Uingereza wamebaki na hifadhi ya Gesi ya Wiki moja tu huku Tanzania majadiliano ya Mradi wa LNG yakichukua mwaka wa 4 sasa hayajakamilika

Lord denning

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2015
Posts
15,819
Reaction score
33,255
Kusema ukweli kuna muda huwa naamini nchi yetu imerogwa. Au ilishawahi kurogwa huko nyuma.

Tangu vita vya Ukraine kuanza Gesi imekuwa bidhaa adhimu na ya thamani sana duniani.

Mataifa mbalimbali yenye Gesi yalichangamka kuanza uzalishaji na yale yanayozalisha yalizalisha zaidi na kutengeneza matrilioni ya fedha kama faida.

Kwa akili za kawaida tu kama Taifa ambalo tuna gesi nyingi, kipindi hiki ndicho tulitakiwa hata kuja na mpango wa mwendokasi wa kuhakikisha tunaanza uzalishaji na uuzaji wa Gesi (LNG) ili kupata faida kubwa kama wanayopata sasa mataifa ya Nigeria, Saudi Arabia, Qatar na Urusi.

Taarifa zilizotolewa jana zinasema kuwa Taifa na Uingereza limebakiwa na hifadhi ya Gesi ya kutumika si zaidi ya wiki moja tu, hivyo endapo Tanzania tungekuwa tunazalisha na kuuza Gesi hiki ndo kipindi tungekuwa tunapiga hela kweli kweli.

Cha ajabu sasa! Hadi leo hatujui mazungumzo ya mradi wa Gesi yalifikia wapi? Ni kama timu za majadiliano zina enjoy kulipwa posho hivyo hazitaki kuharakisha majadiliano suala linalofanya majadiliano kuchukua miaka na miaka ili wajumbe wa timu hizo walambe maposho ya uhakika kwa ajili ya matumbo yao.

Ni mwaka wa 5 sasa tangu tuambiwe nchi yetu iko kwenye majadiliano na hadi sasa hatujui yamefika wapi huku wenzetu wakiendelea kutumia fursa ya mgogoro wa Urusi kutengeneza faida kubwa kutokana na mauzo ya gesi huko duniani.

Tanzania tuna laana na inabidi tutubu kweli na kuomba rehema za Mungu atuondolee hii laana.
Screenshot_20250111_113459_YouTube.jpg
 
@mods nisaidie kurekebisha heading. Sio wiki mbili ni wiki moja tu
 
View attachment 3198480
Nahisi tatizo ni negotiators wetu wanataka cha juu kikubwa sana hivyo wanakwamisha mchakato.
 
Mungu awasaidie na janga la kukosa gas
 
Nahisi tatizo ni negotiators wetu wanataka cha juu kikubwa sana hivyo wanakwamisha mchakato.
Timu ya negotiation inajua wanachokifanya.

Majadiliano yanavyozidi kuchukua muda mrefu ndo faida kwao maana wanazidi kuongeza muda wa kuendelea kula maposho yao.

Ngozi nyeusi tuna laana fulani nakwambia. Endapo huu mradi ungekuwa umesha take off muda huu Tanzania tungekuwa tunazungumza habari ingine kabisa kiuchumi.
 
Tanzania bado wanafikiria waleje wao kwanza matumboni yawe yanashibaaa kila sekunde.
 
Gesi Gani tena..........!

Mbona tuliambiwa gesi yote tulishanyang'anywa na mabeberu na wao ndo watajua wanauza au wanagawa Bure......!
 
Back
Top Bottom