Uhusika wa waliohukumiwa kunyongwa kesi ya Lotter

Uhusika wa waliohukumiwa kunyongwa kesi ya Lotter

Hadi sasa sijaona mahali panapoonesha mahakama inajibu swali la kwa nini wahusika wote hao wahusike kumuua mtu mmoja tu...

Je, wauaji ni majangili wa meno ya tembo?

Je, wauaji ni majambazi wanaochukua kazi za malipo za kuua watu?
 
Hiii ishu ni ishu watu walipewa kazi key suspect hajakamatwa ndio ana taarifa zote muhimu za kina nani alimtuma kumuua Lotter huyo Dada ushirika wake wa kupika na kuficha silaha umemmaliza ila yote wahusika wakuu sasa hivi wana amani na wanapata mvinyo na kusunya kidogo kwamba wamepona hao jamaa 11 watatawanywa magereza tofauti tofauti Ukonga, Maweni, Isanga, Uyui na Butimba.
 
Tatizo la hizi ishu zinaishia kwa Washiriki wadogo wa mwisho...kama hapo wanamaliza tu na hao Wauwaji.

Laiti kama watafuata chaneli mpaka wafike juu kabisa kwa Wahusika wakuu.
Issue zenye chain links zinazohusisha vigogo huwa zinafyeka wanyonge wengi sana ili ku clear any possible tracks,humo wengine hupewa adhabu ya kifo kwa kuwa tu wanamjua mhusika flani papa, huko Mexico wanaharakati wa mazingira wanauawa kila kukicha,mbaya zaidi wanaohusika na mambo hayo wengi ni viongozi wa serikali wanaoshirikiana na majangili wanaopora Maliasili hasa magogo na kuyauza kwa faida kubwa kwenye viwanda via ndani na nje ya Mexico,sasa hata hapa naona kama hiyo michezo inapiga hodi,kuna na helicopter ilishushwa huko mikumi miaka kadhaa nyuma,God forbid
 
Kuna wakaskazini hapa wafanya biashara pale Arusha, lakini mtasikia tu wakaskazini wanajua kubana budget mpaka wanapata pesa, waaapi..... Kuna mtu anajua kubana pesa kama Muhindi na Muha wa Kigoma? Watu ni majambazi, yaani kundi lote hili kumuua mtu mmoja tu tena siyo Raia kwa faida za ujambazi wao!!! Dunia hii
Sasa rasmi nimethibitisha pasipo shaka yoyote kuwa wewe ni mpumbavu, yaani pamoja na mwandishi kuandika kwa mtiririko mzuri kabisa ila wewe ulikuwa busy kutafuta jina lenye asili ya kaskazini ulipigie kambi?what a stupid creature?
 
Sasa rasmi nimethibitisha pasipo shaka yoyote kuwa wewe ni mpumbavu, yaani pamoja na mwandishi kuandika kwa mtiririko mzuri kabisa ila wewe ulikuwa busy kutafuta jina lenye asili ya kaskazini ulipigie kambi?what a stupid creature?
Shithole kbs huyu.kaskazin inamuwasha sana
 
Kuna wakaskazini hapa wafanya biashara pale Arusha, lakini mtasikia tu wakaskazini wanajua kubana budget mpaka wanapata pesa, waaapi..... Kuna mtu anajua kubana pesa kama Muhindi na Muha wa Kigoma? Watu ni majambazi, yaani kundi lote hili kumuua mtu mmoja tu tena siyo Raia kwa faida za ujambazi wao!!! Dunia hii
Una chuki na wivu wa kisichana.
 
Watuhumiwa 11 wamehukimwa na Mahakama kuu ya Tanzania kwa kumuua Wayne Lotter.

Ingawa mfadhili kuu wa kesi hii alikuwa Mchina , bado haijajulikana hakukamatwa au alikamatwa akawa deported. Mwingine Fahmi Karama alikamatwa lakini haijulikani yupo wapi, hata kwenye kesi hakuletwa Kama mtuhumiwa:.

Uhusika kwenye mauaji ya Lotter Ni Kama ifuatavyo:

1. Wa kwanza, Ismail Issa Machips yeye ndio alipewa dili na mchina na kutakiwa kutafuta hitman wa kumuua Lotter. Machips na huyo mchina walikutania Arusha. Kwenye kutafuta hitman akamuhusisha Makoi.

2. Wa pili ni Makoi, yeye alimtafuta Hitman baada ya kushirikishwa na Issa Machips. Na Makoi akapendekeza mtu anayeweza hiyo kazi ni Fahmi Karama. Hivyo Hawa wawili ndio chimbuko hasa la dili lote.

3. Wa tatu Rahma Mwinyi, yeye kazi yake ilikuwa kutunza silaha zilizotumika kumuua Lotter. Na silaha hizo alikuwa anaficha makaburini huko Temeke. Pia huyu Rahma aliingizwa kwenye hili dili na kaka yake Fahmi Karama na alikuwa saa zingine anawapikia msosi watuhumiwa wengine waliokuwa wanakuja hapo kwao Temeke.

4. Wa nne Chambiie Juma, huyu alikuwa dereva taxi kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa KIA. Na Marehemu Wayne Lotter alikuwa mteje wake alipokuwa akifika KIA au kuondoka KIA. Yeye ndio alitoa taarifa kwa wauaji kwamba Mr Lotter ameshapanda ndege na anaelekea Dar.

5. Wa tano, Allen Mafue. Huyu ameingia kwenye hi kesi Kama mfadhili wa mauaji. Yeye ndiye aliyewalipa kiasi Cha millioni 20 za kitanzania akina Karama na ongiste. Na aliwalipa hizo fedha kwenye bureau de change yake.

6. Wa sita Ayoub Selemani Kihoi, yeye kazi yake kubwa ilikuwa kuwafuatilia kwa ukaribu Lotter na mwenzake na kuwapa taarifa wauaji. So kazi yake ilikuwa ni kumonitor na kuwafatilia akina Lotter wanapotoka na kwenda siku hiyo ya mauaji. Na kuwapa attention wauaji wawe tayari.

7. Wa Saba ni Abou Omary mchingile, yeye pamoja na Kihoi walikuwa pamoja kumonitor taxi waliyoitumia akina Lotter na kutoa taarifa imefika wapi na inaelekea wapi ili wauaji wawe attention.

8. Wa nane, Michael David Kwavava, huyu ndio alikuwa dereva taxi wa Mr Lotter ndio aliyemtoa JKIA kumpeleka Baobab Village Masaki. Huyu dereva taxi alikuwa na mawasiliano na Fahmi Karama kabla siku ya mauaji hayajatokea. Na Fahmi alikuwa na mazungumzo naye kwa nusu saa kuhusu huo mpango wake.

9. Wa tisa ni Ndui mana ongiste raia wa Burundi. Huyu ndie aliyetekeleza mauaji kwa kumpiga Risasi Marehemu Lotter. Pia dereva taxi kwavara alimtambua kwenye identification parade iliyofanyika polisi, kwamba ndiye aliyefyatua risasi. Pia alikuwa akishirikiana na Fahmi Karama kwenye mipango yote.

10. Wa kumi ni Godfrey Peter Salamba, huyu ndio alikuwa dereva aliyewaendesha wauaji. Ndio alikuwa dereva wa gari lilobeba wauaji.

11. Wa kumi na moja Hibonimana Augustine Nyandwi, raia wa Burundi . Yeye ndiye aliyeleta silaha iliyomuua huyo Lotter na pia aliratibu mambo mengine ya kufanya mauaji hayo.

Kwenye hao wote wenye ahueni ya kukata rufaa ni wawili dereva taxi, maana mwanzoni kwenye kesi alikuwa Kama shahidi wa Jamhuri ila baadae ikagundulika naye alikuwa na mawasiliano na Karama. Na waliomtaja ni watuhumiwa wengine. Anaweza kubisha kwamba watuhumiwa walimtaja Kama kumkomoa baada ya kusema alimuona ongiste akimpiga risasi Lotter.

Mwingine ni Erick Mafue amabaye bureau de change yake ilitumika kufanya malipo kwa watuhumiwa. Je alitumiwa tu pesa za kigeni abadilishe au pesa zilikuwa za kwake za kufadhili mauaji hayo. Na je alijuwa fedha hizo zitatumika kwenye mauaji?. Wengine kwenye kuchomoka kwenye rufaa ni kazi.
Asante sana mkuu kwa mrejesho huu. Huyu Lotter bila shaka ni yule mzungu aliyeuawa Masaki kama sikosei. Kuna waliodhani kuwa alikuwa ameuawa na watu wa kitengo
 
Kuna wakaskazini hapa wafanya biashara pale Arusha, lakini mtasikia tu wakaskazini wanajua kubana budget mpaka wanapata pesa, waaapi..... Kuna mtu anajua kubana pesa kama Muhindi na Muha wa Kigoma? Watu ni majambazi, yaani kundi lote hili kumuua mtu mmoja tu tena siyo Raia kwa faida za ujambazi wao!!! Dunia hii
This is too low my dear. Try another method to relieve your frustration.
 
Ujambazi unatenda.nazungumzia kesi ambazo unaweza kuingia kwa bahati mbaya.kama hao wengine.kaua mmoja lakini adhabu ni moja.au unaunganishwa tu kwenye kesi ya ubakaji na hauusiki
Hata kesi za ujambazi sio poa Mkuu.

Ile kuvunja nyumba na kuiba hukumu zake zimechangamka.
 
Back
Top Bottom