Uimara na udhaifu wa Mama Samia

Uimara na udhaifu wa Mama Samia

F-Merylin

Senior Member
Joined
Dec 26, 2016
Posts
128
Reaction score
177
Ndugu zangu badala ya kutoa ushauri naomba mniruhusu nimhukumu Mama Samia kwa hotuba zake na teuzi zake japo ni mapema saana kufanya hivyo. Ameanza vizuri kwa ujumla lakini inabidi ajue mapema uimara wake na udhaifu wake:

Uimara wake (strengths):
1. Alimtendea haki sana JPM wakati wa msiba wake. Alimheshimu sana na kuongoza mamilioni ya watanzania kumuaga. katika hili ana Alama A+

2. Uamzi wake wake wa "kuwapa" watu na vyombo vya habari uhuru wa kuongea kwa mujibu wa sheria ni jambo jema. Kuna wakati maafisa wa serikali walikuwa wanatafuta tu sifa kwa kutotenda haki. Katika hili Alama A.

3. Kuahidi kuendeleza nidhamu kazini na matumizi mazuri ya serikali na kuwatumbua wabadhilifu - Alama B (kwa vile ni ahadi tu).

4. Kujiamini na kufanya mabadiliko ya mawaziri na makatibu kwa vigezo vya 'ujuzi/ubobezi' wao - Alama A.
5. Kuahidi kuendeleza miradi mikubwa na midogo ya kimkakati - Alama B (Ahadi tu bado)

Udhaifu (weaknesses)

1. Kujaribu kuwafurahisha wawekezaji/Wazungu - Magufuli "was not a fool" hawa watu si wa kuchekea na kujirahishisha kwao. Kikwete alikuwa Rais mzuri sana lakini tuliishia kuwa na mikataba ya kinyonyaji sana. Anafanya makosa yale yale!

2. Kujaribu kuwafurahisha Wafanyabiashara - ataishia kukusanya mapato kiduchu na mengi yataishia mifukoni mwa TRA

3. Suala la Covid-19 - Kujaribu kuturudisha nyuma tulikotoka wakati tumefika mbali sana. Kwa nini tulizuia takwimu? Kwa nini tunakataa barakoa na chanjo zao? Je tiba zetu za asili azikutusaidia? Je sasa tufanye wazungu wanavyotaka? - Anakosea sana!

4. Kujivua wajibu wake kwa maamzi ya serikali iliyopita wakati yeye alikuwa mshauri mkuu wa JPM. - Uwezi kuwa juzi tu ulikuwa makamu wa Rais na leo unafanya U-turn ya mambo mengi ambayo ulikuwa sehemu ya maamzi yake.

5. Kutupa dalili kuwa tunarudi katika unyonge wa kuwapigia magoti wazungu na ile jeuri aliyotupa Mwl.JK na JPM ianze kupotea!

Siku nyingine:
Baadhi ya teuzi hazikuwa 'fair' au zilikuwa za kuumiza sana kwa wahusika. By the way "CCM inaongozwa na nani?" - Haya yatakuwa ya siku nyingine.
 
Mataga utapata tabu sana usipo kubali kubadilika. Falsafa nyingi za magufuki zilikuwa ni outdated! Hii ni Karne ya 21 moja! Ni karne ya Utandawazi! Ni kituko mtu upo kwenye karne ya 21, lakini mawazo yako yapo karne ya 20!

Karne ya akina Nyerere ya kuwaita Wazungu Mabeberu! Ni wakati sahihi sasa kusbirikiana na matifa mengine kwa manufaa ya pande zote mbili. Kunitenga na Dunia ya utandawazi, ni uwendawazimu wa kiwango cha ajabu!
 
Wako wengine wanao iendesha nchi hii nyuma ya pazia na baadhi tya matendo na maamuzi yanaonesha hilo.
 
Mama anahitaji kujua tunawaza nini kwa vile japo ni Rais awamu yake ni awamu inayoendeleza kile alichoahidi na mgombea mwenza wake JPM
 
Najua hali yako ni mbaya baada ya kuondokewa na yule bwana, subiri nchi irudishwe kwenye mstari nyoofu.
 
FYI bila ya Mwenyezi Mungu na Patners wake wazungu maisha yatakuwa kama Somalia!
Kumradhi jamani.
 
Sababu nyepesi sana hizi, tunataka tuone uimara na udhaifu wake katika maamuzi na utendaji wake. By the way uimara na udhaifu wa mtu unapimwa kwa matokeo , mpaka sasa ni mapema sana kuona matokeo.

Ningeambiwa mimi nipime uimara wake sasa, ningeampa 100% kwa sababu ningempima kwa dhamira na nia aliyonayo.
 
Mataga utapata tabu sana usipo kubali kubadilika. Falsafa nyingi za magufuki zilikuwa ni outdated! Hii ni Karne ya 21 moja! Ni karne ya Utandawazi! Ni kituko mtu upo kwenye karne ya 21, lakini mawazo yako yapo karne ya 20!
Ubeberu maana yake wizi! Kuiba ni kuiba hata kama ni kwa kutumia jina la 'uwekezaji' na kuwa 'modern' haina maana kukubali kuibiwa mchana kweupe. uhu sio 'usasa' bali 'ulofa'
 
Back
Top Bottom