siku ya Ijumaa, jua limezama nami nipo ndani kwangu nikizinyoosha (kupiga pasi) nguo la kutokea usiku huo pamoja na nguo nyingine...
Ilikuwa ni nadra sana kwa vijana wa kariba yangu ifikapo mwisho wa juma (weekend) kuwepo nyumbani baina ya saa mbili na nusu usiku hadi saa sita usiku (wengine hadi alfajiri)
Nilikuwa mpenzi sana wa muziki wa dansi hususani DDC Mlimani Park Orchestra, hivyo kila jumamosi nilikuwa sikosi pale DDC Kariakoo, Magomeni Kondoa ama Lango la jiji.
Ijumaa hii nilipanga kwenda sinema, (Empire). Zama hizo kumbi za sinema ndiyo zilikuwa kimbilio letu kwa ajili ya kuburudika na filamu mbalimbali.
Starehe za sinema miaka hiyo kwa Dar es Salaam kimbilio la 'wanyonge' lilikuwa pale Oysterbay, Drive-in Cinema, ambapo screen ilikuwa kubwa na imewekwa juu sana kiasi cha kuweza kuonekana na watu wote hata walio nje ya ukumbi, hivyo wasiokuwa na uwezo wa kulipia kuingia (na magari yao), walikaa nje kwenye majani mafupi ama vumbini, wakifuatilia filamu, mbu nao walipata lishe ya kutosha.
Kulikuwa na kituo cha daladala eneo la Drive-in Cinema baadaye makondakta wa madaladala wakawa wanafupisha kuita jina lote na kupaita "drai"
Cameo, Empire, Empress, Avalon na Odeon cinema ni baadhi ya kumbi za sinema zilizokiwa maarufu sana Dar enzi hizo. Ratiba yangu wiki hiyo ilikuwa ijumaa kwenda sinema (Empire), jumamosi DDC kariakoo na jumapili kutulia nyumbani baada ya ibada kwa ajili ya maandalizi ya jumatatu kazini.
****************
Saa mbili kasoro robo (tuliita saa mbili kasorobo) nilikuwa tayari nimemaliza kazi muhimu nikafungulia redio (RTD) kipindi pendwa cha michezo, nakumbuka siku hiyo kilitangazwa na Julius Nyaisanga (R.I.P)
Nilibahatika pamoja na vitu vingine, kurudi na radio cassete (music system) kutoka Ulaya. Kabla ya hapo nilikuwa na radio cassete ya kawaida pamoja na 'player ya santuri' (turntable). Kurudi na music system enzi hizo ilikuwa ni fahari sana...
Saa mbili na robo hivi baada ya kusikiliza taarifa ya habari na mazungumzo baada ya habari, nilikuwa tayari kutoka.
Nilichukuwa pikipiki yangu (batavuz) na kuelekea Butiama Restaurant kupata pilau safi ya moto kabla ya kuelekea mjini maeneo ya posta mpya (mtaa wa maktaba) ukumbi wa Empire kuangalia filamu ya Kihindi iitwayo Kurbaan. (Ile kurbaan ya zamani maana sikuhizi nasikia kuna kurbaan mpya na kurbaaniyan)
Filamu hiyo ilitangazwa kwenye kurasa za magazeti maarufu ya enzi hizo, pamoja na mabandiko (posters) kwenye ubao wa matangazo wa Empire.
Filamu nilizianza kuzipenda tangia nipo shule ya kati (middle school), kuna wamisionari walikuwa wanatuletea filamu ya maigizo ya maisha ya Yesu, na kule kijijini kwetu kuna wakati landrover fulani ilikuja na kutuonesha filamu ya namna ya ukulima bora, sikumbuki hata ilikuwa taasisi gani. Kuna baadhi ya viongozi na watu maarufu nilianza kuwaona kupitia filamu hiyo tuliyoletewa kijijini kwetu.
*************************************
Trela (trailer) ilikuwa imeanza tangia saa mbili, mie nilifika saa tatu kasoro kidogo tu, Saa tatu kamili filamu ingeanza.
Waonesha filamu enzi hizo walitumia projector kubwa sana zenye kutumia 'film' (mkanda kwenye magurudumu) kama kitunzia / chanzo cha picha. Mikwaruzo kwenye sauti na picha na chengachenga zilikuwa ni sehemu ya burudani pia kwani hakukuwa na namna bora zaidi wakati huo.
Nikakata tikiti (tiket / ticket) na kuruhusiwa kuingia ndani. Nikapanda ngazi fasta na kuangaza sehemu iliyokuwa wazi, nikapaona nikaenda kuketi; filamu ikaanza na wote tulianza kufuatilia.
***************************
Katika sinema za Kihindi, pamoja na uzuri wa maudhui, lakini pia nilikuwa napenda nyimbo zao. Lugha ilikuwa inatumika ya Kihindi, japo sehemu chache walichanganya na Kiigereza, hakukuwa na sub-titles za kutusaidia, bali kulikuwa na 'spoilers' ukumbini 'much know' sana na kuanza kuhadithia (uongo ulikuwa mwingi sana), usiombee uwe jirani nao! lakini bado tulikuwa tunafurahia.
Katika filamu hiyo pia kulikuwa na nyimbo nyingi, lakini kuna songi (wimbo) mmoja uliniteka hisia sana.
Natamani niwaimbie hapa lakini nimeusahau, ila nakumbuka 'tone' yake.
Kuna Mwimbaji mmoja maarufu sana wa taarabu (R.I.P) aliuiga kwa kuweka maneno ya Kiswahili, aliuta LEILA
Leila Leila Leila, Ewe wangu Leila, kila mtu hapa, akupenda wewe..
Huo ndio wimbo uliniteka sana kiasi cha kunifanya nimkumbuke Hamida...
Wimbo ulikuwa unaimbwa kwa Kihindi, lakini ulikuwa una hisia sana, nilijikuta nimetumbua macho kuangalia screen lakini mawazo yote ni kwa Hamida..., nitampataje Hamida! Kwa uzuri wake, bila shaka kila mtu anampende Hamida (niliwaza)
=
Kulikuwa na Mapumziko mafupi kwenye filamu hizo (half-time), waoneshaji walikuwa wana rewind mikanda na kuandaa mkanda mwingine kwa ajili ya muendelezo, pia kuwapa nafasi watazamaji kunyoosha miguu na kwenda maliwatoni, kununua viburudisho (bisi zikiwemo ), pia kutoa nafasi ya baadhi ya watazamaji kufuta machozi ama kurudi katika hali zao za kawaida maana filamu zilikuwa zinateka hisia haswa vile vile simema yenyewe ilikuwa ni ndefu (long play), ilitumia dakika 90 kufikia halftime.
Wakati wa halftime, nilimpata dada mmoja na kumshawishi tukae pamoja kwa kuwa siti niliyopata palikuwa na nafasi nne ama tano wazi, ilikuwa siti za katikati nyuma kabisa ambapo juu yake kulikuwa kunapita ule mwanga mkali ya projector.
Alikubali baada ya ushawishi mkubwa, alikuwa yeye na rafiki zake wawili wote wakitokea maeneo ya Upanga. Tukanunua bisi (pop-corn) na chingamu (chewing gum) na kurudi ukumbini.
Kipindi cha pili kiliendelea, na tuliendelea kufurahia filamu hadi mwisho. Ilikuwa saa sita na robo hivi usiku tulipotoka ukumbini.
Niliwalipia taksi (co-cabs) wale rafiki zake, siye kwa kutumia kibatavuzi hao tukawa tunawafuata kwa nyuma kuelekea makutano ya barabara ya maktaba na bibi titi (Ali Hassan Mwinyi Rd. iliitwa hivyo kabla), walikunja kulia kufuata barabara hiyo hadi mbele kidogo ya Redcross na kukunja kushoto...
Wao walisimama nyumba fulani nasi tukapitiliza kuitafuta barabara ya Umoja wa mataifa, tukakunja kushoto ili kuelekea faya ili tuikamate barabara ya Morogoro.
Saa saba na dakika chache tulikuwa tayari tumefika mtaani kwangu. Palikuwa kimya sana, kulikuwa na kile 'kibaridi cha Dar cha usiku', nikafungua mlango, nikaingiza pikipiki na kumkaribisha dada niliyekuja naye.
"karibu sana Egline" (siyo jina lake halisi), nilimkaribisha.
Egline alikuwa mtoto wa mwansheria fulani ambaye wiki hiyo alikuwa safarini Nairobi, hivyo siku hiyo walipata fursa nzuri ya kujivinjari walipotaka bila kikwazo, mama yao hakuwa na "noma". Wale rafiki zake kumbe ni watoto wa mama yao mkubwa, walikuja kumtembelea mama yao mdogo kutokea Same - Kilimanjaro.
Ndani nilikuwa nina vinywaji kwenye jokofu dogo (friji), kulikuwa kuna fanta, double cola, pilsner na brandy (Cognac ya Ufaransa) ambayo ilikuwa kwenye kabati lingine.
*******
Tuliamka saa tatu asubuhi baada ya kengele ya kwenye saa kubwa ya mezani (alarm clock) kulgono kiasi, sikuwa vizuri kutokana na mawazo juu ya Hamida.
Naanzaje kupata Hamida?