Uingereza yaichimba mkwara Kremlin

Uingereza yaichimba mkwara Kremlin

Watoto wa mwaka 2000s hao,hawajui unyama wa Uingereza kwenye medani ya Vita na fitna.
Nakumbuka miaka ya 1980 alimchapa Mu Argentina wakigombea visiwa vya Falklands. Kumbuka ukubwa wa Taifa la Argentina lakini walichapwa vizuri tu. Any way huko nyuma sana sijui historia yao UK. Wakongwe zaidi watatuingiza darasani.
 
Nimejikuta nacheka mno mpaka machozi baada ya kusoma kauli ya UK Deputy Chief of Defence Staff Rob Magowan isemayo
"Uingereza ipo tiyari kuingia vitani na Urusi usiku wa leo endapo kama Russia itaivamia Ulaya Mashariki.

View attachment 3159183
“Britain is ready to engage Russia tonight if Russian troops invade Eastern Europe” .

What a joke 😂😂
Achana na UK bro Wana Nguvu za Giza za ajabu nimekumbuka vita Yao na Argentina....!
Putin anawajua😇😇
 
Russia ndio ilikua core ya soviet baad ya kuvunjika walibaki na vitu vingi sana kijeshi .technologia .siraha zingine ndo izo zime enda kutupwa kama chuma chakavu apo ukraine
Niwaka wa 3 sasa anahangaika na Ukraine.
 
Kwenye top 10 ya mataifa yenye nguvu kijeshi UK inazidiwa hata na South Korea. Ni moja ya mataifa yenye nguvu ila kwa Russia, UK ni mdogo sana. Russia kijeshi inalinganishwa na USA.
Kuna wakati aliekuwa waziri wao mkuu aliwahi kuitisha.Russia,Lavrov akamwambia ukithubutu tu wataifuta nchi inayoitwa Uingereza duniani
 
Was***ge tu Hao hawana jipya Kwa sasa Putin Kesha waambia wafunge Midomo kama ni wanaume kweli wamvamie kama ambavyo walivyo Fanya Kwa Saddam na Gadaffi tuone ,

Wamemjaza upepo zelensky kuwa watamuunga na jumuia ya NATO mwenzao anapigwa mpaka Leo hii wamebaki kumtazama Tu what a foolish kama kweli hawa waogopi Russia wakati Russia anaivamia Ukraine kwanini wasingefanya haraka haraka kumuunganisha zelensky ktk huo umoja wa NATO ili Russia Atakavyo ipiga Ukraine wapate kumchangia ni nini wanacho kuogopa haswaa!?
Maswali Mujarrabu kabisa
 
Kwanza uwe unaacha aya ukiandika. Kisha wewe na wasiojua wenzio mzingatie kwamba Soviet Union iliingia mkataba wa kutopigana na Ujerumani (Molotov-Ribbentrop Pact) wa mwaka 1939 kuepusha kupigana ndani ya miaka 10 inayofuatia.

Soviet Union au Urusi kama underdog akashirikiana na Ujerumani kuivamia Poland. Wakaigawana, mwaka huo Ujerumani ikavamia Belgium na ndipo Uingereza ikatangaza vita dhidi ya Ujerumani. Ujerumani ilikuwa inaiogopa sana Uingereza ila ikalazimika iingie vitani. Walipigana miaka mitano ila huo udogo wa Uingereza mnaosema hakuna mwanajeshi wa Ujerumani hata mmoja alitia mguu Uingereza. Hiyo ndio Britain usiyoijua.

Uingereza ikaingia front kupigana kuikomboa Ufaransa na Belgium, baadae Marekani akaja. Miaka hiyo Urusi ikaivamia Finland ikateseka kushinda vita, Ujerumani baada ya kuona Warusi ni wachovu ikawavamia ili iwashinde faster faster maana Waingereza hawapigiki. Then majeshi ya Ujerumani yakaingia Urusi hadi kidogo kuichukua Moscow walifika within 20km, sio mtego wa Urusi ni uwezo mbovu. Warusi zaidi ya 20 million walikufa unasemaje ni mtego.

Allies wakiongozwa na Marekani wakatoa msaada mkubwa sana wa ndegevita, chakula, mafuta, vifaru, malori kwa Soviets kupigana ili wasishindwe na Ujerumani. Wakati huo wao wakipigana Western front. Bila msaada wa allies Urusi alikuwa mnyonge mbele ya Ujerumani ile.

Urusi ilivamiwa na Ujerumani hivyo ilibidi ipigane haukuwa msaada ilikuwa lazima, Uingereza hata haikuvamiwa na iliombwa na Ujerumani haitaki shida ila ikaingia nayo vitani. Urusi ni coward aliyekumbatia wahuni kwenye Molotov-Ribbentrop Pact ili wasimpige, na wakampiga akaja saidiwa na wenye nia njema.
Umeongea kishabiki sana na umeubadilisha ukweli kukidhi fantasy yako uliyoaminishwa kwamba RUSSIA ni taifa maskini lisilo na uwezo wowote.Kasome vizuri historia ya vita vya pili vya dunia halafu jisahiishe wewe mwenyewe.Hauwezi kuondoa ukweli wa kwamba Soviet Russia walikuwa ni washirika muhimu sana na wenye nguvu kwenye allied forces. Kukumbusha tu sehemu kubwa ya Europe wajerumani walipita nayo kama wako tour.Hao UK kilichowasaidia ni hali yao ya kuzungukwa na bahari , na kwamba nguvu kubwa sana Hitler aliziweka kuishinda URUSI na msaada mkubwa wa ndege za kivita za USA ambao ulikuwa unawanyima fursa wajerumani kuvusha majeshi yao kutoka France kuja pwani za UK. Ila ukweli unabaki hali ya UK ilikuwa mahututi sana ,maana wajerumani waliwaponda sana kwa kuwaangushia mabomu kutoka kwenye ndege.Bila dedication ya USA air force kuwazuia wanajeshi wa ujerumani kukatisha British chanel basi UK alikuwa kaishajichokea kwa kipondo.Ukweli utabaki Ujerumani ya vita vya pili ilikuwa ina nguvu kweli kweli.
 
Vijana bana hivi hujui UK ilitawala karibu nusu ya dunia kwa karibu karne nzima?

Vijisiwa vidogo tu lkn hata Marekani, Canada na Australia waliziachia na kuzipa uhuru!

Hiyo potential haijaisha na vita ni pesa na strategies sio maombi na viapo
Kishindo cha wakoma kimesikikaa dunia nzima....ni swala la kuwaambia Ukraine warushe tena Stomshadow.
 
Vita ni pesa uchumi wa Urusi unaingia mara 2 kwa uchumi wa Britain, acheni kuota ndoto, huyu General wa UK sio mpumbavu kama hapo kijiweni mtogole eti hajui Urusi ina uwezo gani akachimba mkwara tu km kimbwa koko cha hapo jalalani kwenu! Mashabiki wa vita mnadhani ni yanga na simba hii
Hapana, hapana, hapanaaaa... Na wewe ni shabiki tuu kama wengine. Russia is a giant in another level! Ikiwa TU, Russia ana Nuclear weapons kuzidi NATO wote, unapata wapi ujasiri wa kusema eti Britain peke yake ana msuli wa kumkabili Russia, ACHENI MAHABA deal with reality!
 
UK hawezi kuimudu vita na Russia wanajifariji kama Zelesky na kutegemea NATO
Huu ndio ukweli wenyewe.
Kuna watu wanasema eti watu hawaijui UK katika masuala ya vita.
Sasa NAMI najiuliza nao hawaijui Urusi katika masuala ya vita?
Urusi ambae ni mbabe wa WWIi
Urusi ni taifa la vita,hapo ulaya wanajaulikana kwa maisha Yao ya vita.
 
Back
Top Bottom