Uhusika wa waliohukumiwa kunyongwa kesi ya Lotter

Uhusika wa waliohukumiwa kunyongwa kesi ya Lotter

Watuhumiwa 11 wamehukimwa na Mahakama kuu ya Tanzania kwa kumuua Wayne Lotter.

Ingawa mfadhili kuu wa kesi hii alikuwa Mchina , bado haijajulikana hakukamatwa au alikamatwa akawa deported. Mwingine Fahmi Karama alikamatwa lakini haijulikani yupo wapi, hata kwenye kesi hakuletwa Kama mtuhumiwa:.

Uhusika kwenye mauaji ya Lotter Ni Kama ifuatavyo:

1. Wa kwanza, Ismail Issa Machips yeye ndio alipewa dili na mchina na kutakiwa kutafuta hitman wa kumuua Lotter. Machips na huyo mchina walikutania Arusha. Kwenye kutafuta hitman akamuhusisha Makoi.

2. Wa pili ni Makoi, yeye alimtafuta Hitman baada ya kushirikishwa na Issa Machips. Na Makoi akapendekeza mtu anayeweza hiyo kazi ni Fahmi Karama. Hivyo Hawa wawili ndio chimbuko hasa la dili lote.

3. Wa tatu Rahma Mwinyi, yeye kazi yake ilikuwa kutunza silaha zilizotumika kumuua Lotter. Na silaha hizo alikuwa anaficha makaburini huko Temeke. Pia huyu Rahma aliingizwa kwenye hili dili na kaka yake Fahmi Karama na alikuwa saa zingine anawapikia msosi watuhumiwa wengine waliokuwa wanakuja hapo kwao Temeke.

4. Wa nne Chambiie Juma, huyu alikuwa dereva taxi kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa KIA. Na Marehemu Wayne Lotter alikuwa mteje wake alipokuwa akifika KIA au kuondoka KIA. Yeye ndio alitoa taarifa kwa wauaji kwamba Mr Lotter ameshapanda ndege na anaelekea Dar.

5. Wa tano, Allen Mafue. Huyu ameingia kwenye hi kesi Kama mfadhili wa mauaji. Yeye ndiye aliyewalipa kiasi Cha millioni 20 za kitanzania akina Karama na ongiste. Na aliwalipa hizo fedha kwenye bureau de change yake.

6. Wa sita Ayoub Selemani Kihoi, yeye kazi yake kubwa ilikuwa kuwafuatilia kwa ukaribu Lotter na mwenzake na kuwapa taarifa wauaji. So kazi yake ilikuwa ni kumonitor na kuwafatilia akina Lotter wanapotoka na kwenda siku hiyo ya mauaji. Na kuwapa attention wauaji wawe tayari.

7. Wa Saba ni Abou Omary mchingile, yeye pamoja na Kihoi walikuwa pamoja kumonitor taxi waliyoitumia akina Lotter na kutoa taarifa imefika wapi na inaelekea wapi ili wauaji wawe attention.

8. Wa nane, Michael David Kwavava, huyu ndio alikuwa dereva taxi wa Mr Lotter ndio aliyemtoa JKIA kumpeleka Baobab Village Masaki. Huyu dereva taxi alikuwa na mawasiliano na Fahmi Karama kabla siku ya mauaji hayajatokea. Na Fahmi alikuwa na mazungumzo naye kwa nusu saa kuhusu huo mpango wake.

9. Wa tisa ni Ndui mana ongiste raia wa Burundi. Huyu ndie aliyetekeleza mauaji kwa kumpiga Risasi Marehemu Lotter. Pia dereva taxi kwavara alimtambua kwenye identification parade iliyofanyika polisi, kwamba ndiye aliyefyatua risasi. Pia alikuwa akishirikiana na Fahmi Karama kwenye mipango yote.

10. Wa kumi ni Godfrey Peter Salamba, huyu ndio alikuwa dereva aliyewaendesha wauaji. Ndio alikuwa dereva wa gari lilobeba wauaji.

11. Wa kumi na moja Hibonimana Augustine Nyandwi, raia wa Burundi . Yeye ndiye aliyeleta silaha iliyomuua huyo Lotter na pia aliratibu mambo mengine ya kufanya mauaji hayo.

Kwenye hao wote wenye ahueni ya kukata rufaa ni wawili dereva taxi, maana mwanzoni kwenye kesi alikuwa Kama shahidi wa Jamhuri ila baadae ikagundulika naye alikuwa na mawasiliano na Karama. Na waliomtaja ni watuhumiwa wengine. Anaweza kubisha kwamba watuhumiwa walimtaja Kama kumkomoa baada ya kusema alimuona ongiste akimpiga risasi Lotter.

Mwingine ni Erick Mafue amabaye bureau de change yake ilitumika kufanya malipo kwa watuhumiwa. Je alitumiwa tu pesa za kigeni abadilishe au pesa zilikuwa za kwake za kufadhili mauaji hayo. Na je alijuwa fedha hizo zitatumika kwenye mauaji?. Wengine kwenye kuchomoka kwenye rufaa ni kazi.
Mbona wengi kwenye iyo listi ya wauaji ni wa upande ule wa pili wanapenda kumuimbia na kumpigia kelele mungu wao kwa kiarabu?

Accumen Mo battawi Nahonyo Mlolongo Covax Kikwajuni One mjingamimi
 
Namba 4 pia akipata wakili mzuri anaweza kuchomoka, ni suala la kucheza na maneno tu hapo... anaweza kuwa aliombwa taarifa bila kujua za nini au zinakwenda wapi.. anapaswa kuwakataa wote hawajui isipokuwa marehemu...
Agharamike na amtafute kibatala
 
Jana nilikua Arusha, na nikasikia watu kwenye kahawa wanaongea wanasonta kiduka fulani wakisema mmoja wapo ni mwenye hilo duka, kwamba huyo mzungu aliye uawa alikua anaendesha project inayozuia ujangili wa wanyama na hasa Tembo wasiuawe, kama ndivyo hapo ndo tujiongeze kwamba Kuna nani
Unamaanisha K from Mogadishu?
 
Mchongo wowote haramu
ukishahusisha watu Zaid ya watano in action ni hatar Sana kuvuja.

Kuna watu mafriji yao hayagandishi.

Hivi are you serious kabisa
unamhusisha mama ntilie akusaidie kuficha silaha?
 
We jamaa utakuwa mchaga 90% nyie ndo mna ushamba wa kibaguzi kweny dini na ukabili ..sasa endelea utakuja jikondesha kwa kutokujiamini.
Ni siku nyingi nimeona propaganda zako za kujipiga ''mental masterbation'' kwa wachaga. It seems you are not getting any relieve dear. Why dont you try another method? Huoni hali yako inazidi kuwa mbaya siku hadi siku?
 
Ni siku nyingi nimeona propaganda zako za kujipiga ''mental masterbation'' kwa wachaga. It seems you are not getting any relieve dear. Why dont you try another method? Huoni hali yako inazidi kuwa mbaya siku hadi siku?
Lazima ufuatilie angalia jamaa yako mra ngapi ananitag ...sikia usipende shobo au nikuonyesha kwa kiasi gani anaitag kweny mijadala yenu...sina ushamba wala siwatambui.

Kaa pembeni sipendi shobo na kingereza cha ugoko..pita kushoto !!
 
Namba 4 pia akipata wakili mzuri anaweza kuchomoka, ni suala la kucheza na maneno tu hapo... anaweza kuwa aliombwa taarifa bila kujua za nini au zinakwenda wapi.. anapaswa kuwakataa wote hawajui isipokuwa marehemu...
Kumbuka alishaandika maelezo ya ONYO
 
Huyo dada aliekuwa anawapikia nae anatakiwa kupata msaada atoke,inawezekana alikuwa anapika kutokana na maelezo ya kaka ake

Hii inshu ina wakubwa wengi sana ndo maana hata imehusisha watu wengi hivyo
Kuficha silaha je?

Hujui keshakiri kwenye maelezo?

Hapo labda atoke kwa makosa ya mawakili wa serikali, tofauti na hapo hatoki
 
Ujambazi unatenda.nazungumzia kesi ambazo unaweza kuingia kwa bahati mbaya.kama hao wengine.kaua mmoja lakini adhabu ni moja.au unaunganishwa tu kwenye kesi ya ubakaji na hauusiki
Mkuu, kwenye Sheria Kuna kitu kinaitwa Kula njama.

Hata Kama muuaji alikuwa mmoja Ila Kuna kundi la watu ambalo liliandaa mchango wa kufanikisha mauaji. Sasa watu hawa ingawa hajaua physically Ila mchango wao kwa namna flani umechangia kufanikisha mauaji.

Nao wanastahili kufungwa Ila sidhani Ka ni sahihi wao kuhukumiwa kifo.

Mfano uyo dada Rahma inaweza kuwa hakufahamu Kama ushiriki wake ni kwenye ishu ya mauaji. Akijitetea vizuri na akapata wakili mzuri anaweza kutoka. Sababu kuwaandalia chakula wauwaji sio mpaka awafahamu anaweza akawa ameambiwa na Kaka yake Kuna wageni ni jamaa zangu wanakuja so andaa chakula ili wapate cha Kula.

Na kuhusu silaha alizoficha makaburini inaweza kuwa alipewa Tu na Kaka yake akamwambia fanya uzihifadhi hizi silaha Ila usiweke maeneo ya nyumbani. Japo anaweza kuhisi hizo silaha haziwezi kutumika Kwa Nia nzuri, Ila sio sababu ya yeye kuambiwa ameshiriki njama za mauaji moja kwa moja.
 
Back
Top Bottom