Mkuu ni ukweli mchungu ila yeye ni Mfalme na familia yake ni ya Kifalme.
Sifa za kuwa mfalme ‘zina-evolve’ kutokana na mahali na muda, watu wa jamii husika ndiyo huamua mtu mwenye sifa zipi anafaa kuwa kiongozi wao na yupi hafai, Mfalme huyo atakuwa na mamlaka gani? Hilo ni wao kuamua hivyo hakuna sifa ‘fixed’ kuhusu sifa za Mfalme.
Ila nami nina imani kama yako kuwa ile taasisi ya kifalme imepitwa na wakati, haifai tena kuwepo pale.
Hizi si zama zile, kazi inazozifanya zinaweza fanywa na kiongozi yoyote mwenye kuchaguliwa na raia.