Uhusika wa waliohukumiwa kunyongwa kesi ya Lotter

Uhusika wa waliohukumiwa kunyongwa kesi ya Lotter

Lotter alikuwa ni one man army, mwanaharakati huru wa masuala ya meno ya tembo.

Kwa ufanisi wake wa kazi, anaogopwa na majambazi kuliko Usalama wa Taifa, Jeshi la TANAPA, Ikulu ya Magufuli, Jeshi la Polisi, Waziri Mkuu, Mkuu wa Mkoa, Uhamiaji mipakani, TRA Airport, na Usalama Bandarini...

Kifupi, Mzungu huyu alikuwa anapinga machafu chafu ya nchi hii na anaumia na hali mbayai ya nchi hii na yuko effective kuliko Rais wa nchi na raia wake milioni 60.
Alikuwa ni mtu na nusu
 
Jamaa alikua anapenda kukaa pale Picnic
Akiwakuta anazungusha lakini hamtajua kaondoka muda gani.Yaani ni mwizi balaa.

Maisha mengi kakulia yale maghorofa ya police machafu machafu pale fire 🔥 opposite Arusha Day Secondary wakati huo Arusha School.

Baada ya Baba yake kufariki akahamia Kaloleni kwa Sister wake mtata mtata ambaye alishughulika sana kumtoa magereza katika kesi nyingine ya mauaji huko kanda ya Ziwa.Godfrey maisha yake mengi between 27 to 40s kayaishi magereza.
 
Machips & Makoi hii ni mara ya kwanza kuionja magereza wala hawana history ya ujambazi nadhani this time waliingia vibaya.
inaonekana hawana criminal case history. hawa hawawezi kuwa master planner wa hii issue ya mission ya mauaji. labda tu sababu ya ukaaji wao mjini mda mrefu wanajua tu ishu za ujangili kama na wengine wanavyofahamu. hawa watakuwa wamechomekwa kwa nguvu. machipsi sio kwamba hata ni tajiri au ni msoma ramani hapana anaishi kwenye nyumba za urithi kaloleni iliko familia yao. huyo Makoi nae muda mwingi anashinda kwa pharmacy yake. hawa hawawezi hata kusuka mpango wa kuua mende.
 
Kuna habari zinazunguka Mitaani kuwa Machips alibambikiwa.
eti machips anapokea deal kutoka kwa mchina!! from nowhere tuu haraka anamtafuta mtu anae itwa makoi ambaye polisi hana record hata ya kuua mnyama! kisha wanagiza silaha nje ya nchi ya kumuua raia wa kigeni ambaye fika wanajua Wakimuua Dunia itapiga kelele wizara ya mali asili haitafunga macho hata wauaji wamepatikana.
 
eti machips anapokea deal kutoka kwa mchina!! from nowhere tuu haraka anamtafuta mtu anae itwa makoi ambaye polisi hana record hata ya kuua mnyama! kisha wanagiza silaha nje ya nchi ya kumuua raia wa kigeni ambaye fika wanajua Wakimuua Dunia itapiga kelele wizara ya mali asili haitafunga macho hata wauaji wamepatikana.
Hata ile kesi ya Ugaidi ya Mbowe ilipangwa na huenda Kamanda angenyongwa hivivi Justuce Sytem ya Nchi yetu inawategemea watu wasiojua PGO na kazi wanarahisisha kwa Kubambikiwa tu au utoe Mpunga mrefu.
 
Namfahamu Makoi,asili yake Kibosho akimiliki maduka kadhaa ya madawa (Pharmacy) ingawa hata kidato cha pili hakumaliza.

Kupitia biashara zake za madawa alijikuta akipanda haraka haraka kibiashara kumbe nyuma ya pazia alikuwa na biashara nyingine.
"Making a million legally has always been difficult. Making a million illegally has always been a little easier. Keeping a million when you have made it is perhaps the most difficult of all. Henryk Metelski was one of those rare men who managed all three. Even if the million he had made legally came after the million he had made illegally, what put him a yard ahead of the others was that he managed to keep it all."

—Not a Penny more, not a Penny less. Jeffrey Archer.
 
inaonekana hawana criminal case history. hawa hawawezi kuwa master planner wa hii issue ya mission ya mauaji. labda tu sababu ya ukaaji wao mjini mda mrefu wanajua tu ishu za ujangili kama na wengine wanavyofahamu. hawa watakuwa wamechomekwa kwa nguvu. machipsi sio kwamba hata ni tajiri au ni msoma ramani hapana anaishi kwenye nyumba za urithi kaloleni iliko familia yao. huyo Makoi nae muda mwingi anashinda kwa pharmacy yake. hawa hawawezi hata kusuka mpango wa kuua mende.
Hiyo nyumba ya urithi wala si yake ni mali ya watoto wa Dada yake wa UK muda sana wanasumbuana na watoto wa Dada yake sijui wamefikishana wapi.

Kuhusu kuhusika huwezi kujua A to Z za mchongo mzima lakini unapswa kujua watu wanatafuta fedha kwa njia mbali mbali bahati mbaya Machips hadi anapata huu msala alikuwa bado katika harakati za kutafuta hela.

Kinachinishangaza ni connection yake na Godfrey Salamba ambaye pasipo shaka ni jambazi sugu.

Mshangao mwingine ni connection ya Makoi sijui kaingia vipi ingawa biashara yake iliupigs mwingi katika muda mchache.
 
Mchongo wowote haramu
ukishahusisha watu Zaid ya watano in action ni hatar Sana kuvuja.

Kuna watu mafriji yao hayagandishi.

Hivi are you serious kabisa
unamhusisha mama ntilie akusaidie kuficha silaha?
Hilo nalo neno.
Lakini kumbuka mkuu, siri ni yako tu, ikiingia mtu wa pili siyo siri tena, siyo kuvujisha lazima wafike wa5!
 
Watuhumiwa 11 wamehukimwa na Mahakama kuu ya Tanzania kwa kumuua Wayne Lotter.

Ingawa mfadhili kuu wa kesi hii alikuwa Mchina , bado haijajulikana hakukamatwa au alikamatwa akawa deported. Mwingine Fahmi Karama alikamatwa lakini haijulikani yupo wapi, hata kwenye kesi hakuletwa Kama mtuhumiwa:.

Uhusika kwenye mauaji ya Lotter Ni Kama ifuatavyo:

1. Wa kwanza, Ismail Issa Machips yeye ndio alipewa dili na mchina na kutakiwa kutafuta hitman wa kumuua Lotter. Machips na huyo mchina walikutania Arusha. Kwenye kutafuta hitman akamuhusisha Makoi.

2. Wa pili ni Makoi, yeye alimtafuta Hitman baada ya kushirikishwa na Issa Machips. Na Makoi akapendekeza mtu anayeweza hiyo kazi ni Fahmi Karama. Hivyo Hawa wawili ndio chimbuko hasa la dili lote.

3. Wa tatu Rahma Mwinyi, yeye kazi yake ilikuwa kutunza silaha zilizotumika kumuua Lotter. Na silaha hizo alikuwa anaficha makaburini huko Temeke. Pia huyu Rahma aliingizwa kwenye hili dili na kaka yake Fahmi Karama na alikuwa saa zingine anawapikia msosi watuhumiwa wengine waliokuwa wanakuja hapo kwao Temeke.

4. Wa nne Chambiie Juma, huyu alikuwa dereva taxi kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa KIA. Na Marehemu Wayne Lotter alikuwa mteje wake alipokuwa akifika KIA au kuondoka KIA. Yeye ndio alitoa taarifa kwa wauaji kwamba Mr Lotter ameshapanda ndege na anaelekea Dar.

5. Wa tano, Allen Mafue. Huyu ameingia kwenye hi kesi Kama mfadhili wa mauaji. Yeye ndiye aliyewalipa kiasi Cha millioni 20 za kitanzania akina Karama na ongiste. Na aliwalipa hizo fedha kwenye bureau de change yake.

6. Wa sita Ayoub Selemani Kihoi, yeye kazi yake kubwa ilikuwa kuwafuatilia kwa ukaribu Lotter na mwenzake na kuwapa taarifa wauaji. So kazi yake ilikuwa ni kumonitor na kuwafatilia akina Lotter wanapotoka na kwenda siku hiyo ya mauaji. Na kuwapa attention wauaji wawe tayari.

7. Wa Saba ni Abou Omary mchingile, yeye pamoja na Kihoi walikuwa pamoja kumonitor taxi waliyoitumia akina Lotter na kutoa taarifa imefika wapi na inaelekea wapi ili wauaji wawe attention.

8. Wa nane, Michael David Kwavava, huyu ndio alikuwa dereva taxi wa Mr Lotter ndio aliyemtoa JKIA kumpeleka Baobab Village Masaki. Huyu dereva taxi alikuwa na mawasiliano na Fahmi Karama kabla siku ya mauaji hayajatokea. Na Fahmi alikuwa na mazungumzo naye kwa nusu saa kuhusu huo mpango wake.

9. Wa tisa ni Ndui mana ongiste raia wa Burundi. Huyu ndie aliyetekeleza mauaji kwa kumpiga Risasi Marehemu Lotter. Pia dereva taxi kwavara alimtambua kwenye identification parade iliyofanyika polisi, kwamba ndiye aliyefyatua risasi. Pia alikuwa akishirikiana na Fahmi Karama kwenye mipango yote.

10. Wa kumi ni Godfrey Peter Salamba, huyu ndio alikuwa dereva aliyewaendesha wauaji. Ndio alikuwa dereva wa gari lilobeba wauaji.

11. Wa kumi na moja Hibonimana Augustine Nyandwi, raia wa Burundi . Yeye ndiye aliyeleta silaha iliyomuua huyo Lotter na pia aliratibu mambo mengine ya kufanya mauaji hayo.

Kwenye hao wote wenye ahueni ya kukata rufaa ni wawili dereva taxi, maana mwanzoni kwenye kesi alikuwa Kama shahidi wa Jamhuri ila baadae ikagundulika naye alikuwa na mawasiliano na Karama. Na waliomtaja ni watuhumiwa wengine. Anaweza kubisha kwamba watuhumiwa walimtaja Kama kumkomoa baada ya kusema alimuona ongiste akimpiga risasi Lotter.

Mwingine ni Erick Mafue amabaye bureau de change yake ilitumika kufanya malipo kwa watuhumiwa. Je alitumiwa tu pesa za kigeni abadilishe au pesa zilikuwa za kwake za kufadhili mauaji hayo. Na je alijuwa fedha hizo zitatumika kwenye mauaji?. Wengine kwenye kuchomoka kwenye rufaa ni kazi.
Duh!
 
Lazima ufuatilie angalia jamaa yako mra ngapi ananitag ...sikia usipende shobo au nikuonyesha kwa kiasi gani anaitag kweny mijadala yenu...sina ushamba wala siwatambui.

Kaa pembeni sipendi shobo na kingereza cha ugoko..pita kushoto !!
Hii ni forum. Ukiandika ujinga ni lazima nikuonyeshe ulikokosea. Wala huna haja ya kunionyesha chochote. Kama kuna watu wanaku-tag huko hainihusu hata kidogo.
 
Hii ni forum. Ukiandika ujinga ni lazima nikuonyeshe ulikokosea. Wala huna haja ya kunionyesha chochote. Kama kuna watu wanaku-tag huko hainihusu hata kidogo.
Sasa Nan umuonye? Kuwa na adabu sipendi shobo.
 
Godfrey Salamba mzee wa Real Madrid
 

Attachments

  • Screenshot_20221205-162304.png
    Screenshot_20221205-162304.png
    284.4 KB · Views: 16
Back
Top Bottom