Uingereza na Ufaransa wanaandamana kwa ugumu wa maisha, Lissu na CHADEMA changamkieni tenda ya kutengeneza Katiba Mpya kule

Uingereza na Ufaransa wanaandamana kwa ugumu wa maisha, Lissu na CHADEMA changamkieni tenda ya kutengeneza Katiba Mpya kule

Hello Wadau,

Binafsi naunga mkono Katiba Mpya ila siungi mkono Katiba Mpya ya kuondoa wahuni wa CCM na kuleta wahuni wa Chadema,nataka Katiba Mpya ambayo ni takwa la Wananchi na mda ndio utaileta watake au wasitake.

Baada ya huo utangulizi, Lisu na Chadema wamekuwa wanawadanganya watu kwamba Katiba Mpya ndio suluhisho na muarobaini wa matatizo Yao ya kiuchumi na kwamba Wao wanapigania Hilo Ili watu wapate neema.

Wamefika mbali wanasema maharage kuwa Juu ni sababu ya Kisiasa kwamba Katiba Mpya itatatua Ugumu wa Maisha, mfumuko wa bei nk.

Sasa huko Uingereza na Ufaransa kwenye Katiba Mpya na Bora watu Wanaandamana Kwa sababu za Ugumu wa Maisha uliosababishwa na mfumuko mkubwa wa bei za chakula na nishati kiasi kwamba uchumi ni mgumu.

Kwa kuwa kina Lissu na Chadema ndio mabingwa wa Katiba za kuleta Maisha Bora Kwa Wananchi,nitoe wito kwao wakachangamkie tenda huko Ufaransa na Uingereza au hata Kenya.

Za kuambiwa changanya na zako,kataa wahuni ogopa matapeli wa Kisiasa👇

Mtu yeyote asiyependa mabadiliko ya katiba iliyopo Tanzania aidha anafaidika kibibafsi na katiba iliyopo au ni mjinga mkubwa na hajui kwanini katiba mpya iwepo.
 
Mtu yeyote asiyependa mabadiliko ya katiba iliyopo Tanzania aidha anafaidika kibibafsi na katiba iliyopo au ni mjinga mkubwa na hajui kwanini katiba mpya iwepo.
Uzuri ni kwamba mabadiliko Huwa hayalaximishwi,yatakuja yenyewe Kwa wakati
 
Ni sawa tu na kusema maendeleo huwa hayalazimishwi yatakuja tu yenyewe. Kweli? Ndio maana Africa hatuendelei.
 
kweli nimeamini kuwa suala la ugumu wa maisha au kupanda gharama za maisha kama vile nafaka na bidhaa zingine ni suala la nchi zote duniani sio Tanzania pekee.
Mungu azidi kuwapa maono viongozi wetu ili tujinasue kwenye mkwamo huu.
 
Kungekuwa na katiba mpya watu wange andamana na suluhisho lingepatikana kwa sababu hakuna katiba mpya watu wanalala na njaa kama mtoa mada wanaugulia ndani kwa ndani. Basi endelea kufuatilia huko ulaya majibu ya suluhu watatoa kwa ajili ya huo huo mgomo ila si hapa bongo. Maadui ambao bado tunapambana nao mpaka leo aliotuachia mwalimu ni ujinga, maradhi na umasikini. Mtoa mada wewe ni ushahidi una ujinga, maradhi na umasikini;
Kwani katiba hii inakataza maandamano?
 
Mtu yeyote asiyependa mabadiliko ya katiba iliyopo Tanzania aidha anafaidika kibibafsi na katiba iliyopo au ni mjinga mkubwa na hajui kwanini katiba mpya iwepo.
Hao wajinga wakubwa wasiojua kwanini katiba mpya iwepo na wenye kujua kwa nini katiba mpya iwepo unadhani ni kundi gani ndio wako wengi?
 
Afrika hata tuletewe katiba iliyotungwa na Malaika huko mbinguni haiwezi kutusaidia chochote amini nakuambia.
Tatizo la Africa lipo kwa watu wake wenyewe ambao wana Sifa zifuatazo:

1. Uvivu
2. Njaa
3. Umasikini
4. Wizi
5. Kutowajibika

NASEMA HIVYO KWA SABABU HATA HII YA SASA INA MAMBO MAZURI AMBAYO HAYAFUATWI mfamo mzuri alivyoingia rais wa ajabu hapa nchini Hayati JPM. Hata ukichagua nani lazima atupige tu
kweli kabisa hasa kutowajibika uvivu wa watawala na wizi ni hatari
 
Hii ipo Wazi kabisa MKUU. Watanzania ili wabadilike ni lazima waache hayo uliyo yaorodhesha.

Hawa pendi kujituma ila wanapenda Fedha. Unamwajiri Kijana Anakuja kazini SAA 4 wakati wewe boss SAA 11 Alfajiri umeshafika ofcn Alafu ndio wakwanza kulalamika kuongezewa mishahara.
sio watanzania wote sema watawala wa kiafirika watu binafusi mbona wanasimamia miladi yao vizuli tu
 
Afrika hata tuletewe katiba iliyotungwa na Malaika huko mbinguni haiwezi kutusaidia chochote amini nakuambia.
Tatizo la Africa lipo kwa watu wake wenyewe ambao wana Sifa zifuatazo:

1. Uvivu
2. Njaa
3. Umasikini
4. Wizi
5. Kutowajibika

NASEMA HIVYO KWA SABABU HATA HII YA SASA INA MAMBO MAZURI AMBAYO HAYAFUATWI mfamo mzuri alivyoingia rais wa ajabu hapa nchini Hayati JPM. Hata ukichagua nani lazima atupige tu
Nakubaliana na wewe lakini sijui kama hiyo ni order of priority. Kama ndio, ningependa kuona namba 5 ndio inakuwa moja. Mleta mada anashindwa kujua kuwa hayo maandamano ni kutafuta uwajibikaji sisi kwetu kuwajibika ni kuacha kazi au madaraka. Kwa wenzetu kuwajibika ni kurekebisha hali kwa kubadili mifumo, vipimo, sheria/taratibu nk. Ni watu wa aina ya mleta mada watakopungua au kukosa ngu ndipo tutaona matatizo yetu yatamalizwa na sisi wenyewe - kama anawaza Lissu na Chadema waende ufaransa, hapa kwetu nani atakuja??? Hawezi kujibu hili.
 
Back
Top Bottom