usijaribu hiyo kitu mkuu ni hatari sana.
kuna bwanamoja miaka ya juzi nafahamiana nae tulifanya biashara akaniambia hiyo hela utamtumia huyu flani kwa M Pesa (ambaye mimi simjui) basi jioni nikatuma kwa simu yangu imepita kama wiki sita nikawa nilishasahau nikapigiwa simu na mwanamke mmoja akijitambulisha ananifahamu ni mwachuo wa chuo flani mimi nilikuwa mpenzi wake anaomba tuonane!
nikawa namkatalia ni ile kipindi cha watu wasiojulikana nikamjibu siku hizi kuna watu wasio julikana tunaongea kwa utani tu. tukaachana.
ikafika majira ya mchana akanipigia tena akitaka kujua mahali niliko maana pia nilimwambia niko busy sana safari hii anataka kunifuata kabisa!!!
bado nikamkatalia.
jioni nikapigiwa simu na namba ngeni sijui safari hii ni mwanaume akanisalimu akaulizia vifaa flani nikamwambia ninavyo akaniambia ofisi yako iko wapi kabla sijamjibu nikamwambia wewe nani amkupa namba akanitajia mahali ameipata. nikamwelekeza aje ofisini kwetu.
nikiwa nawasubiri nikawambia wahudumu wengine kazini "muda wowote mwana wa adamu atasalitiwa" nafsi ikawa inanienda mbio isivyo kawaida!
jamaa kaja na gari aina ya spacio yenye tinted kuangalia ndani kuna wanaume kama 5 Na mwanamke mmoja amekaa siti ya mbele ana mafile nikajua huyu ndio alikuwa ananisokota.
basi wakaniambia unamfahamu mtu anaitwa Flan wakanionyesha namba yake nikawambia hapana wakasema iandike kwenye simu yako upige kama italeta jina.
uzuri haikuleta jina.
wakaniambia mpigie umwiite hapa nikampigia katika kujieleza kumbe ananifahamu na hajui kama niko na polisi . nikawajibu polisi mimi nafanya kazu na watu wengi huenda ananifahm lakini mimi simfahmu nikaambiwa ulimtumia pesa siku flani na saa flani.
nikawambia labda huenda nilimtumia kwa sababu ya shunghli zangu lakini simkumbuki!
baadae wakaondoka wakaniachia namba yao ya simu kwamba nimwite alafu waje wamdake!
sasa nikaja nikakutana na watu kadhaa nikaambiwa katika kufuatilia kuna tawi la benk flani iliwahi kuvunjwa yeye akiwa anahusishwa! .
tuwe makini sana na mitandao pia na watu usio wafahaumu vizuri.