Wakuu naomba mnisaidie hivi unaweza ukaishi UK kwa miaka zaidi ya mitano na ukawa haujui Kiingereza? Maana jana kuna jamaa yangu anaishi UK-Liverpool amekuja likizo sasa nikakaa naye akatokea jamaa yangu mwingine nikamtambulisha sababu jamaa kasikia mjeba amejitundika huko muongo mmoja si akaangusha kwa Lugha yao mshikaji kujibu nikagundua loh!
Shida yangu sio kuona nini bali nashindwa kuelewa kama huko kwa wenzetu kuna mchanganyiko wa lugha. Nisaidieni maana kuna dada mmoja aliniambia akimaliza MBA yake hapa nchini anatafuta course UK angalau ya miezi sita ili ajibrashi hicho kilugha.
Msaada jamani hasa mlioko huko na mnipe ushauri je ni nchi au mji gani anaweza enda ambao hamna mchanganyiko wa lugha?