Uhusika wa waliohukumiwa kunyongwa kesi ya Lotter

Uhusika wa waliohukumiwa kunyongwa kesi ya Lotter

econonist

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Posts
20,189
Reaction score
29,663
Watuhumiwa 11 wamehukimwa na Mahakama kuu ya Tanzania kwa kumuua Wayne Lotter.

Ingawa mfadhili kuu wa kesi hii alikuwa Mchina , bado haijajulikana hakukamatwa au alikamatwa akawa deported. Mwingine Fahmi Karama alikamatwa lakini haijulikani yupo wapi, hata kwenye kesi hakuletwa Kama mtuhumiwa:.

Uhusika kwenye mauaji ya Lotter Ni Kama ifuatavyo:

1. Wa kwanza, Ismail Issa Machips yeye ndio alipewa dili na mchina na kutakiwa kutafuta hitman wa kumuua Lotter. Machips na huyo mchina walikutania Arusha. Kwenye kutafuta hitman akamuhusisha Makoi.

2. Wa pili ni Makoi, yeye alimtafuta Hitman baada ya kushirikishwa na Issa Machips. Na Makoi akapendekeza mtu anayeweza hiyo kazi ni Fahmi Karama. Hivyo Hawa wawili ndio chimbuko hasa la dili lote.

3. Wa tatu Rahma Mwinyi, yeye kazi yake ilikuwa kutunza silaha zilizotumika kumuua Lotter. Na silaha hizo alikuwa anaficha makaburini huko Temeke. Pia huyu Rahma aliingizwa kwenye hili dili na kaka yake Fahmi Karama na alikuwa saa zingine anawapikia msosi watuhumiwa wengine waliokuwa wanakuja hapo kwao Temeke.

4. Wa nne Chambiie Juma, huyu alikuwa dereva taxi kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa KIA. Na Marehemu Wayne Lotter alikuwa mteje wake alipokuwa akifika KIA au kuondoka KIA. Yeye ndio alitoa taarifa kwa wauaji kwamba Mr Lotter ameshapanda ndege na anaelekea Dar.

5. Wa tano, Allen Mafue. Huyu ameingia kwenye hi kesi Kama mfadhili wa mauaji. Yeye ndiye aliyewalipa kiasi Cha millioni 20 za kitanzania akina Karama na ongiste. Na aliwalipa hizo fedha kwenye bureau de change yake.

6. Wa sita Ayoub Selemani Kihoi, yeye kazi yake kubwa ilikuwa kuwafuatilia kwa ukaribu Lotter na mwenzake na kuwapa taarifa wauaji. So kazi yake ilikuwa ni kumonitor na kuwafatilia akina Lotter wanapotoka na kwenda siku hiyo ya mauaji. Na kuwapa attention wauaji wawe tayari.

7. Wa Saba ni Abou Omary mchingile, yeye pamoja na Kihoi walikuwa pamoja kumonitor taxi waliyoitumia akina Lotter na kutoa taarifa imefika wapi na inaelekea wapi ili wauaji wawe attention.

8. Wa nane, Michael David Kwavava, huyu ndio alikuwa dereva taxi wa Mr Lotter ndio aliyemtoa JKIA kumpeleka Baobab Village Masaki. Huyu dereva taxi alikuwa na mawasiliano na Fahmi Karama kabla siku ya mauaji hayajatokea. Na Fahmi alikuwa na mazungumzo naye kwa nusu saa kuhusu huo mpango wake.

9. Wa tisa ni Ndui mana ongiste raia wa Burundi. Huyu ndie aliyetekeleza mauaji kwa kumpiga Risasi Marehemu Lotter. Pia dereva taxi kwavara alimtambua kwenye identification parade iliyofanyika polisi, kwamba ndiye aliyefyatua risasi. Pia alikuwa akishirikiana na Fahmi Karama kwenye mipango yote.

10. Wa kumi ni Godfrey Peter Salamba, huyu ndio alikuwa dereva aliyewaendesha wauaji. Ndio alikuwa dereva wa gari lilobeba wauaji.

11. Wa kumi na moja Hibonimana Augustine Nyandwi, raia wa Burundi . Yeye ndiye aliyeleta silaha iliyomuua huyo Lotter na pia aliratibu mambo mengine ya kufanya mauaji hayo.

Kwenye hao wote wenye ahueni ya kukata rufaa ni wawili dereva taxi, maana mwanzoni kwenye kesi alikuwa Kama shahidi wa Jamhuri ila baadae ikagundulika naye alikuwa na mawasiliano na Karama. Na waliomtaja ni watuhumiwa wengine. Anaweza kubisha kwamba watuhumiwa walimtaja Kama kumkomoa baada ya kusema alimuona ongiste akimpiga risasi Lotter.

Mwingine ni Erick Mafue amabaye bureau de change yake ilitumika kufanya malipo kwa watuhumiwa. Je alitumiwa tu pesa za kigeni abadilishe au pesa zilikuwa za kwake za kufadhili mauaji hayo. Na je alijuwa fedha hizo zitatumika kwenye mauaji?. Wengine kwenye kuchomoka kwenye rufaa ni kazi.
 
Issue kubwa sana hii na ni kutokana na wakubwa wa huko duniani kuifuatilia ndiyo maana leo tunaona hukumu, japo imechukua muda.

Huyu jamaa kauawa kupitia samaki wadogo ila nyangumi wapo kwenye kina kirefu, that's why kuna wakati hii kesi ilipata majibu hukumu itoke ila ikapasishwa ila leo dagaa wanakula mvua na wengine kuaga dunia.

Lotter alikuwa anaharibu ma_deal ya wanene kuna mmoja yupo mitandaoni na ana kelele sana huko anaweza kuwa mmojawapo!.
 
Kuna wakaskazini hapa wafanya biashara pale Arusha, lakini mtasikia tu wakaskazini wanajua kubana budget mpaka wanapata pesa, waaapi..... Kuna mtu anajua kubana pesa kama Muhindi na Muha wa Kigoma? Watu ni majambazi, yaani kundi lote hili kumuua mtu mmoja tu tena siyo Raia kwa faida za ujambazi wao!!! Dunia hii
 
Sijawahi kuifuatilia hii kesi ila kwa hukumu iliyotoka kuna mchezo umefanyika kufunika kombe.

Inaonyesha kuna wahusika wakubwa sana nyuma ya pazia ambao hawajatajwa.

Maana imeanzia tu mtu amepewa deal ya kuua na ndio mnyororo wa wahusika umeanzia hapo. Hao vijana siju wazee ni kweli wanehusika kuua ila je wametumwa na nani? Kwa nini aliyewatuma ambaye ndio chanzo cha mauaji hajausishwa. Nawaza tu kwa kina ila sina interest yoyote na hayo mambo
 
Sijawahi kuifuatilia hii kesi ila kwa hukumu iliyotoka kuna mchezo umefanyika kufunika kombe.

Inaonyesha kuna wahusika wakubwa sana nyuma ya pazia ambao hawajatajwa.

Maana imeanzia tu mtu amepewa deal ya kuua na ndio mnyororo wa wahusika umeanzia hapo. Hao vijana siju wazee ni kweli wanehusika kuua ila je wametumwa na nani? Kwa nini aliyewatuma ambaye ndio chanzo cha mauaji hajausishwa. Nawaza tu kwa kina ila sina interest yoyote na hayo mambo
Jana nilikua Arusha, na nikasikia watu kwenye kahawa wanaongea wanasonta kiduka fulani wakisema mmoja wapo ni mwenye hilo duka, kwamba huyo mzungu aliye uawa alikua anaendesha project inayozuia ujangili wa wanyama na hasa Tembo wasiuawe, kama ndivyo hapo ndo tujiongeze kwamba Kuna nani
 
Back
Top Bottom