Uingereza miaka kumi lakini bado Maimuna

Uingereza miaka kumi lakini bado Maimuna

Pwito

Senior Member
Joined
Mar 28, 2012
Posts
179
Reaction score
39
Wakuu naomba mnisaidie hivi unaweza ukaishi UK kwa miaka zaidi ya mitano na ukawa haujui Kiingereza? Maana jana kuna jamaa yangu anaishi UK-Liverpool amekuja likizo sasa nikakaa naye akatokea jamaa yangu mwingine nikamtambulisha sababu jamaa kasikia mjeba amejitundika huko muongo mmoja si akaangusha kwa Lugha yao mshikaji kujibu nikagundua loh!

Shida yangu sio kuona nini bali nashindwa kuelewa kama huko kwa wenzetu kuna mchanganyiko wa lugha. Nisaidieni maana kuna dada mmoja aliniambia akimaliza MBA yake hapa nchini anatafuta course UK angalau ya miezi sita ili ajibrashi hicho kilugha.

Msaada jamani hasa mlioko huko na mnipe ushauri je ni nchi au mji gani anaweza enda ambao hamna mchanganyiko wa lugha?
 
Sijui kama una akili hata kidogo kichwani mwako. Kwanza umekazana msaada msaaada, unaweza kuniambia ukipata hayo kajibu yatakusaidia nini maishani mwako?

Haya basi tuje kwenye swali lako ambalo nitalijibu kwa swali. Ukiishi Zanzibar miaka 20, hiyo ni guarantee kuwa utakuwa unajua kuogelea just because Zanzibar imezungukwa na maji?
 
Punguza povu mkuu anayeuliza ni kama hajui, kama nawewe ni mmoja wawenye tatizo labda uko huko lakini maimuna subiri wenye vichwa vyao watusaidie kilaza mwenzangu. Mimi nimesoma mpaka Master degree lakini bado broken wewe sijui ndo umeishi huko miaka 20 ndo kama mimi, nimesisitiza msaada ili isijeonekana kinyume kama unavyoona wewe. Napenda nipewe majibu chanya. Narudia tena jamani ni mji au nchi gani huko ulaya nitaondoa haya ma-broken language yangu pasipo kuenda darasani? Period
 
Mi namjua wa dada kama watatu hivi wa Tz wanaishi leicester miaka zaidi ya kumi na hawajui kuongea,barua mpaka wasomewe na marafiki.
 
Mi namjua wa dada kama watatu hivi wa Tz wanaishi leicester miaka zaidi ya kumi na hawajui kuongea,barua mpaka wasomewe na marafiki.

Asante mkuu, ila mimi nimelileta watuambie nini tatizo na tufanyeje ili tujikwamue angalau hii lugha ya biashara tuielewe haswa hawa wenzetu wanaopata kabahati kakuishi huko hata kwa miaka miwili tu.
 
Usiombe kukutana na ndugu zetu wanaokaa Milton Keynes
Yani kuna ndugu yangu ana miaka 12 huko, alienda kusoma
Toka alienda hajawahi hata kujaribu kujiandikisha chuoni!
Yani wamejijengea mazingira ya kibongo bongo wanajisahau

Ieleweke kua sio wote wako hivi, wengine wapo serious kiasi
Ila baadhi yao huko hawataki kujaribu integration yoyote yani
Kuna thread fulani alirusha mkuu Ritz kuyajadili haya mambo
Nadhani anaweza kutupa mwanga zaidi au kukumbusha link.
 
ila wazungu wana akili sana.
Unaweza kuta mtoto ana miaka miwili au mitatu,
hajaenda hata shule,
ila chokoza kingleza balaa!
Aongea ka maji!
 
Ni tatizo la kujisahau na kutojichanganya na wenyeji kisawasawa, kwamba ukiwa nyumbani lugha ni kiswahili na huendi hata kwenye park kucheza na watu wenyeji na kujifunza maneno mbalimbali.

Unapotaka kujifunza lugha ya kigeni inabidi ufanye jitihada kujifunza matamshi na kuyafanyia mazoezi sisi tunashindwa hasa kwenye grammar, kwamba mtu kuwa na uwezo wa kusema sentensi, maneno na mafungu ya maneno. Grammar inatawaliwa na sheria zake na mtu ukizifuata sheria hizi unaweza angalau kuzungumza kiingereza na ukaeleweka, ukasoma magazeti na majarida mbalimbali na kuangalia news.

Kwahio hata kama utaishi miaka 20 na kuendelea ilhali hufahamu namna ya kutamka maneno ya kiingereza na kuweza kujieleza kwa ufasaha basi wewe utaendelea kuzungumza kiingereza chenye kukosewa matamshi na maneno.

Ila kuna shule mbalimbali za kufundisha lugha hii ya kiingereza ingawa kwa asie mwenyeji inakuwa ngumu kuzifuatilia. Lakini Uingereza pekee ndipo penye mchangayiko wa lugha mbalimbali lakini kiingereza kikiwa lugha rasmi.

Kuna lugha za kigeni ambazo zimekubaliwa kutumika katika baadhi ya wilaya na miji mingine kama kisomali na Urdu ambayo ni lugha inayozungumzwa Pakistan.

Ila lazima tukumbushane ukiishi nchi za watu huna budi kuzungumza lugha yao na sio kubishana kwa makelele kwenye mabasi kwa lugha zenu kama wenzetu wanigeria na kutoa masauti makubwa, jambo linalowaudhi sana wenyeji.
 
Mkuu, kwanza pole kwa mkanganyiko ulioupata katika swala hilo ambalo hata mimi pia zamani lilikuwa linanisumbua. Kwa kifupi sana ukwel ni kuwa kuna baadhi ya maeneo ambapo watanzania ni wengi mfano Reading, sasa kuna tabia wengine huwa hawapendi kujichanganya na yawezekana kuna sababu nyingi za wao kutojichanganya yaani mara nyingi wanaongea kiswahili na hata mtindo wao wa maisha ni kama wa Tanzania kabisa na mtu anajisikia kuwa Tanzania zaidi badala ya kuwa uingireza kwa hali hiyo ni rahisi sana kupita mitaani esp.Reading kukuta watu weusi wanaongea kiswahili. Pia hii haimaanishi hawawezi kusikia ama kuelewa wengine wanaelewa lakini kukiongea ndo shida.
 
ila wazungu wana akili sana.
Unaweza kuta mtoto ana miaka miwili au mitatu,
hajaenda hata shule,
ila chokoza kingleza balaa!
Aongea ka maji!

Wewe kichwa maji kweli yaani mtoto kuongea kiingereza ana akili sana ? Mbona madogo wengi wanaongea kiswahili.
 
Wewe kichwa maji kweli yaani mtoto kuongea kiingereza ana akili sana ? Mbona madogo wengi wanaongea kiswahili.
hapa hadi wapelekwe akademia,
au kenya,
au uganda
anaishia kuongea kiganda
 
Sasa utajuaje Kiingereza ilhali hata kiswahili chakupa tabu..MAIMUNA maana yake ni nini? Ni MAIMUNA au MAAMUMA.!!?
Anayekwenda Uingereza ili imsaidie ajue kiingereza nae ni bure tu, kila kitu kinawezekana tu ukitilia mkazo..sisi wengine tumeishi hapa hapa TZ lakini kiingereza tukiongea kinaeleweka based on grammar and syntax. Kuna namna mbili ya kufahamu lugha ya kigeni
1. Ishi katika mazingira yao ukijifunza hyo lugha.
2. Soma sana vitabu vyenye lugha hiyo..kwa lugha nyingine inabdi uwe na muongozo wenye lgha yako.

Nilichojifunza mm ni kuwa sisi ni wavivu sana kwenye kusoma vitabu iwe kiswahili au kiingereza.
 
kwani we humuoni le mutuz...le baharia.....Malecela....

Natamani nimsikie na slang lake atakuwa hana lugha tu bali na swaga la lugha si unajua ukikaa uchagani lazima swaga lake ulipate swaga lake, maana mshikaji kamaliza umri wangu mamtoni yule
 
Punguza povu mkuu anayeuliza ni kama hajui, kama nawewe ni mmoja wawenye tatizo labda uko huko lakini maimuna subiri wenye vichwa vyao watusaidie kilaza mwenzangu. Mimi nimesoma mpaka Master degree lakini bado broken wewe sijui ndo umeishi huko miaka 20 ndo kama mimi, nimesisitiza msaada ili isijeonekana kinyume kama unavyoona wewe. Napenda nipewe majibu chanya. Narudia tena jamani ni mji au nchi gani huko ulaya nitaondoa haya ma-broken language yangu pasipo kuenda darasani? Period

Ukiwa na Masistas digiliii na bado hujui kuwa kuishi uingereza sio ndio kujua kiingereza basi wewe ni juha namba moja. Kiingereza unaweza kujua hata bila kwenda Uingereza. Kilaza ni wewe usiyeelewa hata kwa mifano.

Nimekwambia kukaa karibu na bahari pekee hakukufanyi uwe mvuvi bora, unless uwe umeshiriki uvuvi wenyewe. Hakuna jiji litakalokufanya ujue kiingereza wewe kapuku, kiingereza utakimudu kwa kukiongea mara kwa mara. Unaweza kujifunza kinyamwezi bila kwenda Tabora, foolish coconut.

Kaa usubiri majuha wenzio wakujibu majibu tofauti na haya ya kwangu. Ipo siku utadhani ukivaa nguo za Messi utajua kucheza mpira huku miguu yako yote ya kushoto kama ulivyo ubongo wako
 
Matatizo haya yapo kote duniani. Wapo wageni wengi hapa Tz ambao wameishi miaka mingi hapa lkn hawajui Kiswahili vizuri.
 
Mbona nilikuwa Berlin na Uholanzi na watoto hawajui Kiingereza?

Nilifika hadi juu kule Sweden, watoto wakanipa Hej hej? Na mie nikawaaga Hej Do!!!

Au hao siyo Wazungu? Ufaransa ndiyo kabisa na hasa hawa Nigga In Paris.....
ila wazungu wana akili sana.
Unaweza kuta mtoto ana miaka miwili au mitatu,
hajaenda hata shule,
ila chokoza kingleza balaa!
Aongea ka maji!
 
Mkuu, ni Maimuna na si Maamuma.

Lilikuwa ni Tangazo la shule ya Lugha kama sikosei miaka ya 80 mwishoni na dada akapokea simu (secretary) na alipoulizwa kama Boss yupo kwa Kiingereza, yeye akawa anajibu MAIMUNA.

Kutoka hapo ikawa kama hujui Kiingereza unaitwa Maimuna na ukichakachua cheti cha shule wanakuita KIHIYO.

Back
Top Bottom