Uingereza haina utawala wa kifalme, kinachoendelea pale ni kiini macho

Hicho kitu wanaita constitutional monarch ni usanii mtupu. Walipoona wamepoteza uwezo wa kuendesha ufalme wakaanzisha hicho kufanya brain washing.
Hapa umesema kweli, ila zile sifa za kuwa mfalme kazisema nani?
 
Hakika
Kuhusu namna ya ufalme wa Uingereza tulifundishwa shuleni jinsi ulivyotofauti na Ufalme kama wa Eswatini nahisi wewe ulikua huingii darasani.
 
Kwa msingi huo ndio una ‘m-disqualify’ mfalme Charles III kutokuwa mfalme sababu tu hivi sasa hanazo sifa hizo?
Kwasasa yule sio mfalme bali yeye na familia yake ni watu wabinafsi wanaotumia wengine kuwa na mafanikio.
 
Sasa hivi imekuwa muda muafaka kuliongelea kwasababu ndio habari kubwa duniani.
Ni habari kubwa kwako. Lakin europe us na members wake hili wanalijua muda sana. Ndio maana huwasikii wakihangaika nalo.

Ni ww tu ndio unahangaika nalo. Nchi wanachama wana mambo ya muhim ya kufanya kuliko kupoteza muda kuhoji kwa suala dogo kama hilo
 
Kwasasa yule sio mfalme bali yeye na familia yake ni watu wabinafsi wanaotumia wengine kuwa na mafanikio.
Mkuu ni ukweli mchungu ila yeye ni Mfalme na familia yake ni ya Kifalme.
Sifa za kuwa mfalme ‘zina-evolve’ kutokana na mahali na muda, watu wa jamii husika ndiyo huamua mtu mwenye sifa zipi anafaa kuwa kiongozi wao na yupi hafai, Mfalme huyo atakuwa na mamlaka gani? Hilo ni wao kuamua hivyo hakuna sifa ‘fixed’ kuhusu sifa za Mfalme.

Ila nami nina imani kama yako kuwa ile taasisi ya kifalme imepitwa na wakati, haifai tena kuwepo pale.

Hizi si zama zile, kazi inazozifanya zinaweza fanywa na kiongozi yoyote mwenye kuchaguliwa na raia.
 
Hili sio suala dogo. US hawezi kuwahoji kwasababu hao ni washirika wake. Halafu raia wengi pale UK wanalihoji hili. Ni suala la muda kabla moto haujawaka pale.
 
Ufalme huo ume evolve kiujanjaujanja tu maana walishapiteza ile control ya kifalme. Walifanikiwa sana kuwa-brain wash watu wa UK kwa miaka mingi. Watu wamebakia na ile prestige tu lakini hawanufaiki na uwepo wao.

Kitu kinachokera zaidi ni kwamba kila mtu kwenye ile familia anaonekana special na anapata special treatment kuliko raia wengine. Hili ni jambo la matabaka ambalo linapingwa dunia nzima.
 
Hizo nchi zote head of state wao ni Mfalme wa Uingereza sasa utasemaje hana nguvu??
Nimesema anayo influence ya kidiplomasia kwa kiasi fulani. Nguvu kwenye hizo nchi ipo kwa wananchi wenyewe kupitia bunge na mahakama.
 
Sawa mkuu, lakini vigezo hapo juu vya mfalme hana. Ukiangalia vizuri hana mamlaka ya kuwafuta kazi hao uliowataja bila consent ya bunge au halmashauri ya kanisa la anglikana.
A naweza mfuta kazi waziri mkuu akitaka.
 
Hujui kwamba kuna tofauti kati ya Constitutional Monarchy and Absolute Monarchy. Anyway, tuongee ya kwetu kwani tunaumia sana na kodi nyingi ambazo hatuoni faida yake, serikali imekuwa msalaba kwa wananchi.
 
Huyo marehemu Malkia ndo anaamua nchi iende vitani au LA....... Yaani ndo mkuu WA majeshi
 
haikuwa sehem ya roman empire bali walitawaliwa kimabav na warumi , hlf akil yako inaonesha ww ni mvaa kobaz , hujui kuwa wenzetu huji update kuendana na muda
Acha jazba, huyo ni "mlokole" mwenzio.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…