Johnny Sack
JF-Expert Member
- Jan 21, 2017
- 9,504
- 20,293
Sagal Abdi-Wali aliapishwa Jumatatu kama mbunge wa Chama cha Labour katika Bunge la Uingereza, huku akiweka mkono wake juu ya Quran wakati wa kula kiapo. Anatajwa kuwa mbunge wa kwanza mwenye asili ya Somalia katika historia ya Uingereza.
Abdi-Wali, ambaye aliwasili Uingereza akiwa mtoto mkimbizi kutoka Somalia, alisema ushindi wake ulikuwa pigo kwa "wale wanaotaka kutugawanya".
"Tuna jukumu la kulinda kile tulichokijenga na kukirithisha kwa wengine," alisema baada ya kushinda uchaguzi mdogo katika jimbo la Holborn na St Pancras, katikati mwa London, siku ya Ijumaa.