Uislamu haujakataza asiye muislamu kula mchana wa ramadhani, siungi mkono wasio waislamu kuzuiwa kula mchana

Mungu pekee ndo anajua imani ya mtu.
Kula mbele ya mwenzio wakati unajua. Amefunga ni dharau
Hicho ndio kipimo cha imani

Utajuaje kama imani yako ni thabiti ikiwa hupatwi na majaribu?
 
Mungu pekee ndo anajua imani ya mtu.
Kula mbele ya mwenzio wakati unajua. Amefunga ni dharau
Kwani mke wako anpompikia mtoto wa miaka minne huwa anapatwa na tamaa ya kula?

Au maandalizi ya msosi wa kufuturu si huwa yanafanyika kabla ya muda wa kufuturu, sasa kama wanaweza kujizuia katika mazingira hayo kwanini washindwe pindi wakiona watu wengine wanakula?
 
hakuna anayeshindwa kujizuia.
Ila sio ustaarabu kula mbele ya mtu aliyefunga
 
hakuna anayeshindwa kujizuia.
Ila sio ustaarabu kula mbele ya mtu aliyefunga
Unavyosema sio ustaarabu ni kama kitendo cha mtu kula ni aina fulani ya uchafu kitu ambacho nakiona sio sahihi

Umelifanya tendo la mtu kula lionekane sawa na mtu anapojisaidia mbele za watu

Kama unaweza kujizuia sioni sababu ya wewe kutamani pindi anapokula mwingine, kwasababu hata huyo mtoto ukimpikia sidhani kama utamfungia chumbani ale usiwe unamuona
 
Kula mbele ya mwenzio wakati unajua. Amefunga ni dharau
Turudi katika msingi wa imani Mtume anasema..

"Hakika matendo yanahukumiwa kutokamana na nia.."

Kama mimi nakula mbele ya aliyefunga na nia yangu ni kula kuna tatizo gani ?

Lakini pia kusema kwamba ni dharau huu ni muono wako tunauheshimu,lakini kuna ambao hawaoni kama ni dharau kula mbele ya aliyefunga na huu ni muono wao unatakiwa uuheshimu pia.

Kila mmoja ana maoni au muono wake usitake watu waheshimu muono wako tu.

Alafu mafundisho gani yanayosema kwamba kula mbele ya mtu aliyefunga sio ustaarabu ?

Kwa sababu kula ni kitendo chema katika uislamu,na kufunga ni kitendo chema katika uislamu.

Kwa hivyo mimi nikila mbele ya mtu aliyefunga kunakuwa na ubaya upi au dharau zipi ?
 
Kwahyo leo hii wakristo wa Italia wakiweka sheria hakuna kula hadharani wakati wa kwaresma utaona wametenda haki ?

mbona hakuna tabu ikiwa ni ndani ya nchi yao.
Tatizo la wazungu hua ni wanafiki sana, Hujifanya wanataka kuachia uhuru wa kila kitu lakini mwisho wa siku inapokuja kuhusu uislamu wanaanza kupindisha taratibu zao
 
Sheria lazima ziheshimiwe.

Hata tunachokisema ni kwaba uislamu haujakataza popote watu kula mchana wa ramadhani kwa wale ambao hawalazimiki kufunga.

Hizo sheria zimeekwa Zanzibar, na wenyewe wazanzibari hawana tatizo nazo kabisa. Wanaolialia ni huku bara. Yani kwa kifupi wao wanatamani kule kuwe kama hapa kwao. kila baada ya nyumba mbili Bar
 
Hizo sheria zimeekwa Zanzibar, na wenyewe wazanzibari hawana tatizo nazo kabisa. Wanaolialia ni huku bara. Yani kwa kifupi wao wanatamani kule kuwe kama hapa kwao. kila baada ya nyumba mbili Bar
Hoja yangu ni kuwa sheria hizo zisinasibishwe na uislamu waweke wazi kwamba uislamu haujakataza ila wao ndio wamekataza.

Umeelewa mkuu ?
 
Unaposema 99 ni waislamu hiyo 1% hawana haki ya kula mchana wakati ilikuwa waachwe tu kwa sababu hiyo 1% haina madhara yoyote hata wakila mchana itaonekana kana kwwmba wote wamefunga tu ?

Mkuu 1% ni ndogo sana kwenye nchi, na kikawaida watu kama hao hua wameathieika kabisa na mila za hizo dini zenye majority. Wakristo wa Zanzibar wapo tofauti kabisa na wakristo wabara, wengi wao ni kawaida hata kuwaona na baibui na mitandio wamejivisha, Wameathirika sana na mazingira ya kiislamu kiasi ambacho hicho ambacho munakiona tatizo kwao sio tatizo kabisa, Mana toka mababu zao huo ndio mfumo wa maisha Kule Zanzibar. Nahilo si kwa zanzibar tu nchi zote zenye high majority za kiislmau ndio tartibu zake, Nchi za kiarabu zipo zinaishi kwa taratibu hizo.
 
Asalaam Aleykum ndugu zangu waislamu nawatakia kila heri kwenye funga yenu...Tanzania yetu ni moja, imani za dini zisitugawe.
 
Hoja yangu ni kuwa sheria hizo zisinasibishwe na uislamu waweke wazi kwamba uislamu haujakataza ila wao ndio wamekataza.

Umeelewa mkuu ?

Ni kweli mkuu, Ila Pia hakuna kosa kwenye kujaribu kuprotect mazingira ya Jamii au Dini yasiathiriwe kupitundukia.

Na kama kufuata sheria hasa za uislamu, Wakristo wasingeweza kabisa kuishi kwenye Ardhi za waislamu.
 
Ni kweli mkuu, Ila Pia hakuna kosa kwenye kujaribu kuprotect mazingira ya Jamii au Dini yasiathiriwe kupitundukia.
Ukisema hivi maana yake uislamu haukujua kwamba watu kula mchana kunaweza kukaharibu dini,so watu wameona sasa kula mchana kunaweza kuharibu dini jambo ambalo sio sahihi mkuu.

Na kama kufuata sheria hasa za uislamu, Wakristo wasingeweza kabisa kuishi kwenye Ardhi za waislamu.
Sio kweli mkuu,mtume aliishi na wqsiokuwa waislamu muda mwingi sana na yeye ndiye alikuwa mbora na kinara wa uislamu.

Uislamu tukiusoma kwa mazingatio ya ndani hauna complications kama tunazozileta sisi.

Angalia kama mtume alikataza waislamu wakiwa vitani wasiwauwe wakristo kwenye nyumba zao za ibada badala yake wadeal na wale wanaopigana nao,vipi uislamu huu unaomlinda mkristo wakati wa vita ushindwe kumpa mazingira ya kumlinda katika wakati ambao sio wa vita ?
 
Ni sawa sio tatizo mimi nakubali.

Hoja yangu ni hii..

Hao 1% waachwe huru atakae atakula chumbani kwa hiari yake,atakae ataenda mgahawani ale kama kawaida yake.

Hata kama sheria zinawekwa hoja yangu ni kuwa isinasibishwe kwamba sheria hizi ni za kiislamu.
 
Hii mada haijaletwa kwa mlengo wa Kuelimisha waislamu

bali imeletwa na muhisika kwa mlengo wa kujipendekeza kwa Makafiri

Sent using Jamii Forums mobile app
Kabla ya kuandika uzi huu nilitegemea pia maoni kama haya kwa sababu waislamu shida yetu ukiongea jambo la kurekebisha vilio kama hivi huwa ni vingi

Almuhiiim vilio hivyo havina athari yoyote kwangu.
 
Nilichogundua hapa kuna watu wanajibu maswali kwa mihemko pandizi, kuna mdau amepandisha hadi hiyo poster ya tarehe 18/03/2022 inayohusu tourists lakini watu wameiacha wanajibizana kwa fujo na hasira 😂😂😂
 
Kabla ya kuandika uzi huu nilitegemea pia maoni kama haya kwa sababu waislamu shida yetu ukiongea jambo la kurekebisha vilio kama hivi huwa ni vingi

Almuhiiim vilio hivyo havina athari yoyote kwangu.
Swali fupi tu la kumuuliza huyo anaedai unajipendekeza kwa kwa makafiri je uislamu umemkataza msafiri, mgonjwa, wanawake walio kwenye siku zao, wazee na watoto wadogo kula mgahawani mchana wa siku ya ramadhani?
Ajabu ni mtu huyohuyo anaempiga bakora mkristo anaekula mchana wa ramadhani baada ya kuisha tu mwezi wa Ramadhani nae anazini, analewa, anaiba, anavuta bange na hakuna hukumu yoyote ambayo waislamu wenzake wataitekeleza juu yake hali ya kua anafanya maasi ya waziwazi.
Dini inahitaji elimu na hikma,
Haya mambo ya jazba jazba ndio yanapelekea wasio waislamu kuzidi kuuchukia uislamu kutokana na upumbavu unaofanywa na baadhi ya waislam.
Rejea kisa cha bedui aliekojoa mbele ya msikiti wa mtume ï·º
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…