Uhusika wa waliohukumiwa kunyongwa kesi ya Lotter

Uhusika wa waliohukumiwa kunyongwa kesi ya Lotter

Issue kubwa sana hii na ni kutokana na wakubwa wa huko duniani kuifuatilia ndiyo maana leo tunaona hukumu, japo imechukua muda.

Huyu jamaa kauawa kupitia samaki wadogo ila nyangumi wapo kwenye kina kirefu, that's why kuna wakati hii kesi ilipata majibu hukumu itoke ila ikapasishwa ila leo dagaa wanakula mvua na wengine kuaga dunia.

Lotter alikuwa anaharibu ma_deal ya wanene kuna mmoja yupo mitandaoni na ana kelele sana huko anaweza kuwa mmojawapo!.
Genge la mamafia wa rasilimali za pori akina kinana na majangili wengine ndani ya ccm ,trust me ,hao ndio master planners WA hayo mauaji
 
Kazi ya uana harakati wa mazingira na haki za binadamu ni risky business but worth doing ,dah ,huyo mzungu alikuwa mwiba hasa kwa hao mamafia wa rasilimali za pori ,ameokoa tembo na faru wengi sana kutokana na harakati zake
 
Pamoja na hukumu bado wahusika wakuu hawajapatikana.Kama kweli serikali inataka kujua hii chain, wasiwanyonge wakikaa gerezani kwa muda hawa watasema A to Z kwakuwa watajutia na kumrudia Mungu wao na watafunguka mpaka serikali ishangae unless wataka kufunika kombe kuwaokoa vigogo.
Wapelekwe gereji mbona watasema tu waliowatuma ? , Au zile gereji za torture zipo kwa ajili ya kuwashughulikia Chadema tu ?
 
Watuhumiwa 11 wamehukimwa na Mahakama kuu ya Tanzania kwa kumuua Wayne Lotter.

Ingawa mfadhili kuu wa kesi hii alikuwa Mchina , bado haijajulikana hakukamatwa au alikamatwa akawa deported. Mwingine Fahmi Karama alikamatwa lakini haijulikani yupo wapi, hata kwenye kesi hakuletwa Kama mtuhumiwa:.

Uhusika kwenye mauaji ya Lotter Ni Kama ifuatavyo:

1. Wa kwanza, Ismail Issa Machips yeye ndio alipewa dili na mchina na kutakiwa kutafuta hitman wa kumuua Lotter. Machips na huyo mchina walikutania Arusha. Kwenye kutafuta hitman akamuhusisha Makoi.

2. Wa pili ni Makoi, yeye alimtafuta Hitman baada ya kushirikishwa na Issa Machips. Na Makoi akapendekeza mtu anayeweza hiyo kazi ni Fahmi Karama. Hivyo Hawa wawili ndio chimbuko hasa la dili lote.

3. Wa tatu Rahma Mwinyi, yeye kazi yake ilikuwa kutunza silaha zilizotumika kumuua Lotter. Na silaha hizo alikuwa anaficha makaburini huko Temeke. Pia huyu Rahma aliingizwa kwenye hili dili na kaka yake Fahmi Karama na alikuwa saa zingine anawapikia msosi watuhumiwa wengine waliokuwa wanakuja hapo kwao Temeke.

4. Wa nne Chambiie Juma, huyu alikuwa dereva taxi kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa KIA. Na Marehemu Wayne Lotter alikuwa mteje wake alipokuwa akifika KIA au kuondoka KIA. Yeye ndio alitoa taarifa kwa wauaji kwamba Mr Lotter ameshapanda ndege na anaelekea Dar.

5. Wa tano, Allen Mafue. Huyu ameingia kwenye hi kesi Kama mfadhili wa mauaji. Yeye ndiye aliyewalipa kiasi Cha millioni 20 za kitanzania akina Karama na ongiste. Na aliwalipa hizo fedha kwenye bureau de change yake.

6. Wa sita Ayoub Selemani Kihoi, yeye kazi yake kubwa ilikuwa kuwafuatilia kwa ukaribu Lotter na mwenzake na kuwapa taarifa wauaji. So kazi yake ilikuwa ni kumonitor na kuwafatilia akina Lotter wanapotoka na kwenda siku hiyo ya mauaji. Na kuwapa attention wauaji wawe tayari.

7. Wa Saba ni Abou Omary mchingile, yeye pamoja na Kihoi walikuwa pamoja kumonitor taxi waliyoitumia akina Lotter na kutoa taarifa imefika wapi na inaelekea wapi ili wauaji wawe attention.

8. Wa nane, Michael David Kwavava, huyu ndio alikuwa dereva taxi wa Mr Lotter ndio aliyemtoa JKIA kumpeleka Baobab Village Masaki. Huyu dereva taxi alikuwa na mawasiliano na Fahmi Karama kabla siku ya mauaji hayajatokea. Na Fahmi alikuwa na mazungumzo naye kwa nusu saa kuhusu huo mpango wake.

9. Wa tisa ni Ndui mana ongiste raia wa Burundi. Huyu ndie aliyetekeleza mauaji kwa kumpiga Risasi Marehemu Lotter. Pia dereva taxi kwavara alimtambua kwenye identification parade iliyofanyika polisi, kwamba ndiye aliyefyatua risasi. Pia alikuwa akishirikiana na Fahmi Karama kwenye mipango yote.

10. Wa kumi ni Godfrey Peter Salamba, huyu ndio alikuwa dereva aliyewaendesha wauaji. Ndio alikuwa dereva wa gari lilobeba wauaji.

11. Wa kumi na moja Hibonimana Augustine Nyandwi, raia wa Burundi . Yeye ndiye aliyeleta silaha iliyomuua huyo Lotter na pia aliratibu mambo mengine ya kufanya mauaji hayo.

Kwenye hao wote wenye ahueni ya kukata rufaa ni wawili dereva taxi, maana mwanzoni kwenye kesi alikuwa Kama shahidi wa Jamhuri ila baadae ikagundulika naye alikuwa na mawasiliano na Karama. Na waliomtaja ni watuhumiwa wengine. Anaweza kubisha kwamba watuhumiwa walimtaja Kama kumkomoa baada ya kusema alimuona ongiste akimpiga risasi Lotter.

Mwingine ni Erick Mafue amabaye bureau de change yake ilitumika kufanya malipo kwa watuhumiwa. Je alitumiwa tu pesa za kigeni abadilishe au pesa zilikuwa za kwake za kufadhili mauaji hayo. Na je alijuwa fedha hizo zitatumika kwenye mauaji?. Wengine kwenye kuchomoka kwenye rufaa ni kazi.
mkuu mbona kama unafahamu hili sekeseke vizuri. au kuna wakubwa unajaribu kuwakingia kifua?
20221203_154236.jpg
 
Issue zenye chain links zinazohusisha vigogo huwa zinafyeka wanyonge wengi sana ili ku clear any possible tracks,humo wengine hupewa adhabu ya kifo kwa kuwa tu wanamjua mhusika flani papa, huko Mexico wanaharakati wa mazingira wanauawa kila kukicha,mbaya zaidi wanaohusika na mambo hayo wengi ni viongozi wa serikali wanaoshirikiana na majangili wanaopora Maliasili hasa magogo na kuyauza kwa faida kubwa kwenye viwanda via ndani na nje ya Mexico,sasa hata hapa naona kama hiyo michezo inapiga hodi,kuna na helicopter ilishushwa huko mikumi miaka kadhaa nyuma,God forbid
Hii dunia sometyme inabidi uwe mjinga ili uishi kwa amani. Just assume mtu anayejifanya ndo msimamizi wa maliasili/mali kumbe yeye ndo jambazi kuu. Na ukijaribu kuongea tu unawekwa kwny kiroba.

Mfano hyo issue ya mexico, hapa bongo kuna issue kibao kama hzo, na ukijaribu kuongea, mafionzo watakupa kila aina ya kesi mpaka upauke. Refer:erick kabendera, mwangosi, dokta ulimboka, ben saanane.
 
Kila siku hua nasema wahalifu wa Tanzania ni wapumbavu na hawana akili hauwezi kuset crime kishamba namna hiyo usikamatwe, halafu mauaji unapangia kwenye simu? Halafu mauaji mnapanga kijiji kizima watu zaidi ya 20 mnapanga mauaji utarajie utachomoka? Wahalifu smart hawawezi kukuachia Alama kizembe, hua hawaoni hata kagame anavowafanya wasaliti wake?
 
Napata Picha kwamba mzungu kutoka mashariki ya mbali amekuja bongo na kuitetea hili taifa dhaifu,wahusika wenyewe ambao ni dhaifu wana andaa mchongo wa kumuua ili aache kulitetea taifa dhaifu...mnataka mungu atupe kitu gani ss watanzania??? [emoji850][emoji850][emoji850],

Hii ni aibu sana tena sana usikute ni viongozi wachache tu hapo juu ambao umri wao upo karibuni kuwatupa mkono.
 
Muhimu ni kujiepusha na makundi ya wanaopenda fedha kwa njia haramu na kwa haraka. Bahati mbaya baadhi ya watu kwa miaka hii wamekuwa '' money mongers'' wakupitiliza.
 
Hivi unadhani bado yupo huko gerezani? Sijui lakini hebu jaribu kuulizia yuko wapi kama utaambiwa.

Unakumbuka yale makubaliano baina ya rais wa China na Tanzania hivi karibuni wakati tulipopewa mkopo?
Malikia wa pembe za Ndovu kwa taarifa za Chini chini alishaachiwa yuko jiji la Hong kong Uchina kwao.
 
Halafu kila mmoja atatoka kwa urefu wa pesa yake...
hawa watakuja kutoka tu nadhani kuna watu walishindwa kuweka mambo sawa kati ya wale 22 ambao dpp 11 aliwafutia mashtaka.

wengine hapo sio wahusika Mtu Kama Machpis ni mishen Town ati leo anakuwa mtuhumiwa namba moja kesi ya Mauaj tena mzungui!!!!! kuna kitu Behind scene. hii misheni ni kubwa sana.

nilishtushwa zaidi magazeti yote front page kuandika kwa Maandishi makubwa "11 kunyongwa hukumu ya historia"
 
Pamoja na hukumu bado wahusika wakuu hawajapatikana.Kama kweli serikali inataka kujua hii chain, wasiwanyonge wakikaa gerezani kwa muda hawa watasema A to Z kwakuwa watajutia na kumrudia Mungu wao na watafunguka mpaka serikali ishangae unless wataka kufunika kombe kuwaokoa vigogo.
hakuna anae nyongwa hapo. usihadaike.
 
Back
Top Bottom