Uimara na udhaifu wa Mama Samia

Binafsi najua Mwendazake ni kiongozi ambae amefanya mengi mazuri kwa ajili ya taifa lake hawezi kuwa perfect alikua na weakness lkn amejitahidi kwenye mengi nawajua binadamu huwezi kuwafurahisha makundi yote na wamejaa unafiki ataondoka mama simu moja Sasa hivi wanamsifu kwa kuachia Uhuru wa vyombo vya habari watakuja na agenda nyingine kumponda na kukashfu uongozi wake.This people they will never satisfy.Yesu nwenyewe alisalitiwa na wanafunzi wake Tena akiwepo na anashuhudia ,Mwendazake anasalitiwa baada ya kwenda zake , Gaddafi alifanya kila alichoweza lkn alionekana hafai na wakamsaliti huwezi kuja kuwaridhisha binadamu huwezi huwezi huwezi.
 
Usishindane nao lakini waonyeshe na wewe una akili na maamzi juu ya raslimali zako. sio waje wachote tu na watanzania wanyonge waishie kutopata service zozote na maafisa wa serikali wanufaike wenyewe! Ndio maana tulimpenda JPM alikuwa jiwe (maskini jeuri) kwa ajili ya watanzania na kafanya so much. Hapa tutakuwa legelege kwa wazungu na service kwa umma kama elimu na miundombinu vitakuwa historia pamoja na kujichekesha kwao!
 
Acha uoga wewe! Hii nchi itaendelea tu hata bila ya huyo magufuli wako.
 
Acha uoga wewe! Hii nchi itaendelea tu hata bila ya huyo magufuli wako.
bila shaka itaendelea. Iliendelea Sokoine alipokufa; Nyerere alipostaafu; na Mrema alipofukuzwa kazi na Sasa itaendelea tu! Lakini Mama asipoangalia unafiki na uroho wa wanasiasa waliokuwa wameficha kucha zao, basi JPM atakumbukwa na wengi kwa machozi yasiyoisha!
 
Hata wakati wake, bado hao wanasiasa wanafiki walikuwa ni wengi! tena kuliko wakati mwingine wowote ule! Kama ni kumpotosha, wamempotosha sana! Kiasi cha kusababisha watumishi wa umma tulio wengi, kumchukia kwa maamuzi yake ya kibabe na kikatili aliyo yachukua dhidi yetu, kwa nyakati tofauti.

Wanafiki wapo tu karne na karne! Kama unavyosema, anatakiwa kweli kuwa makini. Mimi ningemshauri awekeze zaidi kwenye ujenzi wa mifumo imara ya kiutendaji kupitia Katiba Mpya! Badala ya kupambana yeye kama yeye. Kwa sababu nchi itabakia milele! Ila sisi tunapita tu. Hata enzi za Magufuli, tulimtahadharisha kuhusu jambo hili, ila yeye alidhani ataishi milele.

Aliamini kwenye Tanzania ya Magufuli badala ya ile Tanzania yenye mifumo imara ya kiutawala. Mwisho wa siku, amekwenda zake katika mazingira ambayo hakuna aliye tarajia.
 
Nawalipa gharama za simu yao. Lakini wao wanataka kuchukua resources zetu kwa wizi.
Ndugu yangu, kaa na resources zako uone kama zitakusaidia. Suala si kuwachukia wazungu kwa sababu ndio watumiaji wakubwa wa hizo resources unazosema kwani kama ni kulaliana hata huku uswahilini ukizubaa waswahili wenzio wanakulalia tu. Kama alivyosema yeye Mama Samia, ukitaka kwenda mbali nenda na wenzio na ukitaka kufika haraka nenda peke yako na sisi tunahitaji kufika mbali hivyo ni lazima twnde na wenzetu. Waangale Wachina waliporuhusu uwekezaji lakini kwa uangalifu sana wameweza kuwa mshindani mkubwa wa Marekani. Hivyo basi hatupaswi kuwasideline wazungu ila ni kwenda nao kwa umakini tukijua tunataka nini na tutakipataje tunachotaka kupata toka kwao.
 

Muhaya wa hovyo! Muda wa kuchukia mataifa mengine ni wakati wa vita au kugombea uhuru. Sasa hivi hatuna vita na tuna uhuru karibia miaka 60 sasa.

Ni wakati wa kuinua national interests zetu. Huwezi kusema USA inagombea korosho, kahawa na pamba ya Tz. CCM wametuingiza kwenye mikataba iliyoua maslahi ya kitaifa, kama Magufuli alidhibiti hilo - Sasha nae afanye hivo. Tuache ujinga na chuki kwa wazungu wakati unataka waje kutalii upate pesa, unataka kuuza mazao yao kwao, unatumia teknolojia yao katika uzalishaji na mawasiliano.
 
Hatupo huru. Kuna neo colonialism since 1961.
 
Nonsense!

The obvious can not be proved!

Tatizo lako unawaza kizamanizamani hivyo huwezi kumuelewa mama yetu.

Acha mama aongoze nchi kwa umahiri wake. Usimpangie.

Uraisi wake hauna ubia na Magufuli. Magufuli alitawala bila kupangiwa na hakusikiliza ushauri wa mtu yeyote. Hatukumuingilia.

Unataka mama yetu asisikilize kilio cha walipakodi aendelee kudhulumu wafanyabiashara kama Magufuli alivyokuwa anafanya? Pathetic!

Kazi iendelee...
 
Mama anahitaji kujua tunawaza nini kwa vile japo ni Rais awamu yake ni awamu inayoendeleza kile alichoahidi na mgombea mwenza wake JPM
Kwa hiyo waliahidi pamoja kudhulumu wafanyabiasha kwa kuwabambikia kodi kubwa na kuwafungulia kesi za uhujumu uchumi na utakatishaji fedha?

Waliahidi pamoja kuzuia uhuru wa vyombo vya habari?

Mwacheni mama yetu aongoze nchi kwa kuzingatia misingi ya sheria na utawala bora kama alivyoanza. Hatutaki kutawaliwa kidikteta kama Magufuli alivyokuwa anafanya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…