Uislamu unamkataa Sheikh aliyehamasisha kukata vichwa. Masheikh wenzie walaani

Uislamu unamkataa Sheikh aliyehamasisha kukata vichwa. Masheikh wenzie walaani

Bani Israel

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2016
Posts
2,284
Reaction score
4,595
Naituma kama nilivyoipokea kutoka jukwaa la masheikh.

Nitamrekebisha shekh aliesema watu watakatwa (vichwa) na kuzungumzia wakristo kama ndio njia ya ukosefu wa amani
Hakuna shekhe, kiongozi, au mtu yeyote aliyepewa ruhusa na Allah kusimamisha uhai wa mtu au kukataza jambo kwa kutumia njia ya vitisho kwa umma.

Uislamu uko wazi kabisa:

“mwenye kuua nafsi isiyo na hatia nikama ameua watu wote.”
(Qur’an 5:32)

Hivyo:
Haihalalishwi kukata vichwa
Haihalalishwi kushambulia watu
Haihalalishwi kuchochea damu kwa sababu za dini, siasa au tofauti ya mawazo
Haihalalishwi kuuana kwa sababu kuna maandamano

Uislamu unakataza kuchochea chuki kati ya dini nyingine.

Mtume ﷺ aliishi na Mayahudi, Wakristo, na makabila mengine bila kuwafanyia uadui.

Katika Qur’an, Allah amesema:

“Wala msibishane na Watu wa Kitabu isipokuwa kwa njia iliyo bora.”

(Qur’an 29:46)

Huyo shekhe aliposema “machafuko yanafanywa na Wakristo” ni kueneza chuki ya kidini, jambo ambalo Uislamu haliruhusu kwa sababu:

linavunja amani

linawagawa wananchi

linazalisha uadui na kuuwa watu wasio na hatia

halina dalili za kisharia

Na kuhusu wito wa kuchinja au kukata vichwa misikitini ni haramu

Mtume ﷺ amesema:

“Mwenye kumwambia watu: muuweni, si miongoni mwetu.”

(Hadith Sahih)

Na pia akasema:

“Muislamu ni yule ambaye Waislamu wengine wameokoka kutokana na ulimi wake na mkono wake.”

(Bukhari & Muslim)

Kwa hiyo, mtu anayewaita Waislamu wachukue panga na wawe tayari (kukatakata) watu:

anataja haramu

anaeneza fitna

anaenda kinyume na mafundisho ya Mtume

sio busara wala si sehemu ya dini

Hata kama ni shekhe — hakuna mtu yuko juu ya sheria ya Allah.

Je vipi kuhusu Maandamano na siasa si kigezo cha kupigana

Katika Uislamu:

Ikiwa serikali imekataa maandamano wananchi wanatafuta haki kwa njia ya amani, sio kubeba silaha. Hapo ni salama.

Ikiwa kuna dhulma bado haikupi ruhusa ya kuuana kiholela.

Mtume ﷺ aliishi wakati wa dhulma nyingi sana hakuwahi kuamrisha (kuchinja) watu.
Kwa hivyo… yale maneno mliyosikia kutoka kwa shehe hayana msingi wa Kiislamu

Kwa muhtasari:

✔ Uislamu unakataza kuchochea vita

✓uislam unakataza maandamano yenyevurugu na uvunjifu wa amani.

✔ Uislamu unakataza chuki kwa Wakristo au dini nyingine

✔ Uislamu unakataza kutishia kuuana

✔ Uislamu unalinda amani ya taifa

✔ Uislamu unakataza kuchukua sheria mkononi

Kuhubiri mauaji kwa jina la dini ni kosa la Kiislamu, la kiutu, na la kisheria.

Ushauri kwenu kama ndugu zangu waislam:

Usifuate maneno ya mtu anayechochea damu.

Fuata Qur’an na Sunnah, sio hasira za watu.

Muislamu anajulikana kwa akili, hekima, na upole, sio kwa panga.
 
Yaani itikadi zake binafsi na wenzake wanaofanana anataka ziwe za dini nzima.

Dhulma anayoitetea ataishuhudia kwa jicho kavu.
Anatuchafulia Sana
 
IMG-20251120-WA0017.jpg
 
Kwanza ningetaka kuuliza mpaka ufike kuwa shehe unapitia hatua zipi?
 
Hivi kawaida kwa kauli ile si alitakiwa akamatwe na kushtakiwa? Yaani mtu anaongelea kuchinja watu na life inaendelea tu fresh😳😳
 
Naituma kama nilivyoipokea kutoka jukwaa la masheikh.

Nitamrekebisha shekh aliesema watu watakatwa (vichwa) na kuzungumzia wakristo kama ndio njia ya ukosefu wa amani
Hakuna shekhe, kiongozi, au mtu yeyote aliyepewa ruhusa na Allah kusimamisha uhai wa mtu au kukataza jambo kwa kutumia njia ya vitisho kwa umma.

Uislamu uko wazi kabisa:

“mwenye kuua nafsi isiyo na hatia nikama ameua watu wote.”
(Qur’an 5:32)

Hivyo:
Haihalalishwi kukata vichwa
Haihalalishwi kushambulia watu
Haihalalishwi kuchochea damu kwa sababu za dini, siasa au tofauti ya mawazo
Haihalalishwi kuuana kwa sababu kuna maandamano

Uislamu unakataza kuchochea chuki kati ya dini nyingine.

Mtume ﷺ aliishi na Mayahudi, Wakristo, na makabila mengine bila kuwafanyia uadui.

Katika Qur’an, Allah amesema:

“Wala msibishane na Watu wa Kitabu isipokuwa kwa njia iliyo bora.”

(Qur’an 29:46)

Huyo shekhe aliposema “machafuko yanafanywa na Wakristo” ni kueneza chuki ya kidini, jambo ambalo Uislamu haliruhusu kwa sababu:

linavunja amani

linawagawa wananchi

linazalisha uadui na kuuwa watu wasio na hatia

halina dalili za kisharia

Na kuhusu wito wa kuchinja au kukata vichwa misikitini ni haramu

Mtume ﷺ amesema:

“Mwenye kumwambia watu: muuweni, si miongoni mwetu.”

(Hadith Sahih)

Na pia akasema:

“Muislamu ni yule ambaye Waislamu wengine wameokoka kutokana na ulimi wake na mkono wake.”

(Bukhari & Muslim)

Kwa hiyo, mtu anayewaita Waislamu wachukue panga na wawe tayari (kukatakata) watu:

anataja haramu

anaeneza fitna

anaenda kinyume na mafundisho ya Mtume

sio busara wala si sehemu ya dini

Hata kama ni shekhe — hakuna mtu yuko juu ya sheria ya Allah.

Je vipi kuhusu Maandamano na siasa si kigezo cha kupigana

Katika Uislamu:

Ikiwa serikali imekataa maandamano wananchi wanatafuta haki kwa njia ya amani, sio kubeba silaha. Hapo ni salama.

Ikiwa kuna dhulma bado haikupi ruhusa ya kuuana kiholela.

Mtume ﷺ aliishi wakati wa dhulma nyingi sana hakuwahi kuamrisha (kuchinja) watu.
Kwa hivyo… yale maneno mliyosikia kutoka kwa shehe hayana msingi wa Kiislamu

Kwa muhtasari:

✔ Uislamu unakataza kuchochea vita

✓uislam unakataza maandamano yenyevurugu na uvunjifu wa amani.

✔ Uislamu unakataza chuki kwa Wakristo au dini nyingine

✔ Uislamu unakataza kutishia kuuana

✔ Uislamu unalinda amani ya taifa

✔ Uislamu unakataza kuchukua sheria mkononi

Kuhubiri mauaji kwa jina la dini ni kosa la Kiislamu, la kiutu, na la kisheria.

Ushauri kwenu kama ndugu zangu waislam:

Usifuate maneno ya mtu anayechochea damu.

Fuata Qur’an na Sunnah, sio hasira za watu.

Muislamu anajulikana kwa akili, hekima, na upole, sio kwa panga.

Huyu ndiye kiongozi wa dini. Mimi siyo muislam lakini maingiliano yangu katila mazingira mbalimbali na waislam, kamwe siwezi kuamini kuwa uharamia ni mafundisho ya dini ya kiislam.

Jamaa yangu alienda Uturuki, waislam wale wa Uturuki walipojua kuwa ni mkristo, wakamchukua na kumtembeza maeneo mbalimbali ndani ya Uturuki yenye historia ya ukristo, mkumbuke kuwa Efeso, Collosai na Galatia, zote zipo Uturuki. Huko ndiko alienda mtume Paulo kuhubiri injili ya Kristo, kisha akaenda Korinto, ambayo leo inaitwa Corith, ipo kama 10km toka mji wa Anethens, Ugiriki. Yule rafiki yangu akiwa Uturuki, jamaa wale waislam ambao hakuwahi kuwajua kabla, walimtoa hotelini, wakaishi naye nyumbani kwao. Aliporudi Tanzania, akaniambia kuwa kama wema ule walionionesha ni kwa sababu ya uislam, basi wacha waendelee na uislam wao.

Muislam anayeuishi uislam halisia na mkristo anayeuishi ukristo, kamwe hawawezi kugombana wala kuuana. Haya yaliyopo BAKWATA, yanayohamasisha chuki, ni mashetani yaliyojificha kwenye viunga vya uislam, lakini hawamchi Allah, kamwe.
 
Huyo ndio Sheikh anayeelewa anachokiamini,wale wengine wahuni tu
 
Back
Top Bottom