Uhusiano wangu na mwanamke wangu kipenzi umeingia doa, muda wowote nitakipoteza nilichokipenda kwa moyo wote

Uhusiano wangu na mwanamke wangu kipenzi umeingia doa, muda wowote nitakipoteza nilichokipenda kwa moyo wote

Habari

Ni kijana 25-27 years

Nina mpenzi Yuko chuo anamalizia mwaka wake wa mwisho.

Ninampenda na yeye alinipenda( kwa Sasa sijui make simuelewi elewi)
mpaka nikapanga akimaliza tu masomo yake nipeleke mahari kwao niishi nae.

Uhusiano wetu umedumu kwa mwaka mmoja Sasa.

Kuna taarifa mbaya nilizipata juu yake kuwa wakati akiwa likizo kwenye mafunzo ya vitendo, aliingia mapenzini na mtu mwingine mpaka akapata ujauzito then akauchomoa.

Chuo kimefunguliwa nikamtembelea nikawa nimepewa taarifa na mtu wake wa karibu kuhusu kilichotokea.

Nilimuuliza ila Cha kushangaza hakuonesha kushtuka kwanza aliniuliza Kama napenda kuambiwa ukweli au kudanganywa Kisha akasema nilichokisikia Ni ukweli na kuwa Yale yalishapita hivyo vyovyote nitakavyomchukulia Ni sawa tu.

Niko njiapanda sielewi nimuache vipi coz nampenda Sana
Na anachokionyesha Ni kuwa Yuko tayali kwa maamuzi yangu yoyote.

Mara ananimbia tuachane kisa amefikiria siwezi kumsamehe kwa alichokifanya.
Nifanyeje?

Asanteni.
Acha utoto kaza kamba ya kiatu na ufate ueleke
 
Mkuu husikii hata aibu kuja hapa kusema manzi kakujibu nanmna hiyo??
"vyovyote utakavyonichukulia ni sawa"
Sasa hapa unataka tukushauri uendelee nae na dalili zote mbovu ushaziona??
 
Sisemi unapaswa kumpenda mtu mkamilifu.
Sisemi hutakosewa.
Sisemi hatakosea.
Ila kuna kitu kinaitwa remorse.
Huyo binti hana hatia moyoni mwake
hajali kukupoteza
hahitaji mapenzi yako
hahitaji maisha na wewe.

Sasa kutoa mimba sio issue ndogo ujue.
Usiendelee na chochote unachotaka kuendelea na huyo mwanamke.
 
Nime note mambo kadhaa.
1. Amekusaliti.
2. Ametoa mimba(muuaji huyo!).
3. Amekudharau sana.
4. Hajakiri kosa.
HITIMISHO..
Hakufai, kuacha au kutokumuacha ni suala jingine.
Pole ndg
 
Kijana mwenzetu,kwanza hako kamwanachuo hakakupendi...pili wewe ndo unaonekana kufosi mapenzi kwake...tatu sku nyingine acha kujifanya kupenda penda mtakuja kufa mapema ..USHAURI WANGU KATA MAWASILIANO NAYE JAPO NI NGUMU ILA NDO UNACHOTAKIWA KUFANYA.
 
Siku moja nimembana aniambie kwanini amefanya vile, maana yangu ilikua nijue chanzo
Jibu alilonipa Ni kuwa hayo yametokea na yamepita Kwanza nishukuru vipi kama ningemkuta nao.
Baada ya hapo akawa ananiambia siwezi kumuacha hata nifanyeje.
Na hii huwa ananiambia sana.

Unajua shida ni moja..Ashakujua kuwa wewe ni dhaifu sanaaaaaa kwake..(HII HALI USIACHE IENDELEE WEWE NI MWANAUME)..so huwezi fanya chochote juu yake kuhusu kumuacha so iko siku utafumania yeye akiwa anagongwa live na atakujibu hivyo hivyo...kaka kuwa mwanaume aiseee achana naye m prove wrong kuwa unaweza kuishi bila yeye(which you can)naongea kwa uchungu sana asee
 
Acha ufala. Mwanamke hapendwi, yeye ndo anatakiwa kukupenda. Ujinga huo wanaume wenzangu wa kuwapenda wanawake uishe. Mwanamke pekee unayetakiwa kumpenda ni mama yalo tu

You are such genius[emoji1491][emoji1487][emoji1487][emoji1487][emoji1487]
 
Habari

Ni kijana 25-27 years

Nina mpenzi Yuko chuo anamalizia mwaka wake wa mwisho.

Ninampenda na yeye alinipenda( kwa Sasa sijui make simuelewi elewi)
mpaka nikapanga akimaliza tu masomo yake nipeleke mahari kwao niishi nae.

Uhusiano wetu umedumu kwa mwaka mmoja Sasa.

Kuna taarifa mbaya nilizipata juu yake kuwa wakati akiwa likizo kwenye mafunzo ya vitendo, aliingia mapenzini na mtu mwingine mpaka akapata ujauzito then akauchomoa.

Chuo kimefunguliwa nikamtembelea nikawa nimepewa taarifa na mtu wake wa karibu kuhusu kilichotokea.

Nilimuuliza ila Cha kushangaza hakuonesha kushtuka kwanza aliniuliza Kama napenda kuambiwa ukweli au kudanganywa Kisha akasema nilichokisikia Ni ukweli na kuwa Yale yalishapita hivyo vyovyote nitakavyomchukulia Ni sawa tu.

Niko njiapanda sielewi nimuache vipi coz nampenda Sana
Na anachokionyesha Ni kuwa Yuko tayali kwa maamuzi yangu yoyote.

Mara ananimbia tuachane kisa amefikiria siwezi kumsamehe kwa alichokifanya.
Nifanyeje?

Asanteni.
Amekuona wewe ni Rais dhaifu
 
Back
Top Bottom