Uhusika wa waliohukumiwa kunyongwa kesi ya Lotter

Uhusika wa waliohukumiwa kunyongwa kesi ya Lotter

Mbona ile ya Lissu wahusika wote walisamehewa na mpaka na Kamera zikanyofolewa na yule muhusika aliesema atampiga Lissu Sindano za Sumu kapandishwa na cheo.
 
Namfahamu Makoi,asili yake Kibosho akimiliki maduka kadhaa ya madawa (Pharmacy) ingawa hata kidato cha pili hakumaliza.

Kupitia biashara zake za madawa alijikuta akipanda haraka haraka kibiashara kumbe nyuma ya pazia alikuwa na biashara nyingine.
Biashara/ Mafanikio yana siri sana.

Fatilia tu utajua
Mtu ana kiduka cha ajabu ajabu kesho yake mambo mengine kabisa
 
Inashangaza sana. Afu kuua mtu mmoja asiyekuwa na walinzi unashirikisha watu 11? watu wawili wangetosha na wasingejulikana....
walimuua ili iweje? mahama haijasema. kuna siri mkuu. wakisema walitumwa ni nani aliwatuma?
unajua kwanini Fahma Karama hajulikani alipo na huyo mchina? kweli hao jamaa hapo ukiwaangalia hawana conection kubwa mpaka kuua raia wa kizungu bila mtandao mkubwa hawawezi kushiri watu 11 kuua mzungu labda tuambiwe kati yao kuna majangili hapo.
 
Namfahamu Godfrey Salamba,baba yake ni marehemu Askari Trafic.

Alianza wizi mdogo mdogo akiwa na umri mdogo kati ya miaka 17 mpak 24.

Baada ya kuishi kwa Dada yake Late Mama Peter alikimbilia Shinyanga na kuunda genge la kuwapora wafugaji fedha hasa wanapotoka katika minada.

Baada ya mafanikio makubwa ya uporaji alijenga na kununua nyumba kadhaa Jijini Dar.

Mama yake kipindi chote akiishi maeneo ya Mwananyamala katika chumba kimoja.

Kabla ya hili tukio la mauaji tulionana maeneo ya Kaloleni Arusha akimiliki Toyota Land Cruiser 105.Alionekana ni mwenye harakati nyingi huku kila akiongea na simu ambazo hazikuwa za kawaida.Tulikuwa tukimkwepa sana kwakuwa zilikuwepo taarifa za uhakika katika Gari yake alikuwa na silaha na mavazi ya jeshi.

Godfrey mara kadhaa alikuwa akipata nafuu za kisheria kwakuwa marehemu Baba yake alikuwa ni Askari.Godfrey ni msukuma wizi/ ujambazi hauna kabila wala ukanda.
tupe picha yake mkuu mngogo, sasa alikodiwa au maana hapo kuna utata au nae ni Jangili.
 
Mkuu, kwenye Sheria Kuna kitu kinaitwa Kula njama.

Hata Kama muuaji alikuwa mmoja Ila Kuna kundi la watu ambalo liliandaa mchango wa kufanikisha mauaji. Sasa watu hawa ingawa hajaua physically Ila mchango wao kwa namna flani umechangia kufanikisha mauaji.

Nao wanastahili kufungwa Ila sidhani Ka ni sahihi wao kuhukumiwa kifo.

Mfano uyo dada Rahma inaweza kuwa hakufahamu Kama ushiriki wake ni kwenye ishu ya mauaji. Akijitetea vizuri na akapata wakili mzuri anaweza kutoka. Sababu kuwaandalia chakula wauwaji sio mpaka awafahamu anaweza akawa ameambiwa na Kaka yake Kuna wageni ni jamaa zangu wanakuja so andaa chakula ili wapate cha Kula.

Na kuhusu silaha alizoficha makaburini inaweza kuwa alipewa Tu na Kaka yake akamwambia fanya uzihifadhi hizi silaha Ila usiweke maeneo ya nyumbani. Japo anaweza kuhisi hizo silaha haziwezi kutumika Kwa Nia nzuri, Ila sio sababu ya yeye kuambiwa ameshiriki njama za mauaji moja kwa moja.
Hii kitu ya kula njama ndio inanifanya sitaki kuazima mtu simu apige sijui yake imesha salio.

Jana tu kuna dada kaniomba atumie namba yangu ya voda kupokelea hela zake. Nikamchana tu kuwa siwezi fanya mana likitokea lolote nimebebwa.
 
Ni heri wapewe kifungo cha muda mrefu kila mmoja kulingana na ushiriki wake hapo kuna mengi yatajulikana ila kuwanyonga kuna taarifa nyingi wataondoka nazo.
Afu huyo mchina ina maana hatambuliki hata kwa jina?
 
images.jpeg

Hivi "Malkia" yuko wapi?
 
Namfahamu Godfrey Salamba,baba yake ni marehemu Askari Trafic.

Alianza wizi mdogo mdogo akiwa na umri mdogo kati ya miaka 17 mpak 24.

Baada ya kuishi kwa Dada yake Late Mama Peter alikimbilia Shinyanga na kuunda genge la kuwapora wafugaji fedha hasa wanapotoka katika minada.

Baada ya mafanikio makubwa ya uporaji alijenga na kununua nyumba kadhaa Jijini Dar.

Mama yake kipindi chote akiishi maeneo ya Mwananyamala katika chumba kimoja.

Kabla ya hili tukio la mauaji tulionana maeneo ya Kaloleni Arusha akimiliki Toyota Land Cruiser 105.Alionekana ni mwenye harakati nyingi huku kila akiongea na simu ambazo hazikuwa za kawaida.Tulikuwa tukimkwepa sana kwakuwa zilikuwepo taarifa za uhakika katika Gari yake alikuwa na silaha na mavazi ya jeshi.

Godfrey mara kadhaa alikuwa akipata nafuu za kisheria kwakuwa marehemu Baba yake alikuwa ni Askari.Godfrey ni msukuma wizi/ ujambazi hauna kabila wala ukanda.
Jamaa alikua anapenda kukaa pale Picnic
 
Hii kitu ya kula njama ndio inanifanya sitaki kuazima mtu simu apige sijui yake imesha salio.

Jana tu kuna dada kaniomba atumie namba yangu ya voda kupokelea hela zake. Nikamchana tu kuwa siwezi fanya mana likitokea lolote nimebebwa.
usijaribu hiyo kitu mkuu ni hatari sana.

kuna bwanamoja miaka ya juzi nafahamiana nae tulifanya biashara akaniambia hiyo hela utamtumia huyu flani kwa M Pesa (ambaye mimi simjui) basi jioni nikatuma kwa simu yangu imepita kama wiki sita nikawa nilishasahau nikapigiwa simu na mwanamke mmoja akijitambulisha ananifahamu ni mwachuo wa chuo flani mimi nilikuwa mpenzi wake anaomba tuonane!

nikawa namkatalia ni ile kipindi cha watu wasiojulikana nikamjibu siku hizi kuna watu wasio julikana tunaongea kwa utani tu. tukaachana.

ikafika majira ya mchana akanipigia tena akitaka kujua mahali niliko maana pia nilimwambia niko busy sana safari hii anataka kunifuata kabisa!!!

bado nikamkatalia.

jioni nikapigiwa simu na namba ngeni sijui safari hii ni mwanaume akanisalimu akaulizia vifaa flani nikamwambia ninavyo akaniambia ofisi yako iko wapi kabla sijamjibu nikamwambia wewe nani amkupa namba akanitajia mahali ameipata. nikamwelekeza aje ofisini kwetu.

nikiwa nawasubiri nikawambia wahudumu wengine kazini "muda wowote mwana wa adamu atasalitiwa" nafsi ikawa inanienda mbio isivyo kawaida!

jamaa kaja na gari aina ya spacio yenye tinted kuangalia ndani kuna wanaume kama 5 Na mwanamke mmoja amekaa siti ya mbele ana mafile nikajua huyu ndio alikuwa ananisokota.

basi wakaniambia unamfahamu mtu anaitwa Flan wakanionyesha namba yake nikawambia hapana wakasema iandike kwenye simu yako upige kama italeta jina.
uzuri haikuleta jina.

wakaniambia mpigie umwiite hapa nikampigia katika kujieleza kumbe ananifahamu na hajui kama niko na polisi . nikawajibu polisi mimi nafanya kazu na watu wengi huenda ananifahm lakini mimi simfahmu nikaambiwa ulimtumia pesa siku flani na saa flani.

nikawambia labda huenda nilimtumia kwa sababu ya shunghli zangu lakini simkumbuki!

baadae wakaondoka wakaniachia namba yao ya simu kwamba nimwite alafu waje wamdake!

sasa nikaja nikakutana na watu kadhaa nikaambiwa katika kufuatilia kuna tawi la benk flani iliwahi kuvunjwa yeye akiwa anahusishwa! .
tuwe makini sana na mitandao pia na watu usio wafahaumu vizuri.
 
View attachment 2436384
Hivi "Malkia" yuko wapi?
Huyu mama namjuwa vzr sana

Tokea anamiliki Beijing restaurant wakati ule iko mitaa ya shoppers plaza mikocheni
Ni mwanamke wa dili sana,Ana mipango 10000 kidogo
Alafu alikujaga tz wakati ule wachina wanajenga reli,akabakia tz na akawa kama mkalimani wa wachina
Kuna dili alishanipaga hehe,aise nkachemsha mwenyewe
Vigogo wengi alikuwa amewashika
Sjui ma rpc na wengineo
Kuna wakati alikuwa mbioni kutoka sasa sijui kama ametoka au laaa
Ila nkifatilia naweza jua maana aliyekuwa dereva wake alikuwa mwanangu sana
Ila mwanamama huyu ni mtu wa mipango sana

Ova
 
usijaribu hiyo kitu mkuu ni hatari sana.

kuna bwanamoja miaka ya juzi nafahamiana nae tulifanya biashara akaniambia hiyo hela utamtumia huyu flani kwa M Pesa (ambaye mimi simjui) basi jioni nikatuma kwa simu yangu imepita kama wiki sita nikawa nilishasahau nikapigiwa simu na mwanamke mmoja akijitambulisha ananifahamu ni mwachuo wa chuo flani mimi nilikuwa moenzi wake anaomba tuonane!

nikawa namkatalia ni ile kipindi cha watu watu wasiojulikana nikamjibu siku hizi kuna watu wasio julikana tunaongea kwa utani tu. tukaachana.

ikafika majira ya mchana akanipigia tena akitaka kujua mahali niliko maana pia nilimwambia niko busy sana safari hii anataka kunifuata kabisa!!!

bado nikamkatalia.

jioni nikapigiwa simu na namba ngeni sijui safari hii ni mwanaume akanisalimu akaulizia vifaa flani nikamwambia ninavyo akaniambia ofisi yako iko wapi kabla sijamjibu nikamwambia wewe nani amkupa namba akanitajia mahali ameipata. nikamwelekeza aje ofisini kwetu.

nikiwa nawasubiri nikawambia wahudumu wengine kazini "muda wowote mwana wa adamu atasalitiwa" nafsi ikawa inanienda mbio isivyo kawaida!

jamaa kaja na gari aina ya spacio yenye tinted kuangalia ndani kuna wanaume kama 5 Na mwanamke mmoja amekaa siti ya mbele ana mafile nikajua huyu ndio alikuwa anisokota.

basi wakaniambia unamfahamu mtu anaitwa Flan h wakanionyesha namba yake nikawambia hapana wakasema iandike kwenye simu yako upige kama italeta jina.
uzuri haikuleta jina.

wakaniambia mpigie umwiite hapa nikampigia katika kujieleza kumbe ananifahamu na hajui kama niko na polisi . nikawajibu polisi mimi nafanya kazu na watu wengi huenda ananifahm lakini mimi simfahmu nikaambiwa ulimtumia pesa siku flani na saa flani.

nikawambia labda huenda nilimtumia kwa sabau ya shunghli zangu lakini simkumbuki!

baadae wakaondoka wakaniachia namba ya yao ya simu kwamba nimwite alafu waje wamdake!

sasa nikaja nikakutana na watu kadhaa nikaambiwa katika kufuatilia kuna tawi la benk flani iliwahi kuvunjwa yeye akiwa anahusishwa! .
tuwe makini sana na mitandao pia na watu usio wafahaumu vizuri.
Naomba uanzishe uzi kwa manufaa ya wengi.
 
Huyu mama namjuwa vzr sana

Tokea anamiliki Beijing restaurant wakati ule iko mitaa ya shoppers plaza mikocheni
Ni mwanamke wa dili sana,Ana mipango 10000 kidogo
Alafu alikujaga tz wakati ule wachina wanajenga reli,akabakia tz na akawa kama mkalimani wa wachina
Kuna dili alishanipaga hehe,aise nkachemsha mwenyewe
Vigogo wengi alikuwa amewashika
Sjui ma rpc na wengineo
Kuna wakati alikuwa mbioni kutoka sasa sijui kama ametoka au laaa
Ila nkifatilia naweza jua maana aliyekuwa dereva wake alikuwa mwanangu sana
Ila mwanamama huyu ni mtu wa mipango sana

Ova
fuatilia nakuaminia Mrangi. za chini chini alishatoka na yuko jiji la Hong Kong uchina kwao. kwani huyu ndio mfadhili wa kumuua mzungu eti Ngongo ?
 
Kwanza tujue Lotter ni nani na alikuws anafanya kazi gani. Hapa ndio tutajua motive ilikuwa nini? Wanaweza kumuua bila kutumwa pia kutegemeana na sababu ya kumuua.
Alikuwa mtetezi wa haki za wanyama na alikuwa anapinga ujangili katika mbuga na hifadhi

Sent from my SM-A217F using JamiiForums mobile app
 
Huyo Lotter alikuwa nani??
Lotter alikuwa ni one man army, mwanaharakati huru wa masuala ya meno ya tembo.

Kwa ufanisi wake wa kazi, aliogopwa na majambazi kuliko Usalama wa Taifa, Jeshi la TANAPA, Ikulu ya Magufuli, Jeshi la Polisi, Waziri Mkuu, Mkuu wa Mkoa, Uhamiaji mipakani, TRA Airport, na Usalama Bandarini, wote kwa pamoja na radio call zao za kushirikishana na mi Land Rover Defender yao na mibunduki na mi metal detector na mijela yao. Not fit for purpose.

Kifupi, Mzungu alikuwa anapinga machafu chafu ya nchi hii na anaumizwa na madhila ya mali asili za nchi yenu, na yuko effective and incorruptible kufuatilia masuala hayo, kuliko Rais wa nchi na raia wake milioni 60.

Ndo wakaamua kumuua.
 
Back
Top Bottom